Home Ustaadh Khamis Al-Ghamawi

Ustaadh Khamis Al-Ghamawi

Published By Ust. Abu Muslim

Ameuliza Akhy Salmaan Shaan kuwa Ibadhi wana mtazamo gani kuhusu ukhalifa wa Othman bin Affan ???

JAWABU: Bismilaahi Rahmaani Rahiim

mtazamo wa madhab ya Ibadhi ni kuwa Athman bin Affan ni sahaba wa Mtume s.a.w. khalifa muongofu wa tatu na mkwe wa Mtume s.a.w. aliyeozeshwa mabinti wawili wa Mtume kwa kufuatana. naye ni katika waliosilimu mwanzo, familia yake ni familia ya kwanza katika uislam wakaelekea Ethiopia, aliandaa sehem kubwa ya jeshi katika vita vya Tabuuk, naye ndiye mnunuzi wa kisima mashuhuri madina .

alichaguliwa na waislam na alitawala vizuri kwa miaka sita bila ya tatizo kisha ukamzidia uzee na mapenzi kwa jamaaa zake, hilo likapelekea hao jamaa zake hasa Mar wan bin Alhakam  kuingilia mambo ya dola na kuharibu kwa miaka sita ya mwisho yautawala wake, naye ni Binadam na yale ya wema aloyafanya yanatupa pumzi za kuona usafi wa niya yake, yaa leiti jamaa zake wasingemuharibia dola yake kwa matendo yao yasiyo ya uadilifu.

kwa Mtazamo huu Ibadhi imepita msimamo wa kati na kati baina ya Mashia wenye kumlani na kutomtaka kabisa, na Masuuni wenye kumtakasa na kila kosa kama kwamba yeye ni malaika aliyekingwa na makosa.

Rejea: Al madkhal fii Fiqh l Ibaadhy uk 10 – 25, Liqaat maa Sh, Alkhalily malngo wa mtazamo wa kiibadhi kwa khalifa Ally na Othman, Alkhawaarij wal haqiiqat l ghaaibah.

TANBIIHI:

Baadhi ya wana tarekhe wa kiibadhi – kama walivyo wa madhehebu zingine –  wana rai zao binafsi kuhusu suaa hili la Othman lakini misimamo yao hiyo haiwakilishi rai ya pamoja ya madhehebu ya kiibadhi,

maibadhi wasio na Ujuzi wanaatazwa kuzungumzia masuala haya hasa yanayohusu fitna ya zama za masahaba ili kuepusha kueneza ya uongo mwingi yaliyozushwa katika kadhia hii na wanalizimishwa kujipamba na qauli ya ALLAH Mtukufu ” huo ni ummah umeshapita wana yao waliyoyachuma nanyi muna yenu wala hamutoulizwa yale waliyokuwa wakiyafanya” 2:134

 

Published By Ust. Abu Muslim

Ameuliza Akhy Salmaan Shaan kuwa Ibadhi wana mtazamo gani kuhusu ukhalifa wa Othman bin Affan ???

JAWABU: Bismilaahi Rahmaani Rahiim

mtazamo wa madhab ya Ibadhi ni kuwa Athman bin Affan ni sahaba wa Mtume s.a.w. khalifa muongofu wa tatu na mkwe wa Mtume s.a.w. aliyeozeshwa mabinti wawili wa Mtume kwa kufuatana. naye ni katika waliosilimu mwanzo, familia yake ni familia ya kwanza katika uislam wakaelekea Ethiopia, aliandaa sehem kubwa ya jeshi katika vita vya Tabuuk, naye ndiye mnunuzi wa kisima mashuhuri madina .

alichaguliwa na waislam na alitawala vizuri kwa miaka sita bila ya tatizo kisha ukamzidia uzee na mapenzi kwa jamaaa zake, hilo likapelekea hao jamaa zake hasa Mar wan bin Alhakam  kuingilia mambo ya dola na kuharibu kwa miaka sita ya mwisho yautawala wake, naye ni Binadam na yale ya wema aloyafanya yanatupa pumzi za kuona usafi wa niya yake, yaa leiti jamaa zake wasingemuharibia dola yake kwa matendo yao yasiyo ya uadilifu.

kwa Mtazamo huu Ibadhi imepita msimamo wa kati na kati baina ya Mashia wenye kumlani na kutomtaka kabisa, na Masuuni wenye kumtakasa na kila kosa kama kwamba yeye ni malaika aliyekingwa na makosa.

Rejea: Al madkhal fii Fiqh l Ibaadhy uk 10 – 25, Liqaat maa Sh, Alkhalily malngo wa mtazamo wa kiibadhi kwa khalifa Ally na Othman, Alkhawaarij wal haqiiqat l ghaaibah.

TANBIIHI:

Baadhi ya wana tarekhe wa kiibadhi – kama walivyo wa madhehebu zingine –  wana rai zao binafsi kuhusu suaa hili la Othman lakini misimamo yao hiyo haiwakilishi rai ya pamoja ya madhehebu ya kiibadhi,

maibadhi wasio na Ujuzi wanaatazwa kuzungumzia masuala haya hasa yanayohusu fitna ya zama za masahaba ili kuepusha kueneza ya uongo mwingi yaliyozushwa katika kadhia hii na wanalizimishwa kujipamba na qauli ya ALLAH Mtukufu ” huo ni ummah umeshapita wana yao waliyoyachuma nanyi muna yenu wala hamutoulizwa yale waliyokuwa wakiyafanya” 2:134

 

Published By Ust. Abu Muslim

Swali: Je Mtume s.a.w. alikuwa dhehebu gani ??

JAWABU: Madhehebu ni njia ya kuifahamu dini ya uislamu aliokuja nayo Mtume Muhammad s.a.w., Hivyo Mtume s.a.w ndiyo muendewa na ni kutokana na kuzifahamu qauli zake ndiyo zimekuja njia nyingi za kupita yaani madhehebu

Hivyo yeye ni asili ya kila dhehebu na kiongozi mkuu wa kila dhehebu, maadam madhehebu hayo yanafuata haki kwa dalili bila ya taassubi na ushabiki. Kasema Allah mtukufu kumwambia Mtume s.a.w. “Kisha tukakuweka juu ya njia ya haya mambo, basi ifuate wala usifuate matamanio ya wasiojua kitu”

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI: Ibadhi wana mtazamo gani kuhusu ukhalifa wa Ally bin Abii Taalib na ule wa Muawiya na Yazidi na Hassan na Hussein ?

JAWABU:

Ally bin Abii Talib ni khalifa wa nne wa uongofu ambaye ummah ulikubaliana juu yake kwa kumchagua baada ya kuuwawa kwa Khalifa Athman bin Affaan. Alijiuzulu ukhalifa alipolikubali wakati wa kuiandika sulhu baina yake na Muawiya. Pia aliuzuliwa ukhalifa kwa ittifaaq ya Amru bin Al aas na Abii Musa Al ash’ary ittifaaq ambayo yeye Khalifa Ally aliiridhia kabla ya kutokea kwake.

Waislam masahaba wasomi na waadilifu walimchagua sahaba Abdullah bin Wahb Arrasiby awe kiongozi wa waislamu baada ya kuuzuliwa huko, hivyo IBADHI wapo pamoja na Ally bin Abii Talib mpaka alipojiuzulu hapo hushikamana na Abdullah bin Wahb Arraasiby.

Muawiya na Banii Umayya kwa ujumla ispokuwa zama za Umar bin Abdi l Aziiz si ukhalifa bali ni ufalme wa kidhalimu, nao ndio asili ya kila itikadi potofu ziloingia katika Ummah huu, na ni kutokana nao ndio vimepatikana vipote viovu na potofu na chanzo cha tawala za kibabe zilizokuwepo na zilizopo katika nchi za kiislamu.

HASSAN NA HUSSEIN

Amma Hassan yeye alichaguliwa na wafuasi wachache wa baba yake wala ummah haukukubaliana juu ya ukhalifa wake, zzaidi ya hayo yeye mwenyewe alimuachia huo ukhalifa mtawala dhalimu Muawiya bila ridhaa ya waliomchagua

IBADHI inawakubali makhalifa wote wanne waongofu, na ipo mbali na ukhalifa wa kijamaa, kikabila, kikoo, … n.k.

Rejea: Swafahaat Mushriqah cha Majid Alkindy.

wassalaam alykum warahmatullah wabarakaatuhu.

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Endapo mtu ana mke wake wameoana lakini ikabainika kuwa yule mume hazai, baada ya hapo yule mwanamke akaenda katika maabara ya kisasa huko Ulaya akatiliwa  spam akapata ujauzito, Je huyu Mwanamke atakuwa amezini? Je wakiwa wale spam ni wa mume wake, lakini kaingizwa kwa njia ya sindano je kuna hukmu gani katika uislamu ?

JAWABU:

A. Kwa hakika Allah mtukufu amemnyanyua mwanadamu na kumtukuza, akamuwekea kizazi kwa taratibu njema, ili kuitukuza nasaba yake na hadhi yake, Amesema Allah mtukufu

وهو الذي خلق من الماء بشرا فجعله نسبا وظهرا وكان ذلك قديرا”

” Naye ndiye aliyeumba viumbe kutokana na maji kisha akamuwekea nasabu na ushemeji, na mola wako ni mlezi”

Na moja ya njia hizo za kupata uhalali na starehe ya kimwili ni kwa kuoana.Hivyo hiyo itakuwa ni moja ya njia za uzinifu. Amesema Samaahat Sheikh Alkhalily – Allah amuhifadhi – ” Jambo hili litapelekea kuchanganyika kwa nasabu na kuharabika kwa mafungamano ya kifamilia na kuharibika mafungamano ya watu, na jambo hili linafanana na kuhalalisha Zinaa”

Na mfano wa swali hili ni lile aliloulizwa Mufti wa Zama zetu Sheikh Ahmad Alkhalily – Allah amuhifadhi – kuwa ikiwa mbegu za mume zimehifadhiwa na akatiwa mwanamke baada ya kufa kwa mme kwa njia ya kupandikiza – sindano – nini Hukmu yake?

Akajibu : ” Mafungamano ya kindoa humalizika kwa kufa mmoja wa wanandoa, kwa msingi huu mwanamke kuchukua mimba kwa mbegu zilizohifadhiwa za mumewe aliyekufa ni aina miongoni mwa aina za zinaa” Fataawa Tibb cha samahaat Sh.Alkhalily uk. 292

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Nini hukmu ya kusoma kitabu cha Barzanji katika Mawlid ?

JAWABU:

Maulamaa wetu- Allah awarehemu- wamekataza kusoma hicho kitabu cha Barzanji kwa kuwa ndani yake  kuna itikadi mbovu za;

MOJA: kuamini shafaa ya kutolewa motoni watu waovu waliokufa bila ya kutubia, nayo ni kupinzana kwa wazi na kauli ya Allah mtukufu isemayo:

ولا يشفعون إلا لمن ارتضى

” Na hawatomuombea yoyote ispokuwa aliyeridhiwa na Allah mtukufu” 21:28

فإن الله لا يرضى عن القوم الفاسقين

” Na hakika Allah mtukufu hawaridhii watu mafasiqi” 9:96

PILI: Itikadi ya kuonekanwa Allah mtukufu huko Akhera, nayo inapingana kwa wazi na kauli yake Allah mtukufu :

“لا تدركه الأبصار وهو يدرك البصار…”

” Macho hayamfikii – hayamuoni – Allah mtukufu lakini yeye anayafikia macho..” 6:103

TATU: Uwepo wa mambo mengi ambayo hayajithibiti katika taarekh na historia kwa ujumla, bali yapo ya uongo hasaa.

NASAHA: Ikiwa hapana budi kusoma basi kisomwe kitabu cha ALNASH AT ALMUHAMMADIYAH au ANNUR ALMUHAMMADIY vya Imaam Abu Muslim Albahlaaniy – Allah mtukufu amridhie -.

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Je inajuzu kukusanyika kwa ajili ya kutukuza mazazi ya Mtume s.a.w. kama ilivyozoeleka katika maeneo mengi?

JAWABU:

Hakuna katazo wa amri ya kufanya hivyo hasa ikiwa hakuna jambo linalokhalifu misingi ya kisheria, na kwa hivyo maulamaa wametofautiana baina ya wnye kujuzisha na kukataza na wenye kuruhusu kwa masharti maalumu.

Na linalofanyiwa kazi na kutolewa fat wa kwa maulamaa wetu – akiwemo Al Imaam Abu Muslim Albahlaany r.a. na Al imaam Almufassir Sh. Ahmad Alkhalily ni kuwa HILO LINAJUZU pamoja na kutovuka mipaka ya kisheria inayohusu mikusanyiko.

hivyo vizuri na bora isomwe siira ya Bwana Mtume s.a.w. na kuelekezana katika tabia njema, na kunasihiana katika yenye kuleta umoja na udugu baina yetu.

Published By Ust. Abu Muslim

000007 - SIMU KWA MCHUMBA

SWALI:

Sheikh wangu, nina maswali haya:

1. nini hukmu ya kuongea na mwanamke ajnabiyyah – anayeweza kumuoa?

2. Je akiwa ni mchumba wake na walii wake amemruhusu kuongea naye?

3. vipi ikiwa wanaongelea mambo ya dini?

Tunataraji jawabu yenye kututosheleza.

JAWABU:

1. Amma kuongea na mwanamke ajnabiyyah katika simu bila ya haja au dharura hiyo ni katika khul wa, kama ambavyo hilo la maongezi linaweza kuleta fitna – bali linaleta fitna katika uhakika wake –

( HIVYO HILO JAMBO LIPO KARIBU ZAIDI NA KUKATAZWA KULIKO KURUHUSIWA )

2. Kuwa kwake ni mchumba wake, hakumpi ruhusa hiyo wala haizingatiwi hiyo ruhusa ya walii wake, na ajabu ya walii huyo…! Na ikiwa hapana budi kuongea iwe ni pamoja na uwepo wa MAHRAM wake.

3. Ikiwa kuna dharura au haja ya kuongea huko ikiwa ni kwa dini, biashara, masom0 n.k. basi wajipambe wanawake na Qauli ya Allah mtukufu:

“فلا تخضعن بالقول فيطمع الذي في قلبه مرض وقلن قولا معروفا”

” Basi msizishushe na kuziregeza sauti zenu, akapata tamaa yule mwenye maradhi katika moyo wake, na semeni kauli za wema” Ahzaab:32

TANBIIHI:

Tusisahau vitimbi vya shetani, wala tusijipe uhuru wa kuikaribia na kuikaribisha Zinaa, Amesema Allah mtukufu:

” ولا تقربوا الزنا إنه كان فاحشة وساء سبيلا “

” wala msiikaribie zinaa, hakika huo uzinifu ni uchafu na njia mbaya ya kupita” Israa :32. Wallaahu aalam.

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Nini hukmu ya kuzitengeneza ndevu?

JAWABU:

Kizuri ni kile kilichoitwa kizuri na sheria, Je kutengeneza vizuri imekusudiwa kuzipunguza au kuzichana?

Ikiwa ni kuzipunguza ndevu basi huko ni kuziharibu sio kuzitengeneza, kwa kuwa ni kwenda kinyume na Qur an na Hadithi za wazi za Mtume s.a.w.

Amesema Allah mtukufu kuwa Ibliis amesema:

(( ولآمرنهم فليغرن خلق الله….))

” Na nitawaamrisha wayabadilishe maumbile waliyopewa na Allah mtukufu”  Annisaa: 19

Na pia Qauli ya Mtume s.a.w. ” Ziwacheni ndevu na punguzeni masharubu”

Amma ikiwa ni kuzichana basi hilo halikatazwi kisheria, bali ndiyo litakiwalo  na lihimizwalo. uislam ni usafi wa ndani na nje. Washukran.

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Assalam alykum warahmatullah wabarakatuhu, naomba kuuliza: Msafiri aliyetoka sehem moja kwenda sehem nyingine kimasomo mfano Tanzania kwenda Algeria kimasomo, Je mtu huyu inafaa kwake kula mchana wa Ramadhani kule aliko. naomba jawabu ndugu zangu waislam

JAWABU:

Atakujibu Allah mtukufu katika kitabu chake pale aliposema :

” وأن تصوموا خير  لكم …”

” Ikiwa mtafunga basi hilo ni kheri kwenu” Wallahu aalam.

Published By Ust. Abu Muslim

Ni zipi sababu za kisheria za kutokufunga  Ramadhani ?

JAWABU:

Sababu za kutokufunga ramadhani kisheria zipo aina mbili, nazo ni:

KUWEPO KWA VIZUIZI VYA FUNGA, navyo ni HEDHI, NIFASI NA JANABA. Amma janaba inatakiwa akoge kabla ya kuchomoza kwa jua, kwa Qauli ya Mtume s.a.w.

من أصبح جنبا أصبح مفطرا

Atakayepambazukiwa na Alfajiri hali ni mwenye janaba, atapambazukiwa hali hana saumu” imepokewa na Imaam Rabii kutoka kwa Abii Hurairah r.a.

Pia Hadithi ya Ummu Salama na Bii Aisha – mama wa waumini – kuwa amesema : “tulikuwa tunafunga na kusali tukiwa katika siku zetu, na tunaamrishwa kulipa saumu zetu na hatuamrishwi kulipa sala zetu” Ameisahihisha Imaam Rabii katika musnad yake na wameipokea wengine kwa lafdhi tofauti kidogo.

SABABU YA PILI: UDHURU WA KISHERIA nao ni:

1. maradhi ambayo mtu hawezi kufunga kwa uzito wa maradhi hayo, kwa kumzidishia maradhi au kumletea kifo, ikiwa ni maradhi yasiyopoa kabisa basi atalisha kila siku ya Ramadhani maskini mmoja. ikiwa yana matarajio ya kpoa atalipaswaumu aliyoiacha atakapo poa.

2. SAFARI ambayo ina matatizo na mashaka, ikiwa haina matatizo na mashaka basi kufunga kwake ni bora kuliko kufungua, na atalipa siku zote alizokula safarini akirudi nyumbani baada ya ramadhani na kabla ya ramadhani nyingine.

3.UJAUZITO : Ikiwa kufunga kutamletea matatizo yeye mwenye ujauzito au ikihofiwa kuwa italeta matatizo kwa mtoto aliye tumboni. na atalipa baada ya kujifungua.

4. UZEE ; Ikiwa uzee huo umepindukia kwa ukubwa, na hawezi kufunga tena basi yeye atalisha maskini kila siku ya Ramadhani.

NOTE:

KULIPA KOTE KUWE KABLA YA KUJA RAMADHANI NYINGINE, ISPOKUWA KAMA KUNA UDHURU WA KISHERIA WA KUZUIYA HILO.

MAJIBU HAYA ALIYATOA SHEIKH WANGU SHABAN BIN SALIM ALBATTASHY – Allah amuhifadhi – Masjid Algheithy  ( Mwera – Zanzibar tar 30 – 05 – 2015 )

Published By Ust. Abu Muslim

Swali:

Shukran kwa darsa ya Funga ( 00010 ), Allah mtkufu atakulipa kila la kheri, ila naomba kuuliza swali moja, iwapo kwa yule ambaye hakupata kufunga kwa udhuru wa yeye kuwa ni mzee sana na hakuweza kuwalisha maskini kwa kutokuwa na hali ya kiuwezo, Je afanyeje ?

Jawabu:

Amesema Allah mtukufu:

لَا يُكَلِّفُ اللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا اكْتَسَبت)

” Allah mtukufu haikalifishi nafsi  yeyote ila kwa kadri iwezavyo, faida ya iloyachuma ni ya kwake, na khasara ya iloyachuma itakuwa juu yake” 2:286

Hivyo yeye atakuwa amesamehewa.

 

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Salam alaykum, Je mwanamke anaweza kushahadia akiwa katika hedhi ?

JAWABU:

Hakuna tatizo ya hilo, inajuzu kutoa shahada mbili na kufanya dhikri zingine zisokuwa ni aya za Quran kamili kwa aloyapokea Bibi Aisha kuwa Mtume s.a.w. hakuwa ni mwenye kuacha dhikri muda wote wa uhai wake, Wallahu aalam.

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Abu Muslim Soma hii hoja ya mawahabi, utupe majibu yake:

mtu huyo aliyeleta taarifa za mwezi alikuwa ni bedui, yaani mtu wa majangwani, Mtume s.a.w. hakumuuliza kabisa suala hili – umetoka wapi -, jambo ambalo linathibitisha kuwa suala la umbali gani wa kuoneana mwezi Mtume s.a.w. haulizingatia kabisa.

jambo muhimu ni kule kuonekanwa mwezi sio mahala gani umeonekanwa,nataka uichukue nukta hii na uifanyie kazi ili kujiepusha na mzozo wa baadhi ya shuyuukh wanaoshindana kutafuta ufuasi wa watu wengi wala sio kwa nia ya kuelekeza palipo na usahihi katika masiala haya ya mwezi, na kuugawanya ummah ndio furaha yao kuu.

JAWABU:

Maneno haya ya shari ya kiwahabi yatajibiwa katika nukta tatu, zingatia:

1- Bedui alitoka Madina bila shaka yoyote, na Mtume kutomuuliza alipotoka yaonyesha utanabahifu wake kwani muda ule haiwezekani kuwa alitoka mbali kutokana hali ya usafiri ya zama zao. Hivyo Mtume kutomuuliza si hoja aslan, wala haikuwepo haja ya kumuuliza hilo kwa kule kujulikanwa kuwa ni wa hapo hapo Madina.

2 – Ni muhimu kujua wapi umeonekanwa mwezi, kama inavyoonesha kwa wazi Quran ilipotaja miezi miandamo mingi sio mmoja, akasema ” Wanakuuliza kuhusu miezi miandamo…” 2:189

Miezi miandamo ni mingi hivyo muhimu kujua wapi umeandama ???

3 – kufuata hoja yenye nguvu kama alivyotufundisha Mtume s.a.w. kama alivyosema wazi Ibn Abbas sahaba mtukufu , kuwa kufuata kila mmoja na muandamo wake ndivyo alivyotufundisha Mtume s.a.w. sio kuugawa ummah, bali ummah unagawika kwa kufuata ususuavu wa vishubuhaat vya kiwahabi, na mfano wa mizozo ya kisheria itakayozuka kwa kufuata rai ya kiwahabi:

—- je ni watu wote watakaopata taarifa kwa wakati wa kuonekanwa mwezi nchi za hukoooo ili kutembea na ibada zote kama eda ya kufiwa, mambo ya talaka, ada za mwezi, zaka n.k.

Na katika yenye kujulisha ususuavu wa nyoyo zao ni kule kutokubali dalili za wazi zikikhalifu rai zao, mfano mwanzo walikuja na kufuata Saudia walipoombwa dalili wakakimbilia kimataifa. Kisha ikawa kimataifa Eid el fitri Amma Eid el hajj basi tufute Saudia,

swali: Je dini ifuate teknolojia au teknolojia ifuate dini?? basi vipi zilikuwa funga za mababu zenu kabla ya tivii na redio ?

ikiwa kuna umoja katika hili, mbona wanafunzi wadogo munapingana kwa wazi na masheikh wenu, fatawa zao zote kila mmoja afuate eneo lake … wengine huku katika wanafunzi wao tufuate kimataifa….

kushikamana na rai ya kila mmoja na mwanadamo wake kama alivyosemaAllah mtukufu na  Mtume s.a.w. ndio umoja na rehma,  kinyume chake ndio furqah na adhabu. kwa hatukuwa tukifunga vizuri kwa pamoja kabla ya daawa hii potovu ya kiwahabi ???

Na alivyo mchafu wa moyo muandishi wa makala hiyo amna washutumu watu kwa kujikweza na kutaka wafuasi… Subhaanallah , Je umeingia katika vifua vyao ukazijua nafsi na nia zao ??

Ndugu yangu:

law wajinga hawa wangekaa kimya basi dunia ingepumzika, jua kuwa wenye elimu wa Ulimwengu mzima wa zama zetu wamekaribia kukubaliana kuwa kila mtu afuate eneo lake, na vikao vya kupitisha hilo vilifanyika huko Saudi Arabia.

USIGHURURIKE NA HADAA, TALBIIS NA SHUBUHAAT ZA KIWAHABI WALOJIVIKA KANZU ZA UONGO ZA KISALAFI.

Published By Ust. Abu Muslim

Assalaam alaykum, Ustadhi Je akiamka , akajikuta amemwaga shahawa khalaf jua lishamoza, afanyeje ???

JAWABU:

Anatakiwa aharakishe kukoga, na kwa kharakisha huko atakuwahajaingia katika hukmu ya kuharibikiwa na swaumu ikiwa ni katka ramadhani, na huko kuharakia ni tabia ya kiislam ya kutokaa na uchafu. Amesema Allah mtukufu:

” إن الله يحب التوابين ويحب المتطهرين “

Hakika Allah mtukufu anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kujisafisha” baqarah 222

Na imepokewa kutoka kwa Mtume s.a.w. ” Hakika ya Allah mtukufu ni mzuri na anapenda vizuri”

Wallahu aalam

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI:

Je ni kweli kuwa, tusome Surat Yaasin mara tatu, mara ya kwanza tuombe umri mrefu wenye kheri, mara ya pili tuombe atufanyie wepesi kila liloz zito pia atuondoshee mabalaa, ya tatu tuombe rizki ya halali, usidharau mkumbushe na mwenzio.

JAWABU:

Usishughulishwe na mambo ambayo hayakuthibiti khusuusiya yake, na Qur an si Khaas kwa nisf shaaban tu, bali siku zote ni Rehma na shifaa. Pia dua mtu aombe si NISFU shaban tu, bali siku zote wala hakuna ubora wa kukhusisha dua yoyote siku hiyo. Wallahu aalam.

Published By Ust. Abu Muslim

SWALI: Assalaam alaykum.naomba kuuliza.hivi kuna madhara gani mtu anapozungumza chooni.na jee kuna hadithi ambayo inazungumzia hayo? Mstahiwa sh.naomba kujibiwa.jion njema.Allah akuhifadhi. MAJIBU: Kutoshughulikia jambo lingine lolote – ikiwemo kuongea au kusoma – wakati wa kujisaidia ispokuwa huko kujisaidia ni katika adabu za kujisaidia. ✋ Amepokea Imaam Rabii r.a kuwa Mtume alikuwa anajisaidia, mtu mmoja akamsalimia hakumuitikia ” Amepokea Ibn Jaarud kutoka kwa Ibn Umar kuwa Mtume amesema ” ukinikuta nikijisaidia basi usinisalimie kwani sintokujibu” Ndugu yangu : ikiwa kuitikia salam ambayo ni waajib imekatazwa basi vipi kuhusu maneno ya paukwa na pakawa? Amma hikma ya kukatazwa hilo basi mimi sijui. Wallahu aalam.

 

Published By Ust. Abu Muslim

000016.. PUNYETO NA SALA. A’aleikum .napenda kuuliza swali je wale watu wenye tabia ya kujitoa manii kwa njia ya mkono vipi itahisabika na wao hawana swala kwamda wa siku 40 kama wale walio zini ?? Na iwapo wakitubia toba ya kweli kabla ya cku 40 je swala zao zitakubaliwa?? Ahsanteni. MAJIBU: Mtu yeyote mwenye kufanya madhambi makubwa na asitubie huyo hakubaliwi mema aloyaleta hata yakiwa kama mbingu na ardhi. Amesema Allah mtukufu : قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao? الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri. أُولَٰئِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَلِقَائِهِ فَحَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَزْنًا Hao ni wale walio zikanusha Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimepotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawathamini kitu. 18: 103 – 105. Pia kasema Allah mtukufu: (…قَالَ إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ) ” akasema: hakika Allah mtukufu anawakubalia – wachamungu – matendo yao mema” [Surat Al-Maeda 27] Hivyo haupo ulazima wa kuzitaja siku maalumu, na inatakiwa watubie wote wafanyao madhambi makubwa – kama ya uzinifu na kupiga punyeto – kabla ya kufa wakapoteza aamali zao”
 

Published By Ust. Abu Muslim

000018 .. QUR AN WAKATI WA MAINGILIANO. Assalaam alaykum.mstahiwa sh.naomba kuuliza.jee kwa wazazi wawili2.wakiwa wapo faragha.wakitafuta mtoto.jee inafaa kuweka qur-an.lengo kwa kile ktacho kuja kisipatwe na madhara ima ya kisheitwaan.au ya kibinaadam.kwa sababu kuna wabaya hua wanafanya ubaya pindi watu wakiwa katika hili ile.naomba kujibiwa.na ikiwa nimekosea kuuliza naomba msamaha.kwa sababu bado ni mwanafunzi. MAJIBU: Nilimuuliza swali hili Sheikh wangu Sh. Shaaban Albattashy – shafaahullah wa aafaahu – yakawa majibu ni: QUR AN ni ujumbe unaotakiwa kusikilizwa na kufahamika sio kwa mchezo wala ihaanah. Amesema Allah mtukufu : (وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنْصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ) ” na itakaposomwa Qur an basi isikilizeni na mukae kimya ili mupate kurehemewa” [Surat Al-Araf 204 Pia jambo hilo linakwenda kinyume na malengo ya kuletwa kwetu hiyo Qur an na utukufu wake. Amma kujikinga na Shetani basi iwatoshe dua ilofundishwa na Mtume kwamba isomwe kabla ya maingiliano kwa muda mdogo اللهم جنبنا الشيطان وجنب الشيطان ما رزقتنا “Allahumma jannibnaa shaitaan wajannib shaitaan maa razaqtanaa” Ewe Allah tuwekee mbali sheitan na umuweke mbali shaitani na kile utakachoturuzuku” Amenijibu haya tukiwa Maahad Al istiqaama – Zanzibar.

Published By Ust. Abu Muslim

MADHARA YA KUTEMBEA MCHAFU.
 SWALI
 Assalam alaykum.sh.naomba kuulza.kuna baadh ya watu.hususan vijana.unamkuta amelala baada ya sala ya asubuh.na alipo amka akajikuta anajanaba.lkn mtu huyu haendi kuoga.mpk kuingia sala ya adhuhur jee hakuna katazo lolote linalosema kua mtu asitembee na janaba.na jee nini madhara yk.mtu kutembea na mwili mchafu???.jion njema
 
 MAJIBU:
 Kwa hakika kukaa na uchafu ni kukaa kinyume na fitrah – maumbile sahihi ya mwanadam – kwani ubinadam ni kupenda usafi wa nafsi na mwili.
 
Mtu huyu atakosa fadhila nyingi ikiwemo ya upungufu wa kusoma qur an, pia hatopendwa na Allah mtukufu.
 
 Atapitwa na ibada bora kama za sala ya dhuhaa nayo ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
 
 Na kukaa huko bila ya kuoga ni kwenda kinyume na maelekezo ya uislam yanayosema: 
(…وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ …ُ )
“Na mukiwa na janaba basi jisafisheni….” [Surat Al-Maeda 6]
 
Je hataki kijana huyu kujichukulia mifano katika Quran mfano wa qauli yake
” (…ِ ۚ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَنْ يَتَطَهَّرُوا ۚ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ)
” ndani ya miskiti kuna wanamme wanaopenda kujisafisha na Allah mtukufu anawapenda wenye kujisafisha”
[Surat At-Tawba 108]
 
 kutembea na uchafu ni sababu miongoni mwa sababu za urafiki na Ibliis. Kwa kuwa daima Shaitan hataki mazuri bali machafu.
Na ikawa alikuwa amefunga – Ramadhan au nje ya ramadhan, Sunnah au Faridha – basi atakuwa amekula mchana na amefunguwa kwa hadithi aloipokea Abuu Hurairah
” Atakayeamka akiwa na janaba ataamka akiwa hana saumu”
 
Wallaahu aalam.

Published By Ust. Abu Muslim

DUA BORA.
 
SWALI;
 Asalamu al. Je kunadua bora kuliko zote??
 
MAJIBU:
Dua bora kuliko zote ni zilopokewa katika Qur an na Sunna iliyothibiti. Kwa makubaliano ya ubora wa vyanzo hivyo.
 
 Dua bora kati ya hizo zilopokewa ni zile zilopokewa ubora wake kutoka kwa Mtume s.a.w. kama :
 
SAYYIDU L ISTIGHFAAR.
 
اللهم إني عبدك وابن عبدك وابن أمتك ناصيتي بيدك ماض في حكمك عدل في قضاؤك أسألك بكل اسم هو لك سميت به نفسك أو علمته أحدا من خلقك أو أنزلته في كتابك أو استأثرت به في علم الغيب عندك أن تجعل القرآن ربيع قلبي ونور صدري وجلاء همي”
 
Au dua hii alikuwa mtume akiisoma sana 
  { ربنا آتنا في الدنيا حسنة و في الآخرة حسنة و قنا عذاب النار }”
Rabbanaa aatinaa fii duniyaa hasanah wafi l aakhirat hasanah waqinaa adhaaba nnaar”
 
 Pia mtume kasema:
” Bora ya dua ni Alhamdulillaah” kaipokea Tirmidhy.
 
 Zipo riwaya pia zionyeshazo dua bora ni mtu akiomba mwenyewe akitakacho.
 
Pia kuna kauli hii ya Mtume s.a.w.
” خير ما قلت أنا والنبيون من قبلي لا إله إلا الله وحده لا شريك له له الملك وله الحمد وهو على كل شيء قدير”
Bora ya niloyasema mimi na mitume walionitangulia kabla yangu ** Laailaahaillallaahu wahdahuu laa shariika lahuu lahu l mulk walahu l hamd wahuwa alaa kulli shay in qadiir”
 
 DUA HIZI BORA NA NYINGINEZO ZIMEKUSANYWA VIZURI KATIKA VITABU HIVI:
1. Tuhfat l abraar cha Sh. Muhaddith Said Alqannuubiy – Allah amuhifadhi -.
 
2. Rawdhat Al iimaniy cha Sh. Murabbiy Hamoud Alswawaafiy – Allah amuhifadhi – .
 
 Hayo ndiyo tulonukuu kutoka kwa Masheikh wetu – Allah awalipe kheri – kama kuna makosa ni yetu, tunamuomba Allah mtukufu msamaha wa makosa hayo. Wallahu aalam