DUA YA LEO
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-13
اللهم ارحم من كان يصوم رمضان الأعوام السابقة ولم تبلغه رمضان هذا العام، واجعل قبره خير منزل بعد فراق الدنيا ..
Twakuomba Yaa Allah mrehemu kila aliyekua akifunga Ramadhani miaka iliyopita na hukumjalia kumfikisha (katika Ramadhani) ya mwaka huu, jaalia Qaburi lake liwe nyumba ya kheri baada ya kufariqiana na dunia.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-12
اللهم اجعل هذا الشهر الجديد خير علينا وبشرنا فيه ببشارة خير واجعل لنا الراحة والتوفيق فيه وابعد عنا كل ضيق.
Takuomba Ewe Allah jaalia mwezi huu mpya uwe na kheri kwetu na utubashirie ndani yake kwa bishara nzuri yenye kheri, na ujaalie kwetu sisi raha na tawfiq ndani yake, na utuweke mbali na kila dhiki.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-11
لهم اجعلنا فيه من المتوكلين عليك ، و اجعلنا فيه من الفائزين لديك ، و اجعلنا فيه من المقربين اليك باحسانك يا ذا الجلال والإكرام .
Twakuomba ewe Allah tujaalie ndani ya mwezi wa Ramdhani tuwe miongoni mwa wenye kutegemea kwako, na utujaalie ndani yake miongoni mwa watakao fuzu kwako, na utujaalie ndani yake katika watakao karibishwa kwako kwa hisani yako ewe mwenye utukufu na ukarimu.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU.
|
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-10
اَللّهُمَّ اغْسِلْنا فيهِ مِن الذُّنُوبِ، وَطَهِّرْنا فيهِ مِنَ الْعُيُوبِ، نسألُكَ اَللّهُمَّ فيهِ ما يُرْضيكَ، وَنعُوذُ بِكَ مِمّا يُؤْذيكَ، وَنسألُكَ التَّوْفيقَ فيهِ لأَنْ انطيعَكَ وألا نعصِيكَ.
Twakuomba Yaa Allah ndani ya mwezi huu tusafishe kutokana na madhambi, na ututwaharishe kutokana na aibu, Twakuomba Yaa Allah tujaalie ndani ya mwezi huu kutenda yakuridhishayo na twajikinga kwako kutokana na yanayo kuudhi, twakuomba tawfiq ndani yake ili tuweze kukutii na tusikuasi.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-9
اللهم في هذا الشهر الكريم اشفِ مرضانا، وارحم موتانا، وقّوم أحياءنا، وأصلح فساد قلوبنا .. اللهم كن لنا وللمسلمين عوناً ومعيناً وهادياً وحافظاً ونصيراً
Ewe Allah Twakuomba katika mwezi huu mtukufu uwaponye wagonjwa wetu na uwarehemu maiti wetu, wape nguvu waliyo hai, na zifanye uzuri nyoyo zetu zilizo haribika, Twakuomba ewe Allah uwe msaada kwetu sisi na waisilamu, na uwe muongozo na muhifadhi na mwenyekunusuru (katika maisha yetu)
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-8
اللّهُمَّ افْتَحْ لنا فيهِ أبوابَ الجِنان، وَأغلِقْ عَنَّا فيهِ أبوابَ النِّيرانِ، وَوَفِّقْنا فيهِ لِتِلاوَةِ القُرانِ يامُنْزِلَ السَّكينَةِ في قُلُوبِ المؤمنين
Twakuomba ewe Allah ndani ya mwezi huu tufungulie milango ya pepo, na uifunge kwetu sisi ndani yake milango ya moto, na utuwezeshe ndani yake kuisoma Qur an ewe mwenye kuteremsha utulivu katika nyoyo za waumini.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-7
اللّهم انا نسألُك أن ترزُقَنا حبَّك.. وحبَّ من يُحبُّك وحبَّ كلِّ عملٍ يُقرِّبُنا الى حبِّك وأن تغفرَ لنا وترحمَنا
Ewe Allah hakika sisi twakuomba uturuzuku mapenzi yako, na mapenzi ya akupendae, turuzuku kupenda kila amali itakayo tukurubisha katika mapenzi yako, na utusamehe pia utuhurumie.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-6
اللهم ارزقنا فيه رحمة الأيتام و اطعام الطعام وافشاء وصحبة الكرام برحمتك يا أرحم الراحمين
Twakuomba ewe Allah uturuzuku ndani ya mwezi huu huruma kwa mayatima, na kulisha chakula (kwa wahitaji) na kuwaenezea, turuzuku pia kusuhubiana na watu wema wakarimu kwa rehema zako ewe mbora wa kurehemu.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-5
اللهم اعنا فيه على صيامه و قيامه ، و جنبنا فيه من هفواته واثامه ، و ارزقنا فيه ذكرك بدوامه ،بتوفيقك يا هادي المضلين
Twakuomba ewe Allah ndani ya mwezi huu wa kheri na baraka tuwezeshe juu ya kuufunga na kusimama (visimamo vya usiku, tuepushe ndani yake kutokana na kuteleza kwa kufanya makosa na madhambi, turuzuku ndani yake utajo wako kwa kudumia (hadi mwisho wa uhai wetu) kwa tawfiq yako ewe mwenye kuongoza waliyopotea.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-4
اللهم اجعلنا فيه من المستغفرين ، و اجعلنا فيه من عبادك الصالحين القانتين ، و اجعلنا فيه من اوليائك المقربين ، برأفتك يا ارحم الراحمين
Twakuomba Yaa Allah tujalie ndani ya Ramadhani tuwe katika wenyekutaka msamaha na (wakasamehewa) na utujalie katika waja wako wema tena watiifu na wanyenyekevu, na tujalie ndani yake katika vipezi wako wenyekukaribishwa, kwa upole wako na huruma zako ewe mbora wa kurehemu.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU. VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-3
اللهم قونا فيه على اقامة امرك ، و اذقنا فيه حلاوة ذكرك ، و اوزعنا فيه لأداء شكرك بكرمك ، واحفظنا فيه بحفظك و سترك يا خير الحافظين.
Twakuomba ya Allah ndani ya mwezi huu mtukufu tupe nguvu ya kusimamia na kutekeleza amri zako (miongoni mwa ibada na kuacha makatazo yako) na utuonjeshe ndani yake ladha ya utajo wako (dhikri yako) tuwezeshe tuwe wenyekutekeeza shukra zako kwa karama zako, tuhifadhi kwa hifadhi yako na sitra yako ewe mbora wa kuhifadhi.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIAMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU.
|
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO-2
اللهم قربنا فيه الى مرضاتك ، وجنبنا فيه من سخطك ونقماتك ، و وفقنا فيه لقرائة اياتك ، برحمتك يا أرحم الراحمين
Twakuomba Yaa Allah ndani ya Ramadhani tukurubishe katika (kuyatenda uyaridhiayo) na uturidhie, tukinge ewe Mola wetu na hasira zako na naqama zako, na utuafikishe (utupe uwezo) wa kuzisoma aya zako kwa rehma au huruma zako ewe mbora wa kurehemu.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |
Published By Said Al Habsy  DUA YA LEO - 1
اللهم اجعل صيامنا فيه صيام الصائمين و قيامنا فيه قيام القائمين ، و نبهنا فيه عن نومة الغافلين ، واعف عنا يا عافيا عن المجرمين .
Twakuomba ewe Allah ujaalie funga zetu ndani ya mwezi huu ziwe funga za wafungaji wa kweli (wenye kuthibiti ujira wao) na visimamo vyetu (katika sala mbalimbali) viwe visimamo vya wenye kusimama kwa ukweli (na kuthibiti malipo) tuzindue kutokana na usingizi wa wenye kughafilka, tusamehe ewe mwenye kusamehe wakosaji na waovu.
TWAKUOMBA YAA RABBI ZIKUBALI FUNGA ZETU VISIMAMO VYETU NA JUMLA YA AMALI ZETU. |