Published By Said Al Habsy  SWALI LA - (1)
Wakati gani Zaka ilifaradhishwa?
JAWABU: Faradhi ya zaka Kwa pamojo ilifaridhashwa makka kwa kauli sahihi, kwa dalili ya aya za Makka ambazo zimezungumzia hivyo, kama kauli ya Allah katika suuratul-Muzammil (aya -20)
《Na shikeni swala, na mtoe zake, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopesho mwema》
Nayo ni Katika sura za mwanzo kuteremka, na yalio semwa kuwa aya hiyo ni ya madina si sahihi, lau kama ni ya madina basi isenge kuwa sehemu hiyo peke yake Kuwa ndio ya madina, na inge pasa yote kuwa ni ya madina, hali ya kuwa sehemu ya mwanzo ya sura imefuta kilichokuwa kimefaradhishwa mwanzo katika sura ambacho ni kusimama sehemu kubwa ya usiku (kwa ibada), na hiyo ilikuwa katika kipindi cha makka, na hii ni dalili ya kuwa aya hiyo ni ya Makka.
Na katika dalili ya jambo hili la zakka ni aya zilizomo katika (suuratul-Ma'arij- 24/25)
《Na ambao katika mali yao iko haki maalumu * kwa mwenye kuomba na anae jizuilia kuomba;》
Na aya zilizo kuja katika suuratul-Mu'uminuna (1 -4)
《Hakika wamefanikiwa Waumini * Ambao ni wenyenyekevu katika swala zao * Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi * Na ambao wanatoa zaka》
Na kauli yake katika suuratu Fussilat (6/7).
《Na ole wao wanao msirikisha * Ambao hawatowi zaka na wanaikataa akhera》
Na kauli ya Allah katika suuratu An-nisaa ( 77)
《Jee huwaoni wale walio ambiwa : Izuieni mikono yenu,na mshike swala na mtoe zaka》
Na hizi aya japo kuwa ni za Madina Lakini zinaelezea kipindi cha Makka, kwa hakika waumini waliambiwa: izuwieni mikono yenu katika kipindi cha Makka, na hapo wa kaambiwa: shikeni swala na mtoe zaka, na wakafaradhishiwa baada ya kufika Maidina kupigana jihadi, wala hapo hawakuamrishwa kuzuia mikono yao, na hii ni kuwa azaka ilikuwa imeshafaradhishwa, lakini ilikuwa imetegemezwa katika nafsi za matajiri wenye wao, na kila mmoja anatoa katika mali yake kwa kiwango kinacho zuia shida za mafukara kwa kadri ya uwezo wake (tajiri), na hali ilipo tulia Madina hapo Mwenyezi Mungu akateremsha upambanuzi wa zaka, na ikaaendelea katika hali hiyo iliyopo Sasa, ama kufaradhishwa kwake kwa ijamaal (bila ya kuwekwa niswabu na mengineo) ilikuwa Makka.
والله أعلم. ----------------- { Na wanao kusanya dhahabu na fedha (mali), wala hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu ilio chungu} ----------------- Imetaarishwa Na Kufikishwa Kwako na:
Thuweiniy Seif Al-Ismailiy. |