Shukurani zote ni kwa Allah mtukufu, na rehma na amani ziwe kwa Mtume wetu Muhammad pamoja Aali zake na Masahaba wake waongofu na kila aliyeongoka kwa uongofu wake mpaka siku ya Kiama. TUHUMA.Miongoni mwa tuhuma batili zilizotufikia, ni tuhuma ya kukufurisha Masahaba wa Mtume (s.a.w) -Allah awaridhie-, basi wamesema: "Ibadhi wanakufurisha Masahaba wa Mtume (S.A.W)". Na hao wenye kutuhumu humalizia katika tuhuma zao kutaja Masahaba hawa:-
Allah awaridhie Masahaba wote wa Mtume wetu (s.a.w). JAWABU.Kwanza: Inapaswa tufahamu kuwa Ibadhi inatafautisha baina ya:
Basi tunapaswa tuzingatie vizuri sana, na tujue kuwa ni jambo la kawaida kumkuta mwanachuoni fulani amekamatana na msimamo wake katika suala fulani, na pengine akapata wa kumuunga mkono katika msimamo wake huo, ni sawa msimamo huo umejengwa juu ya Mafundisho ya Madhehebu au juu ya rai yake binafsi. Kutokana na hapo, ni kosa kuifanya misimamo ya wanachuoni kuwa ndiyo mafundisho ya Madhehebu, hata kama misimamo hiyo imejengwa juu ya mafundisho ya Madhehebu, kwa sababu msimamo unabakia katika uhakika wake wa kukamatana na muhusika wake mahususi tu, na kuwa hiyo ni rai yeke binafsi, basi utamuhusu yeye na yule mwenye kukubaliana naye peke yao tu. Pili: Baada ya kufahamu hilo la kwanza tuzingatie haya yafuatayo:-
SABABU ZILIZOPELEKEA BAADHI YA WANAVYUONI WETU KUITAKIDI BARAA-A KWA MASAHABA HAO WALIOTAJWA HAPO JUUKWANZA:Tufahamu kuwa Uislamu ni dini iliyojengeka juu ya misingi ya uadilifu: Allah mtukufu anatuambia katika Qur-ani tukufu: يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاء لِلّهِ وَلَوْ عَلَى أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالأَقْرَبِينَ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقَيرًا فَاللّهُ أَوْلَى بِهِمَا فَلاَ تَتَّبِعُواْ الْهَوَى أَن تَعْدِلُواْ وَإِن تَلْوُواْ أَوْ تُعْرِضُواْ فَإِنَّ اللّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ((Enyi mulioamini: Kuweni wasimamizi kwa uadilifu mashahidi kwa ajili ya Allah hata kama ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili au jamaa wa karibu, ikiwa ni tajiri au fakiri basi Allah ana haki zaidi kuliko hao, musifuate mapendwa moyo kwa kutofanya uadilifu, na kama mutapindisha au mutakwepa basi hakika Allah kwa munayoyafanya ni mwenye kuyajua vizuri sana)) [Anisaa 4/135] Mtume wetu (S.A.W) anatuambia: إِنَّمَا أَهْلَكَ الَّذِينَ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيهِمْ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمْ الضَّعِيفُ أَقَامُوا عَلَيْهِ الْحَدَّ وَايْمُ اللَّهِ لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا ((Hakika yaliwaangamiza waliopita kabla yenu, walikuwa anapoiba mwenye cheo wao (Sharifu) humuacha, na anapoiba dhaifu wao (mnyonge) humsimamishia adabu ya sheria, naapa Wallahi lau Fatima binti Muhammad (Mtoto wake wa kike) ataiba basi nitaukata mkono wake)). [Bukhari 3288, 4304 Muslim 1688] Khalifa wa kwanza Abu Bakar A-Sidiiq (r.a) alipopewa ahadi ya uongozi alisimama, na katika aliyowaambia watu: أَطِيعُوني ما أَطَعْتُ اللَّهَ ورسولَه فإِذا عَصَيْت اللَّهَ ورسولَه فلا طاعةَ لي عليكم ((Nitiini nikiendelea kumtii Allah na Mtume wake, basi nikija nikimuasi Allah na Mtume wake hakutakuwa na utiifu kwenu wa kunitii mimi)). Na wala hakusema ((Munitii mimi kwa sababu ya usahaba wangu na kuchaguliwa kwangu, na hamuna haki ya kuniasi hata nikimuasi Allah na Mtume wake)). Kwa hiyo, ni dhahiri kuwa uadilifu ndiyo njia ya Uislamu, na upendeleo umepigwa vita ndani ya Uislamu; kwa maana hiyo Usahaba sio muhuri wala ngao ya kuondoshewa hukumu za kisheria iwapo kosa litatokezea kwa mmoja wao yoyote yule, kwa hakika Masahaba wamestahiki sifa njema na cheo kikubwa kwa sababu ya kushika kwao vizuri mafundisho ya dini na kuyanusuru (Uchamungu) na sio kwa kuwafumbia macho iwapo litadhihiri kosa kwao. PILI: Sote tunafahamu kuwa hakuna Aya hata moja katika Qur-ani tukufu iliyomtaja kiuanisho yoyote katika Masahaba hao waliotajwa hapo juu, achilia bali kuwepo Aya iliyombashiria Pepo kiuanisho yoyote katika Masahaba hao au mwengine yoyote. Na Mtume wetu Muhammad (s.a.w) ametuaeleza haya: ((إِنِّي فَرَطُكُمْ عَلَى الْحَوْضِ مَنْ مَرَّ عَلَيَّ شَرِبَ وَمَنْ شَرِبَ لَمْ يَظْمَأْ أَبَدًا لَيَرِدَنَّ عَلَيَّ أَقْوَامٌ أَعْرِفُهُمْ وَيَعْرِفُونِي ثُمَّ يُحَالُ بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ. قَالَ أَبُو حَازِمٍ فَسَمِعَنِي النُّعْمَانُ بْنُ أَبِي عَيَّاشٍ فَقَالَ هَكَذَا سَمِعْتَ مِنْ سَهْلٍ فَقُلْتُ نَعَمْ فَقَالَ أَشْهَدُ عَلَى أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ لَسَمِعْتُهُ وَهُوَ يَزِيدُ فِيهَا فَأَقُولُ إِنَّهُمْ مِنِّي فَيُقَالُ إِنَّكَ لَا تَدْرِي مَا أَحْدَثُوا بَعْدَكَ فَأَقُولُ سُحْقًا سُحْقًا لِمَنْ غَيَّرَ بَعْدِي)) ((Hakika mimi nitakutana nanyi katika hodhi, na yule atakayenipitia hapo atakunywa, na yule atakayekunywa hatopata kiu milele, na kwa hakika watanijia watu nawajuwa na wao wananijuwa kisha kutazuiwa baina yangu na baina yao)) Akasema Abu Hazim: Basi akanisikia Nuuman bin Abi Ayaash naye akasema: Namna hivi ulisikia kutoka kwa Sahl? Nikasema: Ndio. Akasema: "Nashuhudia kwa Abu Said Al-Khudri hakika nimemsikia naye anaongeza ndani yake: ((Basi nitasema: ((Hakika hao ni katika mimi (Masahaba wangu Masahaba wangu))). Hapo patasemwa: Hakika wewe hujui waliyozusha baada yako. Basi nitasema: Awe mbali, awe mbali, yule aliyebadilisha baada yangu)) [Bukhari 3349, 6583, 6584 Muslim 2290, 2297] Riwaya hiyo iko wazi kuhusu hali ya baadhi ya Masahaba wa Mtume (s.a.w) vipi watakavofukuzwa siku ya Kiama katika Hodhi lake S.A.W., na kuwa miongoni mwa sifa zao:
Kwa maana hiyo kusifiwa Masahaba kwa wema ni kwa sababu ya Uchamungu wao na uadilifu wao na kushika kwao dini vizuri, basi sababu ikiondoka bila shaka sifa ya wema nayo itaondoka; kwa sababu sifa hiyo ni tawi ambalo shina lake ni Uchamungu na Uadilifu ambao ndiyo sifa ya kuwemo mja katika utiifu wa Allah mtukufu na Mtume wake (s.a.w). MATOKEO MUHIMU YA KITAREHETukijerea katika tarehe ya matokeo ya waislamu baada ya kufa Mtume (s.a.w) tutakutia matokeo yaliyotokea katika zama za Masahaba (r.a), nayo ni kama ifuatavyo:
Sasa katika matokeo haya muhimu ya kitarehe, tunaporejea na kuyaangalia kuiadilifu tunapata kuwa kulipatikana Watu wa Naharawani, nao ni wale waliojitenga kwa kujitoa kwao katika safu za Imam Aliy wakati alipoamua kukubali wito wa Muawiyah wa kuingia katika Sulhu, kiistilahi sulhu hii inajulikana kwa jina la (TAHKIIM) na Watu wa Naharawani walijulikana kuwa ni (MUHAKKIMAH), waliitwa hivyo kwa sababu wao walitoa hukumu moja kwa moja kwa neno lao ((LAA HUKMA ILLAA LILLAHI)), maana yake ((HAKUNA HUKUMU ISIPOKUWA YA ALLAH TU)), neno lao hilo lilikuwa ni ishara ya wazi ya msimamo wao wa kujishika na Qur-ani tukufu na kujifunga na hukumu ya Allah mtukufu aliyokwisha ihukumu kwa waasi, nayo ni hukumu ya kulipiga vita kundi la waasi mpaka kuzima uasi wao na kuirejea katika amri ya Allah nayo ni Amri ya kumtii Kiongozi muadifu ambaye kwa wakati huo alikua ni Imam Aliy bin Abi Twalib. Huenda mtu akasema: Kama hiyo ndiyo hukumu, basi kwa nini wao walitoka nje ya utiifu wa Imam Aliy na kupinga yale aliyoamua ya kukubali sulhu? Kwa nini walijitoa katika safu yake na kujitenga? Jee! hilo si kosa? Jawabu: Kwa hakika sote tunafahamu kuwa mafundisho ya Uislamu yanasema ((hakuna kumtii kiumbe kwa kumuasi Muumba)), na hapa tunakumbusha neno la Khalifa wa kwanza Abu Bakar (r.a): ((Nitiini nikiendelea kumtii Allah kwenu, basi nikija nikimuasi (Allah) hakutakuwa na utiifu kwenu wa kunitii)). Vile vile Kiongozi katika Uislamu anapochukuwa Ahadi ya uongozi hulazimika na sharti ya kumtii Allah na Mtume wake (S.A.W), na kwa maana hiyo akitoka nje ya utiifu wa Allah na Mtume wake S.A.W huwa amevunja sharti ya utiifu kwa Waislamu, na Allah mtukufu amewakataza Waumini kwenye kitabu chake kwa muwambia: ((Na wala musisaidiane katika dhambi na uadui)) [Maaidah 2] Kwa hiyo kujitoa kwao katika safu za Imam Aliy ni haki bila ya shaka yoyote kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu; kwani wao walijiepusha kusaidia na kushiriki katika kufanyika kosa la wazi waliloliona, nalo ni kosa la kuvunja hukumu ya Allah mtukufu ya kulipiga vita kundi la Muasi kwa kufuata rai ya Muasi Muawiyah ya kufanya naye Suluhu. Tukilifahamu hili, tutajuwa kuwa Watu wa Naharawani walikuwa ni wasomi wenye uoni wa mbali sana, nao walikuwa katika msimamo sahihi kabisa kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu. Kwa hiyo ni jambo la kawaida tukakutia katika safu za Ibadhi kuwapo baadhi ya wanaelimu waliodhihirisha Baraa-a kwa Masahaba hao tuliowataja, kwani wao walifanya hivyo kwa kuzingatia kuthibiti upande wao uhakika wa makosa waliyojitosa ndani yake kwa mujibu wa sheria bila ya kuthibiti kutubia kwao kutokana na makosa hayo ambayo ni:
Hizi ndizo sababu kuu zilizopelekea baadhi ya wanavyuoni wetu kuwaingiza Masahaba hao katika hukumu ya Baraa-a; kwa yale yaliyosihi kwao. Sisi upande wetu, kwa wakati wetu huu wa leo, tunasema neno la Sheikh wetu wa zama hizi, naye ni Sheikh Ahmed bin Ahmed Al-Khalili -Allah mtukufu amuhifadhi na atunufaishe kwa elimu yake- amesema alipoulizwa kuhusu Masahaba (r.a): ((Sisi hatujalazimishwa kufuatilia yale yaliyokwishapita, na kwa hakika kinachotulazimu sisi ni kusawazisha na kuboresha ya wakati wetu, na tuanze na nafsi zetu, na gurudumu ya siku halirudi nyuma, basi haiwezekani kuyadiriki yaliyokwishapita wala kuyatengeneza yaliyokwisha haribika, basi tuna nini sisi hata tushughulike na yaliyokwishapita na kuacha kushughulikia majukumu yetu ya wakati tuliomo ndani yake. Na lililokwishapita kabla yako hata kama ni kwa saa * liachie kulishughulikia, kwani hilo sio utiifu.)). Na Allah ndiye anayejua zaidi. [ Fatwa Aqidah 2/305]. Na kwa hakika waliyoyasema baadhi ya wanavyuoni wetu katika hukumu za Baraa-a kuhusu Masahaba hao au baadhi yao, sisi tunayaangalia kuwa ni anuani ya uadilifu usiokuwa na upendeleo katika Madhehebu ya Ibadhi, na hilo linahakikisha kuwa Ibadhi imesimama katika mafundisho sahihi ya Uislamu, basi hayo ni alama ya wazi kuwa Madhehebu ya Ibadhi haina maathiriko ya kupendelea, si kiukoo, wala kicheo, wala kwa chochote kile, na katika Ibadhi hawezi kiongozi kuchezea uadilifu aslan. Basi asitujie mtu na kutuambia Mwanachuoni wenu fulani amemkufurisha Sahaba Fulani; kwani sisi tutamuambia ikiwa amemkufurisha bila ya haki ya kumkufurisha iliyothibiti kwake atakua amekosea, ama ikiwa amemkufurisha kwa haki ya kumkufurisha iliyothibiti kwake basi huo ni uadilifu wa Kiislamu hakuna doa ndani yake, isipokua kwa wale wenye maradhi ya upendeleo katika nafsi zao. Wabillahi taufiqi. |