Ikiwa Imam atakuwa amesahau kitu katika vitendo vya Salaa basi inaruhusiwa kumkumbusha kwa kusema, “SUBHAANA ALLAH.” Kasema Sahl Bin Said kasema, “Kasema Mtume S.A.W., [1]“ مَنْ نَابَهُ شَيْءٌ فِي صَلاتِهِ فَلْيَقُلْ سُبْحَانَ اللَّهِ. Maana yake, “Atakayekumbusha chochote katika Salaa aseme “SUBHAANA ALLAH.”. Na anayeruhusiwa kukumbusha kwa kusema “SUBHAANA ALLAH.” ni mwanamume, na ikiwa ni mwanamke ndiye anayetaka kukumbusha basi atapiga makofi. Kasema Sahl bin Said kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[2] “ إِنَّمَا التَّصْفِيحُ لِلنِّسَاءِ وَالتَّسْبِيحُ لِلرِّجَالِ. Maana yake, “Na kupiga makofi ni kwa wanawake na Tasbih (yaani kusema Subhaana Allah) ni kwa wanaume.”
|