Haipendezi mtu kusali na huku anasinzia, ni bora alale kidogo mpaka usingizi umtoke. Kwani ikiwa atakuwa anasinzia kuna hatari anaweza akailani nafsi yake badala ya kuomba maghufira. Kasema Bibi Aisha R.A.A.H., “Kasema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., [1]“ إِذَا نَعَسَ أَحَدُكُمْ فِي الصَّلاَةِ فَلْيَرْقُدْ، حَتَّى يَذْهَبَ عَنْهُ النَّوْمُ، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ إِذَا صَلَّى وَهُوَ نَاعِسٌ لَعَلَّهُ يَذْهَبُ يَسْتَغْفِرُ اللَّهَ فَيَسُبُّ نَفْسَهُ. Maana yake, “Akisinzia mmoja wenu na yumo ndani ya Salaa, basi alale mpaka umtoke usingizi. Kwani mmoja wenu atakaposali naye anasinzia inawezekana huenda akawa anaomba maghufira (msamaha, na badala yake) akawa anaiapiza nafsi yake.”
[1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/79 (250), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Abu Daawud 4/75 (115), Ibn Maajah 4/275 (1360), At-Ttirmidhiy 2/91 (323), Bukhaari 1/356 (205), Muslim 4/133 (1309). |