Wakati mtu anasali aweke kizuizi, au alama ya kujulisha sehemu ya mwisho wa msala wake, ili kusudi mtu mwingine asiweze kumkatisha Salaa yake. Kasema Abu Huraira R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W.,[1] “ إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَجْعَلْ تِلْقَاءَ وَجْهِهِ شَيْئًا فَإِنْ لَمْ يَجِدْ فَلْيَنْصِبْ عَصًا فَإِنْ لَمْ يَكُنْ مَعَهُ عَصًا فَلْيَخْطُطْ خَطًّا ثُمَّ لا يَضُرُّهُ مَا مَرَّ أَمَامَهُ. Maana yake, “Anaposali mmoja wenu basi aweke mbele yake chochote kile (kizuizi) ikiwa hana cha kuweka basi aweke fimbo; na akiwa hana fimbo, basi achore mstari kwani hakitamdhuru chochote kitakachopita mbele yake.” Pia kasema Musa Talha kutoka kwa baba yake, "Kasema Mtume S.A.W.,[2] “ إِذَا وَضَعَ أَحَدُكُمْ بَيْنَ يَدَيْهِ مِثْلَ مُؤْخِرَةِ الرَّحْلِ فَلْيُصَلِّ وَلا يُبَالِ مَنْ مَرَّ وَرَاءَ ذَلِكَ Maana yake, “Akiweka mmoja wenu mbele yake mfano wa tandiko la farasi, asali na isimshughulishe anaepita upande mwingine”
|