Published By Said Al Habsy  Ikiwa mtu anasafiri nae yuko juu ya kipando cha safari anachosafiria kama vile amepanda mnyama, au gari, au meli, au ndege, basi atasali akiangalia kule anako elelekea, kama hatoweza kuelekea kibla. Kasema Umar R.A.A., "
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُصَلِّي عَلَى رَاحِلَتِهِ فِي السَّفَرِ حَيْثُمَا تَوَجَّهَتْ بِهِ رَاحِلَتُهُ. قَالَ الرَّبِيعُ: وَذَلِكَ فِي النَّوَافِلِ
Maana, “Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akiwa safarini alikuwa akisali juu ya kipando chake (chombo au mnyama aliempanda) akisali akielekea mahali kinapoelekea kipando chake (anapokwenda).” Kasema Ar-Rabi`i, “Hizi ni katika Salaa za Nawaafil.”
|