Iachwe muda kidogo baina ya adhana na iqama ili watu wajitayarishe kwa Salaa (kutawadha). Kasema Jabir bin Abdallah R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W., [1]“ وَاجْعَلْ بَيْنَ أَذَانِكَ وَإِقَامَتِكَ قَدْرَ مَا يَفْرُغُ الْآكِلُ مِنْ أَكْلِهِ وَالشَّارِبُ مِنْ شُرْبِهِ وَالْمُعْتَصِرُ إِذَا دَخَلَ لِقَضَاءِ حَاجَتِهِ وَلَا تَقُومُوا حَتَّى تَرَوْنِي. Maana yake, “Na jalia kati ya adhana yako na ikama yako muda utakaomtosheleza mtu anayekula kumaliza chakula chake, na mwenye kunywa kumaliza kinywaji chake, na aliyekwenda chooni kujisaidia kumaliza haja yake, na wala msisimame kukimu mpaka mmeniona (na Mtume S.A.W. alisema hivi kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa Imam).” Na hii ni dalili ya kwamba anayemiliki iqama ni Imam wa Salaa.
|