Published By Said Al Habsy  Kasema Abdillah bin Umar bin Aas R.A.A., “Kasema nimemsikia Mtume S.A.W., akisema, “
إِذَا سَمِعْتُمْ الْمُؤَذِّنَ فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ ثُمَّ صَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّهُ مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاةً صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عَشْرًا ثُمَّ سَلُوا اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ لِي الْوَسِيلَةَ فَإِنَّهَا مَنْزِلَةٌ فِي الْجَنَّةِ لَا تَنْبَغِي إِلا لِعَبْدٍ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ تَعَالَى وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ أَنَا هُوَ فَمَنْ سَأَلَ اللَّهَ لِي الْوَسِيلَةَ حَلَّتْ عَلَيْهِ الشَّفَاعَةُ.
Maana yake, “Mnapomsikia mwadhini basi semeni kama anavyosema, halafu mnisalie, kwani atakayenisalia mara moja Mwenyezi Mungu anamsalia mara kumi, halafu muombe Mwenyezi Mungu Mtukufu anipe Al Wasila (daraja ya juu ya enzi) kwani hiyo ni sehemu katika pepo, na haipati, ila mja katika waja wa Mwenyezi Mungu, na naomba niwe mimi. Na atakaye niombea Al Wasilah kwa Mwenyezi Mungu basi anastahiki maombezi yangu".
VIII. Kushuhudia baada ya Adhana.
Kasema Saad Abi Waqas R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W., “Atakayesema baada ya kusikia adhana, “
وَأَنَا أَشْهَدُ أَنْ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا وَبِالإِسْلامِ دِينًا وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا.
WA ANA ASH-HADU AN LA ILAAHA ILA LLAH WAHDAHU LA SHARIKA LAH. WA ASH-HADU ANNA MUHAMMADAN ABDUHU WA RASUULUHU. RADHIYTU BILLAAHI RABBAN. WA BIL ISLAAMI DIINAN. WA BI MUHAMMADIN NABIIYYAN.
Maana yake, “Na mimi nashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu ni peke yake na wala hana mshirika. Na nashuhudia kwamba Muhammad S.A.W. ni mja na mjumbe Wake. Nimeridhika na Allah kuwa Mola wangu, na uisilamu ndio dini yangu, na Muhammad ni Mtume Wake”. Anasamehewa madhambi yake ya nyuma”.
IX. Dua baada ya adhana.
Kasema Jabir R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W, “
مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ النِّدَاءَ اللَّهُمَّ رَبَّ هَذِهِ الدَّعْوَةِ التَّامَّةِ وَالصَّلاةِ الْقَائِمَةِ آتِ مُحَمَّدًا الْوَسِيلَةَ وَالْفَضِيلَةَ وَابْعَثْهُ مَقَامًا مَحْمُودًا الَّذِي وَعَدْتَهُ.
ALLAHUMMA RABA HADHIHI DA`WATIT-TAMMATI WAS-SALAATIL QAAIMA, ATI MUHAMMADAN AL WASILATA WAL-FADHILATA WAB`ATH-HU MAQAAMAN MAHMUDANIL-LADHI WA-ADTAHU.
Maana yake, “Atakayesema baada ya kusikia adhana “Ewe Mwenyezi Mungu mwenye wito huu uliokamilika, na wakati wa Salaa hii ilioingia, nakuomba uumpe Muhammad Al Wasilah, na umpeleke katika mahali penye daraja kuu yenye enzi, ambapo umemuahidi.” “Anastahili maombezi yangu siku ya kiama.”
|