Published By Said Al Habsy  Kasema Abu Huraira, “Kasema Mtume S.A.W, “
اللَّهُمَّ أَرْشِدْ الأَئِمَّةَ وَاغْفِرْ لِلْمُؤَذِّنِينَ.
Maana yake, “Ee Mwenyezi Mungu waongoze ma Imam na wasamehe waadhini.” Hadithi ilio hadithiwa na Ibn Umar R.A.A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W., “
ثَلاثَةٌ عَلَى كُثْبَانِ الْمِسْكِ أُرَاهُ قَالَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَبْدٌ أَدَّى حَقَّ اللَّهِ وَحَقَّ مَوَالِيهِ وَرَجُلٌ أَمَّ قَوْمًا وَهُمْ بِهِ رَاضُونَ وَرَجُلٌ يُنَادِي بِالصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ.
Maana yake, “Watatu (yaani watu aina tatu) siku ya kiyama watakuwa juu ya matuta ya miski nawaona. Akasema, “Mja atakae timiza haki ya Mwenyezi Mungu na haki ya bwana wake, na mtu ambae anawasalisha watu na hali ya kuwa wako radhi nae. Na mtu anaeadhini kwa ajili ya Salaa tano kila siku mchana na usiku”.
|