Published By Said Al Habsy  Aya zilizo taja na kuzungumzia ukafiri katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni nyingi, nitazitaja baadhi yake kwa ushahidi ili kuonyesha sio kila ukafiri, au madhambi makubwa yanamtoa mtu katika uisilamu, kama ifuatavyo: Kasema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Al I`mran aya ya 97, “
﴿وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ الله غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ﴾.
Maana yake, “Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu". Pia Kasema katika Surat Al-Maida aya 44, “
﴿وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ.﴾
Maana yake, “Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri”. Pia Kasema Mwenyezi katika Surat An-Naml aya ya 40, “
﴿لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ وَمَن شَكَرَ فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيٌّ كَرِيمٌ﴾.
Maana yake, “Ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu". Pia Kasema katika Surat Al-Insan aya ya 2 na aya ya 3,
﴿إِنَّا خَلَقنَا الإِنسَـنَ مِن نُّطفَةٍ اَمشَاجٍ نَّبتَلِيهِ فَجَعلنـهُ سَمِيعَا بَصِيرًا} {إِنَّا هَدَينـهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَ إِمَّا كَفُورًا﴾.
Maana yake, “Kwa hakika tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyochanganyika: (ya mwanamume na mwanamke), ili tumfanyie mtihani (kwa amri zetu na makatazo yetu); kwa hivyo tukamfanya ni mwenye kusikia na mwenye kuona.” “Hakika sisi tumemwongoa, (tumembainishia) njia (zote mbili ya kheri na ya shari). Basi (mwenyewe tena) atakuwa mwenye shukrani au mwenye kukufuru, (kukanusha).” |