Published By Said Al Habsy  Salaa tano zilifaradhishwa kwa Mtume wetu S.A.W. pamoja na umma wake usiku wa Miraji, mwaka mmoja kabla ya kuhamia kwake Madina. Kasema Anas bin Malik R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W, “
فَرَضَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ عَلَى أُمَّتِي خَمْسِينَ صَلاةً فَرَجَعْتُ بِذَلِكَ حَتَّى أَمُرَّ بِمُوسَى عَلَيْهِ السَّلام فَقَالَ مَا فَرَضَ رَبُّكَ عَلَى أُمَّتِكَ قُلْتُ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسِينَ صَلاةً قَالَ لِي مُوسَى فَرَاجِعْ رَبَّكَ عَزَّ وَجَلَّ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لَا تُطِيقُ ذَلِكَ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَوَضَعَ شَطْرَهَا فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَأَخْبَرْتُهُ فَقَالَ رَاجِعْ رَبَّكَ فَإِنَّ أُمَّتَكَ لَا تُطِيقُ ذَلِكَ فَرَاجَعْتُ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ فَقَالَ هِيَ خَمْسٌ وَهِيَ خَمْسُونَ لا يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَيَّ فَرَجَعْتُ إِلَى مُوسَى فَقَالَ رَاجِعْ رَبَّكَ فَقُلْتُ قَدْ اسْتَحْيَيْتُ مِنْ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ.
Maana yake, “Mwenyezi Mungu aliwafaridhishia umma wangu Salaa hamsini, na nilirudi na amri hiyo hata nilipompitia Mussa A...S Akasema, “Nini kakufaradhishia Mola wako Mtukufu kwa watu wako” Nikasema, “Amenifaradhishia Salaa hamsini”, Musa akaniambia, “Rudi kwa Mola wako Mtukufu kwani umma wako hawatoweza hivyo”. Nikarudi kwa Mola wangu Mtukufu, akapunguza nusu yake nikarudi kwa Mussa nikamuelezea Akasema, “Rudi kwa Mola wako Mtukufu kwani umma wako hawatoweza hivyo”. Nikamrudia Mola Mtukufu akasema, “Hizo ni tano nazo ni sawa sawa na khamsini, kwangu haibadiliki kauli” Nikamrudia Musa akaniambia mrejee Mola wako”. Nikasema, “Nastahi (kuonea haya) kwa Mola wangu Mtukufu”
Wanavyuoni wamesema Mola Mtukufu amezifaradhisha Salaa tano katika Surat Al-Israai aya ya 78 kasema, “
﴿أَقِمِ الصَّلاةَ لِدُلُوكِ الشَّمسِ إِلَى غَسَقِ الَّيلِ وَقُرءَانَ الفَجرِ إِنَّ قُرءَانَ الفَجرِ كَانَ مَشهُوداً﴾.
Maana yake, “Simamisha Salaa jua linapopinduka (likaenda magharibi) (Salaa ya adhuhuri na alaasiri) mpaka giza la usiku (Salaa ya magharib na ishai), na Qur`aani ya alfajiri (Salaa ya alfajiri). Hakika kusoma Qur`aani katika (Salaa) ya alfajiri kunahudhuriwa. (na Malaika)”.
Pia kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Hud aya ya 114, “
﴿وَأَقِمِ الصَّلاةَ طَرَفَىِ النَّهَارِ وَ زُلَفاً مِّنَ الَّيلِ إِنَّ الحَسَناَتِ يُذهِبنَ السَّيِئاتِ ذَلِكَ ذِكرَى لِلذَّكِرِين﴾.
Maana yake, “Na simamisha Salaa katika ncha mbili za mchana (nayo ni Salaa ya Adhuhuri na Alasiri) na nyakati za usiku zilizo karibu na mchana. (nayo ni Magharibi na Ishai ziko karibu na mwisho wa mchana, na Alfajiri iko karibu na mwanzo wa mchana). Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao kumbuka.”
Pia kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat AR-Rum aya ya 17 na 18, “
﴿فَسُبحاَنَ اللهِ حِينَ تُمسُونَ وَحِينَ تُصبِحُونَ﴾﴿وَلَهُ الحَمدُ فِى السَّماَوتِ وَالأَرضِ وَعَشِيًّا وَ حِينَ تُظهِرُونَ﴾.
Maana yake, “Basi mtukuzeni Mwenyezi Mungu mnapoingia katika nyakati za usiku (kwa kusali Magharib na Isha) na mnapoingia katika asubuhi (kwa kusali Salaa ya Alfajiri). Na sifa zote njema ni zake Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini. Na (mtukuzeni Mwenyezi Mungu S.W.T.) wakati wa Alasiri na mnapoingia wakati wa Adhuhuri.”
|