Published By Said Al Habsy Salaa ni nguzo ya dini na ni kitendo cha kwanza cha ibada katika vitendo kuanza kuhesabiwa siku ya kiyama. Na ni ibada ya kwanza kwa yule aliyebaleghe kuanza kuitimiza bila kuiacha, na hii ni dalili ya umuhimu wake katika dini. Kwa muhtasari nitaelezea mahala, shani na utukufu wake katika dini, kama ifuatavyo. I.Nguzo ya kwanza ya vitendo.Salaa ni nguzo ya kwanza ya vitendo baada ya imani. Kasema Mwenyezi Mtukufu katika Suratil Baqara aya ya 2 na aya ya 3, " ﴿هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ﴾ ﴿الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاةَ﴾. Maana yake, "Ni uwongofu kwa wachamungu Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Salaa".
II. Nguzo imara inayoisimamisha dini.Salaa ni nguzo imara inayoisimamisha dini kikamilifu. Hadithi iliyo hadithiwa na Muadh bin Jabal R.A.A kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[1] “ رَأْسُ الأَمْرِ الإِسْلامُ وَعَمُودُهُ الصَّلاةُ وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الْجِهَادُ. Maana yake, “Kilicho muhimu ni Uisilamu na nguzo yake ni Salaa na kilele chake ni jihad (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu).” Hadithi iliyo hadithiwa na Ibn Umar R.A..A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W., [2]“ لا إيمان لمن لا أمانة له ولا صلاة لمن لا طهور له ولا دين لمن لا صلاة له إنما موضع الصلاة من الدين كموضع الرأس من لجسد. Maana yake, “Hana imani asiyekuwa na amana (siyo muaminifu), wala hana Salaa asiyekuwa na tohara, na wala hana dini asiyekuwa na Salaa, kwani pahala pa Salaa katika dini ni kama vile mahali pa kichwa katika mwili.” Yaani kiumbe bila ya kichwa hakina uhai na vile vile asiye na Salaa hana dini. Pia Bibi Aisha R.A.A.H. kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[3] “ لِكُلِّ شَيْءٍ عَمُودٌ، وَعَمُودُ الدِّينِ الصَّلاَةُ، وَعمُودُ الصَّلاَةِ الْخُشُوعُ، وَخَيْرُكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ. Maana yake, “Kila kitu kina nguzo, na nguzo ya dini ni Salaa, na nguzo ya Salaa ni unyenyekevu, na mbora kati yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mwenye kumcha (Mwenyezi Mungu) zaidi.” Hadithi iliyo hadithiwa na Nafia bin Malik kasema, “Umar bin Khatab R.A.A. aliwaandikia wale aliyo wapa madaraka akaandika, [4]“ إِنَّ أَهَمَّ أَمْرِكُمْ عِنْدِي الصَّلاةُ فَمَنْ حَفِظَهَا وَحَافَظَ عَلَيْهَا حَفِظَ دِينَهُ وَمَنْ ضَيَّعَهَا فَهُوَ لِمَا سِوَاهَا أَضْيَعُ Maana yake, “Lililo muhimu katika mambo yenu kwangu ni Salaa, na yeyote yule atakae ihifadhi basi ameihifadhi dini yake, na yule atakae iharibu basi ndio hivo hivo kaharibu mengine.” III. Nguzo ya pili ya dini. Salaa ni nguzo ya pili ya dini baada ya shahada mbili. Kasema Ibn Umar R.A.A. Kasema Mtume S.A.W., [5]“ بُنِيَ الإِسْلامُ عَلَى خَمْسٍ شَهَادَةِ أَنْ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ وَالْحَجِّ وَصَوْمِ رَمَضَانَ. Maana yake, “Uislamu umejengwa kwa (nguzo) tano, kushuhudia kwamba hapana Mwenyezi Mungu (wa kuabudiwa kwa haki) isipokuwa Allah, na Muhammad S.A.W. ni mjumbe Wake, na kusimamisha Salaa, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu (kwa mtu) mwenye uwezo, na kufunga Mwezi wa Ramadhani.” IV. Kitendo cha kwanza cha ibada kuhesabiwa.Salaa ni kitendo cha kwanza katika ibada ambacho mja ataanza kuhesabiwa siku ya kiyama. Kasema Abu Huraira R.A.A., “Nimemsikia Mtume S.A.W. akisema, [6]“ إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاتُهُ فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ. Maana yake, “Kitu cha kwanza anachoanza kuhesabiwa mja siku ya kiyama katika vitendo vyake ni Salaa yake, ikiwa imetengenea basi amefaulu na ameshinda ni ikiwa imeharibika basi amefeli na amekhasirika”. V. Makimbilio ya mwanaadamu wakati wa shida.Subira na kuwa na msimamo thabiti ni jambo gumu sana, na hii ni asili ya maumbile ya mwanaadamu kwani kaumbwa na papara, akifikwa na shari basi hu-haha na kubabaika, na akifikwa na kheri hutakabari[7]. Hii ni tofauti na yule anaehifadhi Salaa yake, Mola anamhifadhi na tabia hizo, na anamuwezesha kuwa na msimamo imara katika kila hali inayomsibu. Kasema Mola Mtukufu kuhusu tabia ya mwanaadamu katika Surat Al-Maa`rij aya ya 19 mpaka ya 23, ‘ ﴿إِنَّ الإِنْسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا﴾﴿إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا﴾﴿وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا﴾﴿إِلَّا الْمُصَلِّينَ﴾﴿الَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلاتِهِمْ دَائِمُونَ﴾. Maana yake, “Hakika mtu ameumbwa na papara. Inapo mgusa shari hupapatika. Na inapo mgusa kheri huizuilia. Isipokuwa wanao Sali. Ambao wanadumisha Salaa zao”. Mwanaadamu akiona milango yote ya faraja imefungika kwake naye yuko katika shida na dhiki, basi utamuona ana kimbilia kwa Mola Mtukufu kwa kunyenyekea na ibada, ingawa hili lilikuwa alifanye kwanza, na akipatikana na jambo basi azidishe ibada na kujisogeza karibu na Mola ili aweze kupata msaada, faraja, na kuthibitishwa. Mfano mzuri ni Mtume S.A.W. akipatwa na jambo la kumhuzunisha basi huwa akisali. Kasema Hudhaifa R.A.A.,[8] “ كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا حَزَبَهُ أَمْرٌ صَلَّى. Maana yake, “Ilikuwa Mtume S.A.W. likimfika jambo zito husali”. Pia Miishari kasema, "Nimemsikia Mtume S.A.W akisema,[9] “ يَا بِلالُ أَقِمْ الصَّلاةَ أَرِحْنَا بِهَا. Maana yake, “Ewe Bilal kimu Salaa itutulize kwayo.” VI. Inamzuilia mtu kufanya maasi.Hakika Salaa inayo saliwa kwa kutimiza masharti yake, inakuwa sababu ya kumzuia mtu kuacha na kumkinga na maasi. Kasema Mola Mtukufu katika Surat Al-A`nkabut aya ya 45, “ ﴿وَأَقِمِ الصَّلاةَ إِنَّ الصَّلاةَ تَنهَى عَنِ الفَحشَآءِ وَ المُنكَرِ﴾. Maana yake, “Na ushike Salaa (simamisha/dumisha Salaa). Hakika Salaa inazuilia mambo machafu na maovu”. VII. Kipenzi cha Mtume S.A.W.Salaa ilikuwa ni kipenzi cha Mtume S.A.W. Kasema Anas R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W.,[10] “ حُبِّبَ إِلَيَّ مِنْ الدُّنْيَا النِّسَاءُ وَالطِّيبُ وَجُعِلَ قُرَّةُ عَيْنِي فِي الصَّلاةِ. Maana yake, “Nimependezeshewa kwangu katika dunia wanawake, na manukato na nimejaaliwa kipenzi cha macho yangu katika Salaa.” Yaani kiburudisho cha moyo.
VIII. Wasia wa mwisho wa Mtume S.A.W.Mtume S.A.W. wakati wa maradhi yake naye yuko katika saa zake za mwisho za uhai wake, alikua akiusia mara kwa mara kusimamisha Salaa. Hadithi ya Anas Bin Malik R.A.A. kasema, [11]“ كَانَتْ عَامَّةُ وَصِيَّةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ حَضَرَتْهُ الْوَفَاةُ وَهُوَ يُغَرْغِرُ بِنَفْسِهِ الصَّلاةَ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ. Maana yake, “Ilikuwa wasia wake sana Mtume S.A.W wakati yalipomfikia mauti nae anavuta pumzi zake za mwisho ni: Salaa na wale munao wamiliki katika mikono yenu ya kulia”. IX. Kipimo cha kumtofautisha mtu na ukafiri.Salaa ni kipimo cha imani cha kumtofautisha mtu na ukafiri. Ibn Abbas R.A.A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[12] “ لَيْسَ بَيْنَ الْعَبْدِ وَالْكُفْرِ إِلاَّ تَرْكُهُ لِلصَّلاَةِ. Maana yake, “Hakuna tofauti baina ya mja na kafir ila kwa kuacha Salaa”. Yeyote yule atakayeacha Salaa atakuwa amekufuru, ama atakuwa amekufuru kufuru neema, ambayo itakuwa imemtoa katika imani, lakini atakuwa bado ni Muislamu au atakuwa amekufuru kufuru shirk ambayo itakuwa imemtoa katika Uisilamu. Inshallah nitazielezea tofauti za kufuru hizi mbili na hukumu zake, nitakapofikia mahala pake. X. Asiyesali amefananishwa na washirikina.Kasema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat AR-rum aya ya 31,” ﴿وَأَقِيمُواْ الصَّلاةَ وَلاَ تَكُونُواْ مِنَ المُشرِكِينَ﴾. Maana yake, “Na simamisheni Salaa, na wala msiwe katika washirikina.”
[1] At-Ttirmidhiy 9/202 (2541, Ahmad (21008). [2] Ttabarani 1/113 (162). [3]Al-Imamu Al-Rab`iu 1/93 (285) [4] Malik 1/7 (5). [5] Bukhaari 1/11(7). [6] At-Ttirmidhiy 2/189 (378). [7] Kuwa na majivuno na kiburi. [8] Abu Daawud 4/88 (1124). [9] Abu Daawud 13/165 (4333). [10] Ahmad 28/74 (13526), Nisaai 12/288 (3878). [11] Ibn Maajah 8/164 (2688). [12] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/96 (303), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Ibn Habaan 4/304 (453), Ahmad Hambal 3/370 (15021), Ddaraqtun 2/53 (4), Ddaaramy 1/307 (1233).. |
Published By Said Al Habsy Salaa ni nguzo imara inayoisimamisha dini kikamilifu. Hadithi iliyo hadithiwa na Muadh bin Jabal R.A.A kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[1] “ رَأْسُ الأَمْرِ الإِسْلامُ وَعَمُودُهُ الصَّلاةُ وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الْجِهَادُ. Maana yake, “Kilicho muhimu ni Uisilamu na nguzo yake ni Salaa na kilele chake ni jihad (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu).” Hadithi iliyo hadithiwa na Ibn Umar R.A..A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W., [2]“ لا إيمان لمن لا أمانة له ولا صلاة لمن لا طهور له ولا دين لمن لا صلاة له إنما موضع الصلاة من الدين كموضع الرأس من لجسد. Maana yake, “Hana imani asiyekuwa na amana (siyo muaminifu), wala hana Salaa asiyekuwa na tohara, na wala hana dini asiyekuwa na Salaa, kwani pahala pa Salaa katika dini ni kama vile mahali pa kichwa katika mwili.” Yaani kiumbe bila ya kichwa hakina uhai na vile vile asiye na Salaa hana dini. Pia Bibi Aisha R.A.A.H. kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[3] “ لِكُلِّ شَيْءٍ عَمُودٌ، وَعَمُودُ الدِّينِ الصَّلاَةُ، وَعمُودُ الصَّلاَةِ الْخُشُوعُ، وَخَيْرُكُمْ عِنْدَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ. Maana yake, “Kila kitu kina nguzo, na nguzo ya dini ni Salaa, na nguzo ya Salaa ni unyenyekevu, na mbora kati yenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule mwenye kumcha (Mwenyezi Mungu) zaidi.” Hadithi iliyo hadithiwa na Nafia bin Malik kasema, “Umar bin Khatab R.A.A. aliwaandikia wale aliyo wapa madaraka akaandika, [4]“ إِنَّ أَهَمَّ أَمْرِكُمْ عِنْدِي الصَّلاةُ فَمَنْ حَفِظَهَا وَحَافَظَ عَلَيْهَا حَفِظَ دِينَهُ وَمَنْ ضَيَّعَهَا فَهُوَ لِمَا سِوَاهَا أَضْيَعُ Maana yake, “Lililo muhimu katika mambo yenu kwangu ni Salaa, na yeyote yule atakae ihifadhi basi ameihifadhi dini yake, na yule atakae iharibu basi ndio hivo hivo kaharibu mengine.”
|
Published By Said Al Habsy Salaa ni nguzo ya pili ya dini baada ya shahada mbili. Kasema Ibn Umar R.A.A. Kasema Mtume S.A.W., [1]“ بُنِيَ الإِسْلامُ عَلَى خَمْسٍ شَهَادَةِ أَنْ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ وَالْحَجِّ وَصَوْمِ رَمَضَانَ. Maana yake, “Uislamu umejengwa kwa (nguzo) tano, kushuhudia kwamba hapana Mwenyezi Mungu (wa kuabudiwa kwa haki) isipokuwa Allah, na Muhammad S.A.W. ni mjumbe Wake, na kusimamisha Salaa, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba ya Mwenyezi Mungu (kwa mtu) mwenye uwezo, na kufunga Mwezi wa Ramadhani.”
|
Published By Said Al Habsy Salaa ni kitendo cha kwanza katika ibada ambacho mja ataanza kuhesabiwa siku ya kiyama. Kasema Abu Huraira R.A.A., “Nimemsikia Mtume S.A.W. akisema, [1]“ إِنَّ أَوَّلَ مَا يُحَاسَبُ بِهِ الْعَبْدُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنْ عَمَلِهِ صَلاتُهُ فَإِنْ صَلُحَتْ فَقَدْ أَفْلَحَ وَأَنْجَحَ وَإِنْ فَسَدَتْ فَقَدْ خَابَ وَخَسِرَ. Maana yake, “Kitu cha kwanza anachoanza kuhesabiwa mja siku ya kiyama katika vitendo vyake ni Salaa yake, ikiwa imetengenea basi amefaulu na ameshinda ni ikiwa imeharibika basi amefeli na amekhasirika”.
|
Published By Said Al Habsy Subira na kuwa na msimamo thabiti ni jambo gumu sana, na hii ni asili ya maumbile ya mwanaadamu kwani kaumbwa na papara, akifikwa na shari basi hu-haha na kubabaika, na akifikwa na kheri hutakabari[1]. Hii ni tofauti na yule anaehifadhi Salaa yake, Mola anamhifadhi na tabia hizo, na anamuwezesha kuwa na msimamo imara katika kila hali inayomsibu. Kasema Mola Mtukufu kuhusu tabia ya mwanaadamu katika Surat Al-Maa`rij aya ya 19 mpaka ya 23, ‘ ﴿إِنَّ الإِنْسَانَ خُلِقَ هَلُوعًا﴾﴿إِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ جَزُوعًا﴾﴿وَإِذَا مَسَّهُ الْخَيْرُ مَنُوعًا﴾﴿إِلَّا الْمُصَلِّينَ﴾﴿الَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلاتِهِمْ دَائِمُونَ﴾. Maana yake, “Hakika mtu ameumbwa na papara. Inapo mgusa shari hupapatika. Na inapo mgusa kheri huizuilia. Isipokuwa wanao Sali. Ambao wanadumisha Salaa zao”. Mwanaadamu akiona milango yote ya faraja imefungika kwake naye yuko katika shida na dhiki, basi utamuona ana kimbilia kwa Mola Mtukufu kwa kunyenyekea na ibada, ingawa hili lilikuwa alifanye kwanza, na akipatikana na jambo basi azidishe ibada na kujisogeza karibu na Mola ili aweze kupata msaada, faraja, na kuthibitishwa. Mfano mzuri ni Mtume S.A.W. akipatwa na jambo la kumhuzunisha basi huwa akisali. Kasema Hudhaifa R.A.A.,[2] “ كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا حَزَبَهُ أَمْرٌ صَلَّى. Maana yake, “Ilikuwa Mtume S.A.W. likimfika jambo zito husali”. Pia Miishari kasema, "Nimemsikia Mtume S.A.W akisema,[3] “ يَا بِلالُ أَقِمْ الصَّلاةَ أَرِحْنَا بِهَا. Maana yake, “Ewe Bilal kimu Salaa itutulize kwayo.”
|
Published By Said Al Habsy Salaa ilikuwa ni kipenzi cha Mtume S.A.W. Kasema Anas R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W.,[1] “ حُبِّبَ إِلَيَّ مِنْ الدُّنْيَا النِّسَاءُ وَالطِّيبُ وَجُعِلَ قُرَّةُ عَيْنِي فِي الصَّلاةِ. Maana yake, “Nimependezeshewa kwangu katika dunia wanawake, na manukato na nimejaaliwa kipenzi cha macho yangu katika Salaa.” Yaani kiburudisho cha moyo.
|
Published By Said Al Habsy Mtume S.A.W. wakati wa maradhi yake naye yuko katika saa zake za mwisho za uhai wake, alikua akiusia mara kwa mara kusimamisha Salaa. Hadithi ya Anas Bin Malik R.A.A. kasema, [1]“ كَانَتْ عَامَّةُ وَصِيَّةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ حَضَرَتْهُ الْوَفَاةُ وَهُوَ يُغَرْغِرُ بِنَفْسِهِ الصَّلاةَ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ. Maana yake, “Ilikuwa wasia wake sana Mtume S.A.W wakati yalipomfikia mauti nae anavuta pumzi zake za mwisho ni: Salaa na wale munao wamiliki katika mikono yenu ya kulia”.
|
Published By Said Al Habsy Salaa ni kipimo cha imani cha kumtofautisha mtu na ukafiri. Ibn Abbas R.A.A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[1] “ لَيْسَ بَيْنَ الْعَبْدِ وَالْكُفْرِ إِلاَّ تَرْكُهُ لِلصَّلاَةِ. Maana yake, “Hakuna tofauti baina ya mja na kafir ila kwa kuacha Salaa”. Yeyote yule atakayeacha Salaa atakuwa amekufuru, ama atakuwa amekufuru kufuru neema, ambayo itakuwa imemtoa katika imani, lakini atakuwa bado ni Muislamu au atakuwa amekufuru kufuru shirk ambayo itakuwa imemtoa katika Uisilamu. Inshallah nitazielezea tofauti za kufuru hizi mbili na hukumu zake, nitakapofikia mahala pake.
[1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/96 (303), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Ibn Habaan 4/304 (453), Ahmad Hambal 3/370 (15021), Ddaraqtun 2/53 (4), Ddaaramy 1/307 (1233).. |