I.Kasema Salim kasema, "Ibn Umar alikuwa anamwambia mtu akitaka kusafiri, "Sogea karibu yangu ili nikuage kama vile Mtume S.A.W. alivyokuwa akituaga". Halafu anasema, [1]" أَسْتَوْدِعُ اللَّهَ دِينَكَ وَأَمَانَتَكَ وَخَوَاتِيمَ عَمَلِكَ. Astawdi`u Llaha diinak, wa amanatak, wa khawatima amalik. Maana yake, "Namkabidhi Mwenyezi Mungu dini yako, na uaminifu wako, na mwisho wa vitendo vyako".
II. Kasema Mohamed bin Ka`ab, "Mtume S.A.W anapolitayarisha jeshi likiwa tayari kwa kuondoka analiaga kwa kusema, [2]" أستودع الله دينكم وأماناتكم وخواتيم أعمالكم. Astawdi`u Llaha dinakum, wa amanatakum, wa khawatima amalikum. Maana yake, "Namkabidhi Mwenyezi Mungu dini yenu, na uaminifu wenu, na mwisho wa vitendo vyenu".
III. Kasema Anas R.A.A., "Mwanamume mmoja alikuja kwa Mtume S.A.W akasema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W mimi nataka kusafiri nipe mafao ya njiani, "Akasema Mtume S.A.W kumjibu, [3]" زَوَّدَكَ اللَّهُ التَّقْوَى (قَالَ زِدْنِي قَالَ) وَغَفَرَ ذَنْبَكَ (قَالَ زِدْنِي بِأَبِي أَنْتَ وَأُمِّي قَالَ) وَيَسَّرَ لَكَ الْخَيْرَ حَيْثُمَا كُنْتَ. Maana yake, "Mwenyezi Mungu akuzidishie ucha-Mungu". Akasema, "Niongeze". Akasema, "Na akusamehe madhambi yako"., Akasema, "Niongeze kwa kikomboleo chako baba yangu na mama yangu". Akasema, "Na akurahisishie heri popote utakapo kuwepo". زَوَّدَكَ اللَّهُ التَّقْوَى ,وَغَفَرَ ذَنْبَكَ, وَيَسَّرَ لَكَ الْخَيْرَ حَيْثُمَا كُنْتَ. Zawdaka Llahu t`taqwa, waghafara dham`baka, wa yassara laka l`khaira haithuma kunta. Maana yake, "Mwenyezi Mungu akuzidishie ucha-Mungu, na akusamehe madhambi yako, na akurahisishie heri popote utakapo kuwepo ".
|