Published By Said Al Habsy  I. Kuwa na udhu.
Kutoka kwa Abi Mussa R.A.A. kasema, "Aliomba Mtume S.A.W. maji akatawadha halafu akainua mikono yake akasema, [1]"
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِعُبَيْدٍ أَبِي عَامِرٍ وَرَأَيْتُ بَيَاضَ إِبْطَيْهِ فَقَالَ اللَّهُمَّ اجْعَلْهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَوْقَ كَثِيرٍ مِنْ خَلْقِكَ مِنْ النَّاسِ.
Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe mja wako Abi Aamir, na nikaona weupe wa kwapa zake, akasema, "Ewe Mwenyezi Mungu mjalie siku ya kiyama awe na daraja ya juu katika viumbe Wako miongoni mwa watu".
II. Kuelekea Kibla.
Kutoka kwa Abdillah bin Masoud R.A.A. kasema, [2]"
اسْتَقْبَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْكَعْبَةَ فَدَعَا عَلَى نَفَرٍ مِنْ قُرَيْشٍ عَلَى شَيْبَةَ بْنِ رَبِيعَةَ وَعُتْبَةَ بْنِ رَبِيعَةَ وَالْوَلِيدِ بْنِ عُتْبَةَ وَأَبِي جَهْلِ بْنِ هِشَامٍ فَأَشْهَدُ بِاللَّهِ لَقَدْ رَأَيْتُهُمْ صَرْعَى قَدْ غَيَّرَتْهُمْ الشَّمْسُ وَكَانَ يَوْمًا حَارًّا.
Maana yake, “Mtume S.A.W. alielekea kibla akawaapiza watu katika Makureshi: Shaiba bin Rabia, na Utba bin Rabia, na Walid bin Utba na Abu Jahil bin Hashim, na namshuhudisha Mwenyezi Mungu nimewaona wameuawa, na jua limewabadilisha (wameanza kuoza) na ilikuwa ni siku ya joto".
*Kutoka kwa Abu Huraira R.A.A. kasema, "Alikuja Tufail bin Amr Al`Daus kwa Mtume S.A.W akasema, "Hakika watu wa kabila la Daus wameasi na wamekataa (kusilimu) waapize Mwenyezi Mungu". Akaelekea Mtume S.A.W. kibla na akainua mikono yake akasema, [3]"
اللَّهُمَّ اهْدِ دَوْسًا وَأْتِ بِهِمْ اللَّهُمَّ اهْدِ دَوْسًا وَأْتِ بِهِمْ.
Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu waongoze kabila la Daus na waachie waje kwetu, Ewe Mwenyezi Mungu waongoze kabila la Daus na waachie waje kwetu".
*Kutoka kwa Bibi Aisha R.A.A.H. kasema, "Niliingia kwa Mtume S.A.W. naye alikuwa kavaa kikoi na joho la kuogea akaelekea kibla na akanyoosha mikono yake akaomba,[4] “
اللَّهُمَّ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ فَأَيَّ عَبْدٍ مِنْ عِبَادِكَ ضَرَبْتُ أَوْ آذَيْتُ فَلَا تُعَاقِبْنِي بِهِ.
Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu mimi ni mwanadamu ikiwa nimempiga mja yeyote yule katika waja wako, au nimemuudhi basi usiniadhibu kwa ajili hiyo".
III. Kuinua mikono wakati wa kuomba dua.
Kasema Uthman bin Abi Shaiba kutoka kwa Ibn Umar R.A.A. kuwa, [5] "
ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ عَنْهُمَا أَنَّهُ كَانَ يَرْمِي الْجَمْرَةَ الدُّنْيَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ يُكَبِّرُ عَلَى إِثْرِ كُلِّ حَصَاةٍ ثُمَّ يَتَقَدَّمُ حَتَّى يُسْهِلَ فَيَقُومَ مُسْتَقْبِلَ الْقِبْلَةِ فَيَقُومُ طَوِيلًا وَيَدْعُو وَيَرْفَعُ يَدَيْهِ ثُمَّ يَرْمِي الْوُسْطَى ثُمَّ يَأْخُذُ ذَاتَ الشِّمَالِ فَيَسْتَهِلُ وَيَقُومُ مُسْتَقْبِلَ الْقِبْلَةِ فَيَقُومُ طَوِيلًا وَيَدْعُو وَيَرْفَعُ يَدَيْهِ وَيَقُومُ طَوِيلًا ثُمَّ يَرْمِي جَمْرَةَ ذَاتِ الْعَقَبَةِ مِنْ بَطْنِ الْوَادِي وَلَا يَقِفُ عِنْدَهَا ثُمَّ يَنْصَرِفُ فَيَقُولُ هَكَذَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَفْعَلُهُ.
Maana yake, “Ibn Umar R.A.A. alikuwa akipiga mnara wa Jamarat al Dunya kwa vijiwe vidogo, (na alikuwa) akikabir[6] kwa kila kijiwe, halafu anajongea mbele mpaka kwenye utambarare atasimama kuelekea kibla, na atasimama kisimamo kirefu akiomba, na (huku) ameinua mikono yake, halafu anapiga mnara wa katikati, halafu atakwenda kushotoni kwenye tambarare, na atasimama kisimamo kirefu na anaomba, na ameinua mikono yake, na atasimama kisimamo kirefu, halafu atapiga mnara wa Jamarat al Aqaaba katikati ya bonde na wala hasimami pale, halafu ataondoka, na anasema, "Hivi ndivyo nilivyomuona Mtume S.A.W. akifanya" (yaani Mtume S.A.W. alikuwa akiinua mikono yake wakati wa kuomba).
*Kutoka kwa Abi Mussa R.A.A. kasema, "Aliomba Mtume S.A.W. maji akatawadha halafu akainua mikono yake akasema, [7]"
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِعُبَيْدٍ أَبِي عَامِرٍ وَرَأَيْتُ بَيَاضَ إِبْطَيْهِ فَقَالَ اللَّهُمَّ اجْعَلْهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَوْقَ كَثِيرٍ مِنْ خَلْقِكَ مِنْ النَّاسِ.
Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu msamehe Ubaid Abi Aamir” na nikaona weupe wa kwapa zake akasema, "Ewe Mwenyezi Mungu mjalie siku ya kiyama awe na cheo cha juu katika waja Wako".
*Kutoka kwa Ibn Abbas R.A.A. kutoka kwa Mtume S.A.W kasema, [8]"
لَا تَسْتُرُوا الْجُدُرَ مَنْ نَظَرَ فِي كِتَابِ أَخِيهِ بِغَيْرِ إِذْنِهِ فَإِنَّمَا يَنْظُرُ فِي النَّارِ سَلُوا اللَّهَ بِبُطُونِ أَكُفِّكُمْ وَلَا تَسْأَلُوهُ بِظُهُورِهَا فَإِذَا فَرَغْتُمْ فَامْسَحُوا بِهَا وُجُوهَكُمْ.
Maana yake, "Msizifunike kuta[9]. Yeyote atakae angalia (kusoma) barua ya ndugu yake bila idhini yake basi huwa kama anaaangalia moto. Muombeni Mwenyezi Mungu kwa viganja vyenu, na, mkimaliza kuomba dua panguseni nyuso zenu".
IV. Kuwa na unyenyekevu, hamu, khofu, na matarajio.
Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Suratil A`araaf aya ya 55, na aya ya 56, "
﴿ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ﴾ ﴿وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا إِنَّ رَحْمَتَ اللَّهِ قَرِيبٌ مِنَ الْمُحْسِنِينَ﴾.
Maana yake, "Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi warukao mipaka. Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wanao fanya mema".
*Pia kasema Mola Mtukufu katika Surat Anbiyaa aya ya 89, na aya ya 90,"
﴿وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَى رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنْتَ خَيْرُ الْوَارِثِينَ﴾ ﴿فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَى وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ﴾.
Maana yake, "Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi. Basi tukamwitikia, na tukampa Yahya na tukamponyeshea mkewe. Hakika wao walikuwa wepesi wa kutenda mema, na wakituomba kwa shauku na khofu. Nao walikuwa wakitunyenyekea".
*Pia kasema Mola Mtukufu katika Surat Assajdah aya ya 16, na aya ya 17, "
﴿تَتَجَافَى جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنْفِقُونَ﴾ ﴿فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴾.
Maana yake, "Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku. Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda".
V. Kuihifadhi sauti kuwa ya wastani.
Wakati mtu anapoomba dua akiwa peke yake, au sehemu kuna watu, basi asiipaze sauti yake ikawakera wengine, na wala isiwe ndogo sana, lakini iwe yenye kusikilizika kidogo kwake mwenyewe.
*Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat al A`araaf aya ya 205, "
﴿وَاذْكُرْ رَبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنَ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ وَلَا تَكُنْ مِنَ الْغَافِلِينَ﴾.
Maana yake, “Na mkumbuke Mola Mlezi wako nafsini kwako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni. Wala usiwe miongoni wa walio ghafilika”.
*Pia kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Qaaf aya ya 16, "
﴿وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ﴾.
Maana yake, “Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake”.
*Kutoka kwa Musa al Ash`ari R.A.A. kasema, "Alikuwa pamoja na Mtume S.A.W. wakati na wao wanapanda kilima, mtu mmoja akawa kila akipanda kilima anasema kwa sauti, "LAA ILAAHA ILLA LLAAH WALLAHU AKBAR" Mtume S.A.W. akamwambia, [10]"
إِنَّكُمْ لَا تُنَادُونَ أَصَمَّ وَلَا غَائِبًا.
Maana yake, "Nyinyi hamumuombi kiziwi wala yule ambaye hayuko".
*Ametuambia Abu Rabiy`a Zayd bin `Auf L-`Aamiry L-Basary kasema, "Katuambia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit L-Bannaniy, kutoka kwa Abi `Uthmaan Nnahdiy kwamba Abu Musa L-Ash`ary kasema, "Tulikuwa pamoja na Mtume wa Mola (S.A.W.) katika safari, tulipokuwa tunaukaribia mji wa Madina watu wakapiga Takbiyr, na wakapaza sauti zao kisha Mtume (S.A.W.) akasema,[11]"
يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّكُمْ لاَ تَدْعُونَ أَصَمَّ وَلاَ غَائِبًا إِنَّ الذِي تَدْعُونَهُ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ أَعْنَاقِ رِكَابِكُمْ.
Maana yake, “Enyi watu! Kwa hakika nyinyi hamumuombi kiziwi wala asiye kuwepo. Hakika mnaemuomba yupo kati yenu, na baina ya shingo za vipando vyenu”. Kisha akasema, "
يَا أَبَا مُوسَى هَلْ أَدُلُّكَ عَلَى كَنْزٍ مِنْ كُنُوزِ الْجَنَّةِ؟.
Maana yake, “Ewe Aba Musa! Jee, nikwambie kuhusu moja ya khazina za Peponi? Kasema, "Nikasema, "Ni nini hiyo ewe Mtume wa Allah?, Akasema, "La Hawla wala Quwwata illa bi-Llaah”. Kasema Jaabir R.A.A., "Maana ya kauli ya Mtume (S.A.W.) kwetu sisi, "
إِنَّ الذِي تَدْعُونَهُ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَ أَعْنَاقِ رِكَابِكُمْ.
Maana yake, “Hakika ambae mnamuomba yupo kati yenu, na baina ya shingo za vipando vyenu”. Hayo ni kwa maana ya maneno ya Mola Mtukufu, "
﴿مَا يَكُونُ مِن نَّجْوَى ثَلاَثَةٍ اِلاَّ هُوَ رَابِعُهُمْ وَلاَ خَمْسَةٍ اِلاَّ هُوَ سَادِسُهُمْ وَلآ أَدْنَى مِن ذَالِكَ وَلآ أَكْثَرَ إِلاَّ هُوَ مَعَهُمُ, أَيْنَ مَا كَانُوا﴾[13]
Maana yake, "Haupatikani mnong`ono wa watu watatu ila Yeye huwa ni wa nne wao, wala watano ila Yeye huwa ni wa sita wao, wala wa wachache kuliko hao wala zaidi ila Yeye huwa pamoja nao popote walipo". Na Akasema, "
﴿وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ ﴾[14]
Maana yake, "Na Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni (mwake). [15]
VI. Kumtukuza Mola Mtukufu na kumsalia Mtume S.A.W.
Kabla ya kuomba dua kwanza inapendeza kumtukuza Mola Mtukufu, kumhimidi, na kumsalia Mtume S.A.W. Kutoka kwa Fadhalah bin Ubaid kasema, "Wakati alipokua amekaa aliingia mtu mmoja akasali halafu akasema, “
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي.
Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe, na unionee huruma". Akasema Mtume S.A.W., [16]"
عَجِلْتَ أَيُّهَا الْمُصَلِّي إِذَا صَلَّيْتَ فَقَعَدْتَ فَاحْمَدْ اللَّهَ بِمَا هُوَ أَهْلُهُ وَصَلِّ عَلَيَّ ثُمَّ ادْعُهُ.
Maana yake, "Umefanya haraka, ewe mwenye kusali, ukimaliza kusali na kukaa kwa ajili ya kuomba dua basi umhimidi[17] Mwenyezi Mungu kama Anavyostahiki, halafu niombee dua mimi, halafu tena muombe Mwenyezi Mungu".
*Kutoka kwa Muawiya bin Abu Sufiani R.A.A. kasema, "Nimemsikia Mtume S.A.W. akisema, [18]"
مَنْ دَعَا بِهَذِهِ الْكَلِمَاتِ الْخَمْسِ لَمْ يَسْأَلِ اللهَ شَيْئًا إِلَّا أَعْطَاهُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَاللهُ أَكْبَرُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيْكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ اْلحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيْرٌ لاَ إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَلاَ حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللهِ.
Maana yake, "Atakaeomba kwa maneno haya matano, hatomuomba Allah chochote kile isipokuwa atampa: Laa Ilaha illa Llahu, waLlahu Akbar, Laa ilaha illa Llahu, wahdahu la sharika lahu, lahu L`Mulku, wa lahu l`hamdu wa huwa ala kulii shain qdiir, Laa ilaha illa Llahu, wala haula wala quwwata ila billah.
Maana yake, “Hapana anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na Allah ni mkubwa kuliko kila kitu. Hapana anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Peke Yake hana mshirika, ufalme ni Wake, na sifa zote njema na shukrani zote ni Zake. Hapana anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, naye ni muweza wa kila jambo. Hapana anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na wala hakuna nguvu wala uwezo isipokuwa wa Allah".
*Kutoka kwa Abdillahi bin Buraidah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Mtume S.A.W., "Kuwa alimsikia mtu mmoja akisema, "
اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ أَنِّي أَشْهَدُ أَنَّكَ أَنْتَ اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ الْأَحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ كُفُوًا أَحَدٌ.
Allahumma innii as`aluka annii ash`hadu annaka anata Llahu la Ilaha ila anta Al`Ahadu, As`Samadu, Al`ladhi lam yalid wa lam yuulad wa lam yakun lahu kufuan Ahad.
Maana yake, "Ewe Allah ninakuomba, (huku) ninashuhudia kuwa Wewe ni Allah Hakuna mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe, Mmoja, Anayetegemewa, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa, na wala hakuna anayefanana Naye" Akasema Mtume S.A.W., [20]"
لَقَدْ سَأَلْتَ اللَّهَ بِالِاسْمِ الَّذِي إِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى وَإِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ
Maana yake, "Kwa hakika umemuomba Mwenyezi Mungu kwa jina ambalo akiombwa kwalo basi hutoa, na akiombwa dua basi hujibu".
VII. Kuwa na dhana nzuri.
Kutoka kwa Abu Huraira R.A.A. kasema, "Kasema Mtume S.A.W., [21]"
يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي وَأَنَا مَعَهُ إِذَا ذَكَرَنِي فَإِنْ ذَكَرَنِي فِي نَفْسِهِ ذَكَرْتُهُ فِي نَفْسِي وَإِنْ ذَكَرَنِي فِي مَلَإٍ ذَكَرْتُهُ فِي مَلَإٍ خَيْرٍ مِنْهُمْ وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ بِشِبْرٍ تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا وَإِنْ تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا وَإِنْ أَتَانِي يَمْشِي أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً.
Maana yake, "Anasema Mola Mtukufu, "Mimi ni karibu na fikra za mtu anaponifikiria, na Mimi niko nae anapo nidhukuru (kunitaja, kunikumbuka), na akinikumbuka katika moyo wake, basi namkumbuka katika nafsi Yangu, na akinikumbuka katika kikao, namkumbuka katika kikao kilicho bora kuliko alichonikumbukia, na akinisogelea kwa shubiri namsogelea kwa dhiraa, na akinisogelea kwa dhiraa namsogelea kwa pima, na akija kwangu huku anatembea, namuendea kwa haraka"
VIII. Kukiri dhambi.
Kutoka kwa Saad bin Abi Waqas R.A.A. kasema, "Kasema Mtume S.A.W., "[25]
دَعْوَةُ ذِي النُّوْنِ إِذْ دَعَا وَ هُوَ فِيْ بَطْنِ الْحُوْتِ ﴿لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنَ الظَّالِمِينَ﴾ إِنَّهُ لَمْ يَدَعْ بِهَا مُسْلِمٌ فِيْ شَيْءٍ قَطَّ إِلَّا اسْتَجَابَ اللهُ لَهُ بِهَا.
Maana yake, "Dua ya Dhin-Nun aliyo omba naye yuko katika tumbo la nyangumi Laa ilaha illa Anta Subh`hanaka inni kuntu mina dh`dhalimiin.[26]. Hapana mungu isipo kuwa Wewe Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu. "Hakika haombei Muislam kwa chochote katu isipokuwa Mwenyezi Mungu atamjibu".
*Kutoka kwa Saad R.A.A., "Kasema Mtume S.A.W., [27]"
لَقَدْ كَانَ دُعَاءُ أَخِيْ يُوْنُسَ عَجَبًا، أَوَّلُهُ تَهْلِيْلٌ، وَأَوْسَطُهُ تَسْبِيْحٌ، وَآخِرُهُ إِقْرَارٌ بِالذَّنْبِ، ﴿لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنْتُ مِنَ الظَّالِمِينَ﴾. مَا دَعَا مَهْمُوْمٌ وَلَا مَغْمُوْمٌ وَلَا مَكْرُوْبٌ وَلاَ مَدْيُوْنٌ فِي يَوْمٍ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ إِلَّا اسْتُجِيْبَ لَهُ.
Maana yake, "Hakika dua ya ndugu yangu Yunus ilikuwa inastaajabisha, mwanzoni Tahlil[28], na katikati yake Tasbih, na mwisho wake kukiri kwa dhambi, Laa ilaha illa Anta Subh`hanaka inni kuntu mina dh`dhalimiin.[30]. Haombi mwenye huzuni, wala mwenye majonzi, wala mwenye dhiki (usumbufu, mateso), na wala mwenye deni, kila siku mara tatu isipokuwa atajibiwa".
*Kutoka kwa Abu Huraira R.A.A., kasema, “Kasema Mtume S.A.W., "Hakika dua yenye kuleta mafanikio (bora) aseme mtu, "[31]
اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي وَأَنَا عَبْدُكَ ظَلَمْتُ نَفْسِي وَاعْتَرَفْتُ بِذَنْبِي يَا رَبِّ فَاغْفِرْ لِي ذَنْبِي إِنَّكَ أَنْتَ رَبِّي إِنَّهُ لَا يَغْفِرُ الذَّنْبَ إِلَّا أَنْتَ.
Allahumma anta Rabbi wa ana abduka, dhalamtu nafsi, wa ataraftu bidhambi, yaa Rabbi fagh`fir lii dhambi, innaka anta Rabbi innahu la yagh`firu dhambi illa ant.
Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu, Wewe ni Mola wangu na mimi ni mja Wako, nimeidhulumu nafsi yangu, na nakiri kwa makosa yangu, Ewe Mola wangu Nisamehe madhambi yangu, hakika hakuna anaesamehe madhambi isipokuwa Wewe".
IX. Kuirudia dua mara tatu.
Kutoka kwa Abdillah bin Masoud R.A.A. kasema, [32]"
كَانَ أَحَبُّ الدُّعَاءِ إِلَى رَسُوْلِ اللهِ أَنْ يَدْعوَ ثَلَاثًا.
Maana yake, "Alikuwa Mtume S.A.W. anapoomba dua anapenda kuirudia mara tatu".
X. Ajiombee kwanza yeye halafu amuombee mwingine.
*Kutoka kwa Ubay bin Ka`ab R.A.A. kutoka kwa Mtume S.A.W.[33],
كَانَ إِذَا ذَكَرَ أَحَدًا فَدَعَا لَهُ بَدَأَ بِنَفْسِهِ.
Maana yake, "Alikuwa Mtume S.A.W. akimtaja mtu na akataka kumuombea dua, basi kwanza anaanza kujiombea mwenyewe"
Na mifano mizuri ni ile inayotokana na Mitume ya Mwenyezi Mungu A.S. kama ifuatavyo:
*Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Suratil A`araaf aya ya 151, "
﴿قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَلِأَخِي وَأَدْخِلْنَا فِي رَحْمَتِكَ وَأَنْتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ﴾.
Maana yake, "(Musa) akasema: Mola Mlezi wangu! Nisamehe mimi na ndugu yangu, na ututie katika rehema Yako. Nawe ni Mwenye kurehemu kushinda wote wenye kurehemu".
*Pia kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Ibrahim aya ya 41, "
﴿رَبَّنَا اغْفِرْ لِي وَلِوَالِدَيَّ وَلِلْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ يَقُومُ الْحِسَابُ﴾.
Maana yake, "Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili, na Waumini, siku ya kusimama hisabu".
*Pia kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Suratil H`ashri aya ya 10, "
﴿وَالَّذِينَ جَاءُوا مِنْ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ﴾.
Maana yake, "Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu”.
XI. Awe na uhakika wa kukubaliwa.
Kila wakati mtu anapoomba dua basi awe na yakini[34] yakujibiwa dua yake ili mradi hakuomba maasi au kukata udugu.
*Kutoka kwa Abu Huraira R.A.A. kasema, "Kasema Mtume S.A.W., [35]"
لاَ يَقُولَنَّ أَحَدُكُمْ: اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي إِنْ شِئْتَ، اللَّهُمَّ ارْحَمْنِي إِنْ شِئْتَ، وَلَكِنْ لِيَعْزِمْ عَلَى الْمَسْأَلَةِ، فَإِنَّهُ لاَ مُكْرِهَ لَهُ.
Maana yake, “Asiseme mmoja wenu (wakati anapoomba dua): “Ewe Allah! Nisamehe ukitaka. Ewe Allah! Nirehemu ukitaka. Bali aazimie (kwa kusudio la kujibiwa) katika maombi yake. Kwani Yeye hapana wa kumlazimisha”.
XII. Ahitimishe dua kwa kusema Amiin.
Kasema Zuhairy Numairy R.A.A., "Tulitoka usiku mmoja pamoja na Mtume S.A.W. na tukamkuta mtu mmoja alikuwa akiomba dua kwa king`ang`anizi (kuirudia rudia) na unyenyekevu. Mtume S.A.W. alisimama akisikiliza akasema, [36]"
أَوْجَبَ إِنْ خَتَمَ فَقَالَ رَجُلٌ مِنْ الْقَوْمِ بِأَيِّ شَيْءٍ يَخْتِمُ قَالَ بِآمِينَ فَإِنَّهُ إِنْ خَتَمَ بِآمِينَ فَقَدْ أَوْجَبَ فَانْصَرَفَ الرَّجُلُ الَّذِي سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَتَى الرَّجُلَ فَقَالَ اخْتِمْ يَا فُلَانُ بِآمِينَ وَأَبْشِرْ.
Maana yake, “Atajibiwa ikiwa ataikamilisha" Akasema mmoja wetu, "Ataikamilisha kwa kitu gani?". Akasema Mtume S.A.W., "Kwa (kusema) Amin, basi akiikamilisha kwa Amin hapana shaka dua yake itakubaliwa". Yule mtu aliemuuliza Mtume S.A.W. akamuendea yule mtu aliyekuwa akiomba dua akamwambia, "Ewe fulani ikamilishe dua yako kwa kusema "Amiin". Na bashiri bishara njema (yaani uwe na tamaa ya kujibiwa)".[37]
Mifano ya masafa na vipimo huongewa na viumbe wenye kuumbwa, kwani tukiangalia kwa makini, tutaona kiumbe akikaribia sehemu fulani huwa mbali na nyingine. Na akiwa katika mahali fulani, huwa hayupo sehemu nyingine, kwa sababu masafa yanahitajia kuondoka na kusafiri safiri mara hapa, na mara kule. Lakini Allah Mtukufu yuko mbali na upungufu huo.
|