Published By Said Al Habsy  Mimi ni mvulana ninaefikia umri wa miaka 19 na wakati wa ndoa yangu umekaribia; nilipomuuliza mmoja wa rafiki zangu waliooa kuhusu kujitoharisha baada ya kuingiliana na mke kanijibu kwa namna isiyo bayana. Naomba kufahamishwa kuhusu tohara baada ya maingiliano ?
Tohara baada ya maingiliano ni kuoga janaba kule kule kunakowajibika kwa kuota usingizini maingiliano na mfano wa hayo, na kuoga huko ni kuosha najsi kwanza, kisha kutawadha au kutosheka na kusukutua na kuingiza maji puani, kisha kuosha kichwa na kuueneza mwili kwa maji pamoja na kuyafikisha maji kwa mkono kwenye sehemu za mwili zilizojificha kama kitovuni, makutanoni mwa mapaja na kwapani. Na Allah anajua zaidi. |