Published By Said Al Habsy  Je nguo za mwenye janaba hunajisika kwa jasho lake ? Na je hunajisika nguo za mwenye hedhi na mwenye nifasi kwa jasho lao ?
Mwili wa mwenye janaba si najsi hata zinajisike nguo zilizogandana nao, na vivyo hivyo mwenye hedhi na mwenye nifasi. Kuamrishwa wao kuoga si kwa kuwa wao ni najsi, bali ni amri ya kiibada kama vile kuosha viungo vya udhu kutokana na hadathi ndogo. Dalili juu ya hayo ni nyingi. Kati yake ni kwamba Mtume –rehma za Allah na amani zimshukie- alikuwa akisalia nguo anayojifunikia akimuingilia mkewe. Pia kauli yake kwa Bibi Aisha –Allah amridhie-, "Nipe mkeka wa kusujudia", yeye akasema: mimi nimo kwenye hedhi! Akamwambia, "Hedhi yako haimo mkononi mwako". Na alikuwa –rehma za Allah na amani zimshukie- akilala pamoja na wakeze wakiwa katika hali ya hedhi na mwili wake ukigusana na miili yao. Na Allah anajua zaidi.
|