Published By Said Al Habsy  Mtu hawezi kusema kwasababu ya maradhi ya kudumu vipi atasali na kufunga ?
Anapaswa asali kwa moyo na afanye kila analoweza kama rukuu, sujudu, kusimama na kukaa; asiloweza kufanya amesameheka. Vile vile inamlazimu saumu akiwa anaiweza; akiwa hawezi kufunga alishe maskini mmoja kwa kila siku. Hayo ikiwa akili yake nzima, ama akipoteza akili atakuwa si mkalifiwa na hakitamlazimu chochote. Na Allah anajua zaidi. |