Published By Said Al Habsy  Kama nimeingia msikitini kabla ya adhana ya magharibi kwa kiasi nusu saa, je nisali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti au la ?
Kwa kuwa jua wakati huo linakuwa limeanza kuwa manjano usisali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, na inakutosha kuleta dhikri ya albaaqiyaatu a’saalihaatu kabla hujakaa (yaani subhana’Llah, walhamduli’Llah, wala ilaha illa’Llah, wa’Llahu akbar, wala hawla wala quwwata illa bi’Llah). Na Allah anajua zaidi. |