Published By Said Al Habsy  Je ni kweli kuwa mmetoa fatwa kwamba sala ya watu inabatilika ikiwa aliye nyuma ya imam (sutra) amerefusha nguo yake ikafunika vifundo vya miguu? Kama hilo ni kweli nini kosa la yule aliye mwisho wa safu naye hakurefusha nguo yake ? Kisha sisi tuna mtihani wa bwana mmoja mtu mzima daima anakuwa sutra naye haachi kurefusha nguo yake, na anasema suala la kubatilika sala ya mwenye kurefusha nguo halikuwapo katika enzi za maimamu, na kwamba kurefusha nguo kumeharamishwa kukiwa kunakusudiwa kujiona ; nini jawabu yenu kwake ?
Fatwa hiyo ni kweli nayo ni katika ambayo haipasi watu watafautiano juu yake kwa vile imethibiti kuwa sala ya mweye kurefusha nguo inabatilika kwa dalili ambazo hazina shaka usahihi wake. Na anayekikabili kisogo cha imamu chote peke yake ikiharibika sala yake inaharibika sala ya safu yake bila khilafu. Penye khilafu ni pale iwapo atashirikiana naye kukabili kisogo cha imamu japo kidogo mtu ambaye sala yake ni sahihi. Suali la nini kosa la wengineo walio mwishoni mwa safu katika lile alifanyalo huyu aliyesimama nyuma ya imamu ni suali lisilostahili kuulizwa ; kwani usahihi na uharibifu wa sala ni katika yanayokhusu maelezo ya wasfu si katika yanayohusu maelezo ya ukalifisho, na kwa hiyo haishurutishwi humo kufanya kwa makusudi ili kuharibu sala. Mfano wake ni kama hadathi inayotengua udhu hata akiwa aliyeifanya hakukusudia. Unaonaje kama mtu atasali na najsi bila kujua ; huyu hana kosa akibakia hajui kwa kuwa ukalifisho umemuondokea, lakini wajibu wa kulipa sala hautamuondokea atakapojua kwa vile sala yake imeharibika, kwasababu uharibifu wa sala ni katika maelezo ya wasfu. Basi halikadhalika kuhusu suala hili. Na madai ya huyo aliyeshikilia kurefusha nguo asiyejali ya kwamba kauli hii haikujulikana katika enzi za maimamu ni uongo mtupu unao onesha ujinga wa mwenye kuyasema na kuendelea kwake kuvutiwa na batili ; kwani yanajulikana yaliyopokewa kwa hao maimamu yakishuhudia kinyume na madai yake. Kisha inatosha Sunna ya Mtume wa Allah –rehma za Allah na amani zimshukie- iliyotoa maamuzi juu ya hilo. Na madai ya kwamba uharamu wa kurefusha nguo umeambatishwa na kujiona si kweli na tumebainisha vipi madai hayo si kweli katika utafiti tulioufanya makhususi kwa suala hilo ambamo tubainisha pia kuwa kurefusha nguo kwenyewe ni kujiona, basi rejea utafiti huo. Na Allah anajua zaidi. |