Maana ya Saumu
Published By SH. Abdullah Al Shueli
Saumu ni neno la Kiarabu lenye maana ya kujizuilia na kitu na kukiacha. Mfano wa kama vile farasi akiwa amejizuilia kutembea tembea au amekataa kula wanasema farasi amefunga. Au upepo ukiwa umesimama wanasema upepo umefunga. Au mtu akikaa kimya bila ya kuzungumza wanasema mtu huyo amefunga. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Maryam aya ya 26,"
﴿إِنِّى نَذَرتُ لِلرَّحمَنِ صَومًا فَلَن أُكَلِّمَ اْليَومَ إِنسِيًّا﴾.
Maana yake, "Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa (Mwenyezi Mungu) Mwingi wa Rehema ya kufunga, kwa hivyo leo sitasema na mtu." Ama kisheria maana ya neno saumu ni kujizuilia na vitu maalum vinavyofunguza, kwa wakati maalum ambao uko baina ya kuingia kwa alfajiri, mpaka kuzama kwa jua, kwa shuruti maalum, na kwa nia ya kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na kufanya ibada. |
Published By Said Al Habsy  Saumu ni moja ya nguzo ya dini ya Kiislamu iliyothibiti kutokana na kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Hadithi za Mtume Wake S.A.W., kama ifuatavyo. Kasema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Al-Baqara aya ya 183,"
﴿يَأيُّها الَّذِينَ ءَامَنُوا كُتِبَ عَلَيكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الّذِينَ مِن قَبلِكُم لَعَلَّكُم تَتَّقُونَ﴾.
Maana yake, "Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mwenyezi Mungu." Pia Kasema katika Surat Al-Baqara aya ya 185, “
﴿فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ﴾.
Maana yake, “Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu na afunge”. Ziko Hadithi nyingi za Mtume S.A.W., zinazoelezea kuwepo na kuwajibika kwa funga ya mwezi wa Ramadhani, ambazo tutazitaja baadhi yake kwa muhtasari, katika sehemu tofauti kufuatana na mahitajio yake. Kutoka kwa Ibn Umar R.A.A. kasema, "Kasema Mtume S.A.W
[1] Bukhariy 1/11(7), Muslim 1/102 (20).
|
3. SAUMU KABLA YA UISILAMU.
Published By Said Al Habsy  Saumu ilikuwa pia ni wajibu kwa umma nyingine zote zile zilizopita kabla. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Suratil Baqara aya ya 183, “
﴿يَأيُّها الَّذِينَ ءَامَنُوا كُتِبَ عَلَيكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الّذِينَ مِن قَبلِكُم﴾.
Maana yake, "Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu." Lakini kwa kadiri siku zilivyokuwa zinapita, na baada ya kuondoka Mitume ya umma zile, waliifanyia saumu mabadiliko kukidhi haja zao na matamanio yao. Mipaka yake ikarukwa na lengo na kusudio hasa la Saumu ikabadilika.
Leo hii katika kila dini duniani kuna athari ya funga, lakini athari hizo katika dini hizo hazilingani kabisa na funga zile za asili ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu alizo wakusudia waja wake. Mfano Nabii Musa A.S. alikuwa akifunga siku 40, na pia Nabii Issa A.S. yeye na wafuasi wake walikuwa wakifunga siku 40. Na Manasara walikuwa wakifunga mwezi mzima wa Ramadhani, lakini mwezi huo ulipoangukia wakati wa joto, basi wanavyuoni wao wakaamuwa kutokufunga wakati huo kwa ajili ya shida ya joto na badala yake wafunge siku nyingine za wakati wa baridi. Kwa ajili ya kubadilisha mwezi wa saumu wakaongeza ziada siku 10 za kufunga ili iwe kafara na toba yake na wakawa wakifunga siku 40, siku hizi zinajulikana maarufu kwao kama kwaresima
[1] Siku arubaini za mfungo wa Wakristo kabla ya sikukuu ya Pasaka.
|