Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi  Amesema Abu Sufiyan Mahboub bin Ruhail (r.a): "Na ambayo yamepokewa kwetu kutoka kwa Jabir bin Zaid -Rehma za Allah ziwe kwake-, kua yeye aliulizwa: Ni yapi yenye wasaa kwa watu ujinga wake? Basi alisema: ((Ni yale waliyoitakidi uharamu wake ikiwa tu hawajayafanya, au kumpenda aliyeyafanya, au kujitenga na wanaelimu iwapo watajitenga na aliyeyafanya, au kusimama kwa kutowapenda wala kutowachukia))
Amesema Mahboub (r.a): "Ufafanuzi wa aliyosema Jabir bin Zaid wakati alipoulizwa kuhusu yaliyokua na wasaa kwa watu ujinga wake naye akasema: ((Ni yale waliyoitakidi uharamu wake ikiwa tu hawajayafanya, au kumpenda aliyeyafanya, au kujitenga na wanaelimu iwapo watajitenga na aliyeyafanya, au kusimama kwa kutowapenda wala kutowachukia)) hayo ni kua lau mtu hakujua kama ulevi ni haramu wala nguruwe ni haramu na mfano wake miongoni mwa aliyoyaharamisha Allah na hali yeye ni mwenye kuyaramisha, basi huyo yumo katika wasaa wa hilo ikiwa hatoyajua hayo kama yaalivyo, ikiwa hakula nguruwe au hakunywa ulevi au akampenda mwenye kuyafanya hayo au akawachukia Maulamaa iwapo watachukia mwenye kuyafanya hayo, au akasimama kwa kutowapenda wala kuwachukia." |