Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi  Wayahudi na Wasabiina na Wakiristo na Wamajusi; hakika wao ni Wapotevu na Washirikina; kwa sababu hawamuamini Mtume Muhammad (s.a.w), basi hata kama atapatikana katika wao anayeshika Dini yake halitomtosha hilo chochote mbele ya Allah na hukumu yake, bali inalazimika juu yake kuamini Utume wa Muhammad (s.a.w) na kuyakubali aliyo kuja nayo Muhammad (s.a.w) na kukubali kufanya Ibada kwa mujibu wa Sheria ya Muhammad (s.a.w), kwa sababu Sheria ya Muhammad (s.a.w) ni yenye kukalia Sheria zote zilizokua kabla yake, na imekuja katika Hadithi:
(Lau kuwa Mussa yuko hai basi asingeli pata nafasi isipokua ya kunifuata mimi).
Ikiwa hiyo ndiyo hukumu ya Mtume Mussa (a.s.w) wanayemkubali wote hao, basi hukumu hiyo inawalazimu zao wao.Basi watu wa mila hizo wote ikiwa ipo Dola ya Kiislamu na wao wapo katika mamlaka ya mipaka yake, atawaita Kiongozi wa Dola ya Kiislamu na kuwalingania katika kuingia ndani ya Uislamu, na ikiwa watakubali basi hapo watakuwa ni Waislamu, na watapata wao wanayopata waislamu na yatalazimika juu yao yanayolazimika juu ya waislamu.
Na ikiwa watakataa kuingia katika Uislamu hapo atawapa khiyari ya kuingia katika hukumu ya Jizya (kodi maalumu) watakayotoa wakiwa wanyonge, na hakuna katika Jizya kiwango maalumu, lakini itakua kama atakavyoona Kiongozi, na hiyo Jizya italazimika kwa wale wanaoweza kupigana tu katika wao, na sio kwa Mwanamke, wala Mzee mkongwe, wala Mtoto, wala Mkuu wao wa Dini ambae hashughuliki isipokua na Ibada zake, Mkuu huyo ni yule asiyekua marejeo yao katika mambo yao ya kivita dhidi ya Uislamu na Waislamu katika rai, basi ikiwa watatoa Jizya watapata haki ya Dhimma ya Waislamu, haki hiyo ni kuzuia kuwafikia wao katika Madhara yale wanayozuia Waislamu kufika katika Nafsi zao, basi italazimika kwa Dola ya Kiislamu izuie mwenye kutaka kuwadhulumu (Himaya).
Na ikiwa wamekataa kutoa Jizya ya Unyonge basi itakua ni haki kwa Dola ya Kiislamu kuwapiga vita, na hatoondosha kwao hukumu ya vita, na atachukua Ngawira katika mali zao, na kuteka wanawake wao na vizazi vyao mpaka wakubali Uislamu au watoe Jizya ya unyonge.
|