Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi  Shafaa (Uombezi) ni kuomba mazuri kwa ajili ya mwengine, na mazuri hayo ima kupandishwa cheo cha huyo mwengine au kumuokoa na kuangamia.
Basi ataombea yule ambae atapata Idhini ya Allah mtukufu, na ataombea kwa ajili ya yule ambae ameridhiwa na Allah mtukufu.
﴿مَن ذَا ٱلَّذِى يَشْفَعُ عِندَهُ إِلاَّ بِإِذْنِهِ﴾
﴾Ni nani huyo ambae ataombea kwake yeye isipokua kwa Idhini yake?﴿
[Baqara 255]
﴿وَلاَ يَشْفَعُونَ إِلاَّ لِمَنِ ٱرْتَضَىٰ﴾
﴾Na hawataombea isipokua kwa yule ambae amemridhia (Allah mtukufu)﴿
[An-biyaai 28]
Basi kwa hakika hakuna Muombezi yoyote atakayeombea mwenye kuidhulumu nafsi yake kwa maasi ya Ushirikina au kwa maasi makubwa yasiyo kuwa ya kishirikina na hali alikufa bila ya kutubia kwa Allah kutokana na udhalimu wake.
﴿وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ ٱلاْزِفَةِ إِذِ ٱلْقُلُوبُ لَدَى ٱلْحَنَاجِرِ كَـٰظِمِينَ مَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلاَ شَفِيعٍ يُطَاعُ﴾
﴾Na waonye wao kwa siku yenye kukaribia (siku ya Kiama); wakati nyoyo zitakapokua karibu ya makoromeo hali wamefazaika; hakuna kwa Madhalimu([1]) kipenzi yoyote wala muombezi yoyote atakayetiiwa﴿
[Ghaafir 18]
Na kwa hakika Allah mtukufu ameshatubainishia katika Kitabu chake ni nani walio madhalimu, na sisi ni wenye kusadikisha hukumu ya Allah mtukufu na hakuna mkweli zaidi kuliko yeye, basi ametuambia.
﴿وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ﴾
﴾Na mwenye kuichupa mipaka ya Allah basi hao ndio Madhalimu﴿
[Baqara 229]
﴿وَمَن لَّمْ يَتُبْ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ﴾
﴾Na ambae hatotubu basi hao ndio Madhalimu﴿
[Hujuraat 11]
Na Shafaa itakayotoka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w) itakua kwa ajili ya watu wa kisimamo cha Kiama wote kwa ujumla, ili wafanyiwe hesabu zao kisha waende katika mafikio yao ya milele.
Na watapata Waumini katika Umma wake Shafaa maalumu ya kunyanyua daraja zao, vile vile watapata Manabii na Mawalii na Malaika nafasi za kuombea.
Na kwa hakika Maombezi yao hao wote ni kwa wale aliotuelezea Allah mtukufu hali zao katika Neno lake.
﴿وَلاَ يَشْفَعُونَ إِلاَّ لِمَنِ ٱرْتَضَىٰ وَهُمْ مّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ﴾
﴾Na hawaombei isipokua kwa yule ambae amemridhia, na wao kwa kumwogopa yeye ni wenye huruma﴿
[An-biyaai 28]
Na kwa hakika Allah mtukufu haridhii Waovu wenye kuasi ikiwa ni Washirikina au Wanafiki, Amesema Allah mtukufu.
﴾فَإِنَّ ٱللَّهَ لاَ يَرْضَىٰ عَنِ ٱلْقَوْمِ ٱلْفَـٰسِقِينَ﴿
﴾Basi hakika Allah haridhii kwa watu Mafasiki﴿
[Taubah 96] |