Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi  Na hawa Mitume wanazo sifa za lazima kusifika kwa sifa hizo katika Haki yao, na ziko sifa ambazo haiwezekani kwao kuwa nazo, na ziko sifa inafaa kwao kusifika kwa sifa hizo.
1. Sifa za lazima kuwa nazo Mitume
Inalazimika kwa Mitume kuwa ni wenye Amana, Ukweli, Kuhifadhika na mabaya, Ufahamu mkali, Kuzinduka, na Hifadhi itokayo kwa Bwana wao, basi halipatikani kutoka kwao Kosa kubwa, tena hawaachiwi katika Kosa dogo, na wao hawaendi kinyume kwa kuyafanya yale walioamrishwa kuyakataza kwa Waja, na wao hawafichi kitu katika Ufunuo walioamrishwa kuufikisha kwa Waja.
﴿وَمَا هُوَ عَلَى ٱلْغَيْبِ بِضَنِينٍ﴾
﴾Na hakuwa yeye katika Mambo yaliyofichwa ni mwenye ubakhili﴿
[Tak-wir 24]
2. Sifa zilizokua haiwezekani kuwa nazo Mitume
Na haiwezekani kwao wao kuwa ni wenye Khiyana, Uongo, Kutohifadhiwa, Upuuzi, Uzembe, kufanya Makosa makubwa, na kubakia katika Madogo, na kubadilisha kitu katika Ufunuo.
﴿قُلْ مَا يَكُونُ لِى أَنْ أُبَدّلَهُ مِن تِلْقَاء نَفْسِى إِنْ أَتَّبِعُ إِلاَّ مَا يُوحَى إِلَىَّ إِنّى أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبّى عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ﴾
﴾Sema haiwi kwangu mimi nibadilishe kutoka katika ya Nafsi yangu; haikua kwangu isipokua ni kufuata yale ambayo yanafunuliwa kwangu, hakika mimi ninaogopa ikiwa nitamuasi Bwana wangu Adhabu ya siku kubwa﴿
[Yuunus 15]
3. Sifa zinazofaa kuwa nazo Mitume
Na inafaa kwao wao kula, kunywa, kulala, kuingilia kindoa, kuwa na Wake, kupata kizazi, kwenda katika Masoko, kuzungumza katika yanayowahusu, kufanya mizaha inayofaa. |