Published By Sh. Hafidh Al-Sawafi  Na hawa Malaika ni makundi, miongoni mwa wao ni Mitume wa Allah kwa Ufunuo wa Manabii wake kama vile Jibrilu:
﴿نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلاْمِينُ﴾
﴾Amateremka nayo –yaani Qur-ani- Roho wa kuaminiwa –yaani Jibrilu-﴿
[Shuaraa 193]
na miongoni mwa Malaika ni Waandishi wa Matendo ya Waja.
﴿كِرَاماً كَـٰتِبِينَ يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ﴾
﴾Watukufu walio waandishi; wanayajua ambayo munayafanya﴿
[Infitaar 11-12]
Na miongoni mwa hao Malaika wako Wenye kuhifadhi
﴿وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَـٰفِظِينَ﴾
﴾Na hakika kuna juu yenu Wenye kuhifadhi﴿.
[Infitaar 10]
Na miongoni mwa hao Malaika ni Wakhazina wa Moto.
﴿وَسِيقَ ٱلَّذِينَ كَـفَرُواْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ زُمَراً حَتَّى إِذَا جَاءوهَا فُتِحَتْ أَبْوٰبُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مّنكُمْ يَتْلُونَ عَلَيْكُمْ ءايَـٰتِ رَبّكُمْ وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَـاء يَوْمِكُمْ هَـٰذَا قَالُواْ بَلَىٰ وَلَـٰكِنْ حَقَّتْ كَلِمَةُ ٱلْعَذَابِ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ﴾
﴾Na watapelekwa wale ambao wamekufuru katika Jahannamu kwa makundi, mpaka watakapoijia itafunguliwa Milango yake na watasema Wakhazini wake kuwaambia wao: Jee!! Hawakuja kwenu Mitume katika nyinyi wanaosoma kwenu nyinyi Aya za Bwana wenu na wakawa wanahadharisha kwenu makutano ya siku yenu hii? Watasema: Ndio walitujia lakini limekua ni haki Neno la Adhabu juu ya Makafiri﴿
[Zumar 71]
Na miongoni mwa Malaika wako Wakhazini wa Pepo.
﴿ وَسِيقَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوْاْ رَبَّهُمْ إِلَى ٱلّجَنَّةِ زُمَراً حَتَّىٰ إِذَا جَاءوهَا وَفُتِحَتْ أَبْوٰبُهَا وَقَالَ لَهُمْ خَزَنَتُهَا سَلَـٰمٌ عَلَيْكُـمْ طِبْتُمْ فَٱدْخُلُوهَا خَـٰلِدِينَ﴾
﴾Na watapelekwa wale ambao wamemcha Bwana wao katika Pepo kwa makundi, mpaka watakapoijia na ikafunguliwa milango yake na wakasema Wakhazini wake: Amani iko juu yenu, muko vizuri basi iingieni; ni wa kubakia﴿
[Zumar 73]
Na miongoni mwa Malaika ni wale wanaochukua Roho za Waja, na wengine ni wale wanaochukua Arshi.. na wengine wamo katika mengine ambayo Allah amewaumba kwa ajili ya hayo, na akawakhusisha na hayo katika Ibada, na Kuomba msamaha kwa Waumini waliomo katika Ardhi. |