Sheikh Khalfan Mohamed Al-Eiseri (r.a) alizaliwa nchini Burundi katika Kijiji cha Mtaho ndani ya mwaka 1962 naye alianzia malezi yake akiwa na wazazi wake katika nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki ya Kati, hadi ilipofikia mwaka wa 1973 ndipo Baba yake alipomleta katika Ardhi yao ya asili Oman kwa ajili ya masomo na malezi pia, wakati huo Sheikh Khalfan alikuwa na umri wa miaka 11, na baada ya Baba yake -Allah amrehemu- kufariki katika mwaka wa 1974 ndipo Mama yake alipotawalia malezi ya Sheikh Khalfan (r.a). Sheikh Khalfan Al-Eiseri (r.a) alibobea vizuri katika Elimu ya Kidunia, kama alivyobobea vizuri zaidi katika Elimu ya Kidini, pia Allah mtukufu alimtunukia Sheikh Khalfan tunza ya kuweza kuzijua lugha nyingi kuu Ulimwenguni, basi alikua ni mzungumzaji wa Lugha takriban 27 tofauti. Sheikh Khalfan ni Jua la Nuru lililoangaza kila upande wa Dunia kielimu na kitabia na ufundishaji, aliuotoa umri wake kwa ajili ya Allah mtukufu katika njia ya kulingania ulinganio wa Haki, na katika hilo alianzisha Tovuti maarufu iitwayo www.islamfact.com. Sheikh Khalfan Al-aiseri (r.a) alifariki dunia katika mji wa Muscat Oman tarehe 12/5/2015. Allah amrehemu. |