Sala

Sala (160)

Children categories

MAANA YA NENO SALAA KILUGHA,KISHERIA,UMUHIMU NA UTUKUFU WAKE

MAANA YA NENO SALAA KILUGHA,KISHERIA,UMUHIMU NA UTUKUFU WAKE (13)

View items...
FADHILA ZA SALAA

FADHILA ZA SALAA (9)

View items...
HUKUMU ZA ANAYEACHA SALAA.

HUKUMU ZA ANAYEACHA SALAA. (8)

View items...
ADHABU ZA KUACHA SALAA

ADHABU ZA KUACHA SALAA (4)

View items...
WAKATI WA SALAA.

WAKATI WA SALAA. (1)

View items...
WITO WA SALAA (ADHANA).

WITO WA SALAA (ADHANA). (7)

View items...
FADHILA ZA ADHANA.

FADHILA ZA ADHANA. (5)

View items...
MAANA YA ADHANA NA JINSI INAVYOTAMKWA

MAANA YA ADHANA NA JINSI INAVYOTAMKWA (1)

View items...
WITO WA KUANZA KWA SALAA. (IQAMA).

WITO WA KUANZA KWA SALAA. (IQAMA). (3)

View items...
SHURUTI ZA KUKAMILIKA ADHANA NA IQAMA

SHURUTI ZA KUKAMILIKA ADHANA NA IQAMA (4)

View items...
SUNNA ZA ADHANA.

SUNNA ZA ADHANA. (7)

Vifuatavyo ni vitendo vya Sunna wakati wa kuadhini:

View items...
YANAYO HARIBU ADHANA NA IQAMA

YANAYO HARIBU ADHANA NA IQAMA (1)

View items...
YANAYOPENDEZA BAINA YA ADHANA NA IQAMA.

YANAYOPENDEZA BAINA YA ADHANA NA IQAMA. (3)

View items...
SHURUTI ZA SALAA

SHURUTI ZA SALAA (23)

View items...
KUELEKEA KIBLA.

KUELEKEA KIBLA. (4)

View items...
KUONDOKA SHARTI YA KUELEKEA KIBLA

KUONDOKA SHARTI YA KUELEKEA KIBLA (4)

View items...
SITRA ( KIZUIZI CHA KUJULISHA MWISHO WA MSALA)

SITRA ( KIZUIZI CHA KUJULISHA MWISHO WA MSALA) (4)

View items...
NGUZO ZA SALAA.

NGUZO ZA SALAA. (19)

View items...
MAMBO YANAYO HARIBU SALAA

MAMBO YANAYO HARIBU SALAA (9)

Yafuatayo ni mambo ambayo yakifanywa wakati wa Salaa yana haribu Salaa.

 

View items...
VITENDO VYA SUNNA KATIKA SALA

VITENDO VYA SUNNA KATIKA SALA (7)

View items...
YASIYOPENDEZA KUFANYWA KATIKA SALAA

YASIYOPENDEZA KUFANYWA KATIKA SALAA (13)

Kila anaesali anatakiwa awe makini, mwenye kuvihudhurisha viungo na akili zake zote, na ajiepushe na yaliyo katazwa au yale ya kumshughulisha kwani yanaweza kuharibu Salaa yake. Yafuatayo ni miongoni mwa mambo ambayo hayapendezewi kuyafanya wakati wa Salaa

View items...
YANAYORUHUSIWA WAKATI WA SALA

YANAYORUHUSIWA WAKATI WA SALA (7)

Yafuatayo ni yale yanayoruhusiwa kuyafanya wakati wa Salaa kufuatana na mahitajio na dharura ya wakati ule.

View items...
NAMNA YA KULIPA SALAA.

NAMNA YA KULIPA SALAA. (3)

View items...
Written by

Salaa zilizocheleweshwa bila ya sababu ni Salaa zile zilizizo cheleweshwa kwa ajili ya uzembe au uvivu au sababu nyingine ambazo hazikubaliwi kisheria. Na kuchelewesha Salaa kwa uzembe au kwa uvivu au bila ya sababu iliyo ruhusiwa kisheria ni madhambi makubwa. Inabidi Salaa ile ilipwe na aliye ichelewesha atubu.  Ikiwa Salaa zilizo chelewesha ni nyingi basi atazilipa zote wakati ule aliokumbuka isipokuwa wakati ulio haramishwa kusaliwa Salaa. Na ushahidi wakulipa Salaa, ni kwamba kama vile mtu anavyotakiwa kulipa saumu alizoacha, au zaka, ni kiasi hicho hicho kwa Salaa. Kwani hilo ni deni mbele ya Mwenyezi Mungu, na deni la Mwenyezi Mungu lina haki ya kulipwa kwanza kuliko madeni mengine. Kutoka kwa Ibn Abbaas kasema, "Kasema Mtume S.A.W., “[1]

فَاللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ.

 Maana yake, “Deni la Mwenyezi Mungu lina haki ya kulipwa”.

Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuniwezesha kuandika juzu ya pili ya vitabu vya Fiqh. Na kwa vile masuala ya Salaa ni mengi na nimeyaeleza kwa muhtasari, hayakuweza yote kuenea katika kitabu hiki. Kwa hali hiyo nimeyagawa katika sehemu mbili, sehemu ya pili ya kitabu cha Fiqh cha Salaa yaani juzu ya tatu ya vitabu vya Fiqh itakuwa kama ifuatavyo kwa mukhtasari:

1.Salaa ya Jamaa na  hukumu zake. 2. Imam wa Salaa, hukumu na shuruti zake. 3.  Namna ya kusimama wakati wa Salaa. 4. Salaa ya Ijumaa, hukumu na shuruti zake. 5. Salaa ya safari hukumu na shuruti zake. 6. Muda wa safari na maana ya safari. 7. Salaa ya maiti shuruti na hukumu zake. 8. Salaa za Sunna muakkada, za Idi, Witri, sunna za alfajiri, magharibi, tahiyatu masjid, na kadhalika. 9. Salaa zilizo mandub, Salaa za dhuha, taraweh, Salaa ya kuomba mvua. 10. Salaa za nafla, Salaa za usiku, 11.Salaa ya kuomba ushauri kwa Mwenyezi Mungu, na kadhalika. Sijdat sahau na sijdat tilawa. Misikiti haki zake na fadhila zake. Na mambo mengineyo Inshaallah. 

 

والله ولي التوفيق

 DUA.

NAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ALIETUKUKA ATUANDIKE SOTE PAMOJA MIONGONI MWA WAJA WAKE WALE WALIOTUBIA, NA ATUJAALIE KATIKA WAJA WAKE WANAOMWABUDU BILA YA  KUMSHIRIKISHA, NA KATIKA KUNDI LAKE LENYE KUFAULU NA KATIKA VIPENZI VYAKE WAMWOGOPAO, AMIN.

EWE MWENYEZI MUNGU TUNAKUOMBA UTUTENGENEZEE DINI YETU AMBAYO NI KINGA YA MAMBO YETU, NA UTUTENGENEZEE DUNIA YETU AMBAYO YAKO MAISHA YETU, NA UTUTENGENEZEE AKHERA YETU AMBAYO NDIYO MAREJEYO YETU. AMIN.

EWE MWENYEZI MUNGU TUNAKUOMBA USITUACHILIE TUKIWA NA DHAMBI YOYOTE ILE ILA UMEISAMEHE, NA WALA MGONJWA KATI YETU ILA UMEMREJESHEYA AFYA YAKE, NA WALA ALIYEPOTOKA NJIA ILA UMEMWONGOZA, NA WALA ALIE ADUI KWETU ILA UMETUKINGA NAYE, NA UMEMTOSHELEZA[1] Ahmad 5/285 (3224). Mfano wa Hadithi hii imetolewa na Bukhariy 22/293 (6771). 

Written by

Salaa zilizocheleweshwa kwa sababu maalum ambazo haziko katika uwezo wake bila ya kukusudia, kama vile Salaa zilizocheleweshwa kwa sababu ya usingizi, kusahau, au kusali bila ya kuwa na tohara kamili na baadae mtu akakumbuka baada ya muda wa Salaa ile kupita. Salaa za namna hii zinasaliwa mara tu mtu anapokumbuka. Kasema Jaabir bin Zaid R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W., [1]

مَنْ نَسِيَ صَلاَةً أَوْ نَامَ عَنْهَا فَلْيُصَلِّهَا إِذَا ذَكَرَهَا.

Maana yake, “Atakaesahau Salaa au akalala mpaka Salaa ikampita basi aisali atakapoikumbuka.” Na mtu hahisabiwi dhambi kwa kutokukusudia kuichelewesha Salaa. Kasema Ibn Abbas R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W.,[2]

رَفَعَ اللَّهُ عَنْ أُمَّتِي الْخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ، وَمَا لَمْ يَسْتَطِيعُوا، وَمَا أُكْرِهُوا عَلَيْهِ .

Maana yake, “Ameusamehe Mwenyezi Mungu umma wangu makosa (Bila ya kukusudia) na kusahau na mambo wasioyaweza kuyafanya na mambo waliolazimishwa kuyafanya.”

 [1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/56 (184), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Ibn Maajah 2/390 (690), At-Ttirmidhiy 1/296 (162), Ddaaramy 1/305 (1229), Nnasaai 2/469 (611).

[2] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/251 (794), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Ibn Maajah 6/215 (2033).

Written by

Mwenyezi Mungu S.W.T. ameiwekea kila Salaa ya faridha wakati wake maalum, haijuzu kuisali kabla ya wakati wake au kuichelewesha baada ya wakati wake isipokuwa kwa sababu maalum. Kasema Mola Mtukufu katika Surat Nnisaai aya ya 103, “

﴿إنَّ الصَّلاةَ كاَنَت عَلىَ المُؤمِنِينَ كِتَـباً مَوقُوتاً.

 

Maana yake, “Kwa hakika Salaa kwa waislamu ni faridha iliyowekewa nyakati mahsusi.”

Written by

Inaruhusiwa kumzuia mtu asimkatishe Salaa yake, yaani kupita baina yake na baina ya sitra aliyoiweka au mahala anaposujudu. Kasema Abu Sa`id L-Khudryy R.A.A., “Kasema Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W., [1]

إن أَحَدُكُمْ إِذَا كَانَ  في صَلاة فَلا يَدَعْ أَحَدًا يَمُرُّ بَيْنَ يَدَيْهِ وَلْيَدْرَأْهُ مَا اسْتَطَاعَ فَإِنْ أَبَى فَلْيُقَاتِلْهُ فَإِنَّمَا هُوَ شَيْطَانٌ.

Maana yake, “Iwapo mmoja wenu yumo ndani ya Salaa asimuachie mtu kupita mbele yake, amsukume kadri awezavyo, akikataa basi amsukume kwa nguvu kwani huyo ni Shetani.”

 

 [1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/77 (243), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Abu Daawud 2/352 (598), Ibn Maajah 3/215 (944), Ddaaramy 1/384 (1411), Nnasaai 15/23 (4779), Bukhaari 2/321 (479), Muslim 3/73 (782).

Written by

Inaruhusiwa kufanya vitendo vya kujisalimisha nafsi yake, au ya mtu mwingine, au mali yake, au mali ya mtu mwingine kutokana na madhara ya aina yoyote yale. Mfano kumwokoa mtu anaye taka kuzama, au kipofu au mtoto anayetaka kutumbukia kisimani na kadhalika. Halafu akaendelea na Salaa yake mahala alipofika ili mradi awe hakugeuza uso wake kutoka kibla na wala hakuzungumza. Na iwapo atageuza uso wake au atazungumza basi Salaa yake itakuwa imeharibika, na itabidi aianze kuisali kutoka mwanzo.

Written by

Inaruhusiwa kuua nge au nyoka na kila kile kinachodhuru kwa harakati kidogo na halafu aendelee na Salaa yake mahali alipofika. Kasema Abu Huraira R.AA., “Kasema Mtume S.A.W., [1]

اقْتُلُوا الْأَسْوَدَيْنِ فِي الصَّلاةِ الْحَيَّةَ وَالْعَقْرَبَ.

Maana yake, “Viuweni viwili vyeusi katika Salaa; nyoka na nge.”

 [1] Abu Daawud 3/103 (786).

Written by

Ikiwa makohozi au mate hayo ni mengi basi anaruhusiwa anaesali kuyameza kama yatakuwa yanamshugulisha na Salaa. Pia inajuzu kuyatoa makohozi na makamasi kwa kutumia kitambaa wakati wa Salaa, ikiwa yata mshughulisha na Salaa yake au akayetema pembeni ikiwa anasali nje peke yake. Kasema Abu Sa`id L-Khudryy R.A..A., “Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. aliona makohozi kwenye ukuta wa Kibla akayakwangua halafu akawaelekea watu akasema,[1]

إِذَا كَانَ أَحَدُكُمْ يُصلِّي فَلاَ يَبْزُقْ قِبَلَ وَجْهِهِ فَإنَّ الله قِبَلَ وَجْهِهِ إِذَا صَلّى.

Maana yake, “Ikiwa mmoja wenu anasali basi asiteme mbele yake, kwani Mwenyezi Mungu yuko mbele yake wakati anaposali.” (makusudio kaelekea kibla kwa hivyo kamkusudia Mwenyezi Mungu Mtukufu kule aliko elekea).

 

 [1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/109 (261), mfano wa Hadithi hii imetolewa ya makatazo ya kutema mbele na Abu Daawud 2/70 (404), Muslim 3/163 (853). Bukhaari 2/360 (500).

Written by

Anaruhusiwa mtu kufanya kitendo kidogo hafifu kilicho nje ya Salaa kwa manufaa ya Salaa. Mfano kuondoa uchafu mahala anapo sujudia.  Kasema Muaqib, “Mtume S.A.W. alimuambia mtu mmoja aliyekuwa akiweka sawa sehemu anayo sujudia naye yuko katika Salaa, [1]

إِنْ كُنْتَ فَاعِلا فَوَاحِدَةً.

Maana yake, “Ikiwa huna budi kufanya basi fanya mara moja”.

 [1] Bukhaari 4/406 (1131), Muslim 3/160 (851).

Written by

Inaruhusiwa kwa anayesali kulia kwa ajili ya khofu ya akhera, lakini bila ya kujiliza au kukusudia. Hadithi iliyo hadithiwa na Mutrafiin kasema,[1] “  

أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يُصَلِّي وَلِجَوْفِهِ أَزِيزٌ كَأَزِيزِ الْمِرْجَلِ يَعْنِي يَبْكِي.

Maana yake, “Nimemkuta Mtume S.A.W. nae anasali na ndani ya kifua chake kuna mvumo kwa ajili ya kulia kama mfano wa mvumo wa sufuria linalochemka yaani alikuwa akilia.” Lakini ikiwa mtu atajiliza au atajilazimisha alie basi Salaa yake inaharibika, kwani kulia katika Salaa sio katika kitendo cha Salaa.

 [1] Nnasaai 4/457 (1199).

Written by

Ikiwa Imam atakuwa amesahau kitu katika vitendo vya Salaa basi inaruhusiwa kumkumbusha kwa kusema, “SUBHAANA ALLAH.”  Kasema Sahl Bin Said kasema, “Kasema Mtume S.A.W., [1]

مَنْ نَابَهُ شَيْءٌ فِي صَلاتِهِ فَلْيَقُلْ سُبْحَانَ اللَّهِ.

Maana yake, “Atakayekumbusha chochote katika Salaa aseme “SUBHAANA ALLAH.”. Na anayeruhusiwa kukumbusha kwa kusema “SUBHAANA ALLAH.” ni mwanamume, na ikiwa ni mwanamke ndiye anayetaka kukumbusha basi atapiga makofi. Kasema Sahl bin Said kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[2]

إِنَّمَا التَّصْفِيحُ لِلنِّسَاءِ وَالتَّسْبِيحُ لِلرِّجَالِ.

Maana yake, “Na kupiga makofi ni kwa wanawake na Tasbih (yaani kusema Subhaana Allah) ni kwa wanaume.” 

 [1] Ahmad 46/284 (21736), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Abu Daawud 3/126 (805), Nnasaai 16/265 (5318), Bukhaari 4/425 (1142),

[2] Ahmad 46/284 (21736).

Page 1 of 12
FaLang translation system by Faboba