Tohara

﴿وَلَقَد كَرَّمنَا بَنِيْ ءآدَمَ وَحَمَلـنَاهُمْ فِى البَرِّ وَالبَحرِ وَرَزَقنَـاهُم مِنَ الطَّيِّبَـتِ وَفَضَّلنـاهُم عَلَى كَثِيرٍ مِّمَّن خَلَقنَا تَفضِيلاً

 

"Na hakika sisi tumemtukuza binaadamu na tumewapa vya kupanda katika ardhi (barani) na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri na tumewatukuza kuliko wengi tuliowaumba kwa utukufu ulio mkubwa kabisa."

 


BAADHI YA MANENO MUHIMU YANAYOTUMIKA KISHERIA.

Yafuatayo ni baadhi ya maneno yanayotumika kisheria kutambulisha baadhi ya matokeo na vitendo:

1. Najasa au Khub`th: Ni uchafu ule ambao unao onekana na unaoharibu tohara ambao unaweza kumpata mtu, au kitu au nguo au pahala. Ukumbusho muhimu: Sio kila uchafu ni najasa. Tutaelezea InshaAllah kwa ufafanuzi baadae tutakapofika sehemu yake.

2. Hadath: Ni tokea linatokana na mtu mwenyewe, ambalo linasababisha kuharibu tohara yake, na kumzuia kufanya baadhi ya ibada ambazo zinahitajia tohara kamili kama vile Salaa, au Tawafu na kadhalika. Na hadathi zimegawanyika katika sehemu mbili:

(2.1) Hadath ndogo: Ni tokeo ambalo humsababishia mtu kuharibika udhu wake, na husababishwa na kutokwa na haja ndogo, au kubwa, au upepo kupitia njia ya haja kubwa, au kutokwa na Madhi au Wadii, au kwa kukamata najasa. Na mtu anajitoharisha kwa kujitia udhu.

(2.2) Hadath kubwa: Ni tokeo ambalo likimtokezea mtu anahitajiakujitoharisha kwa josho kubwa, na husababishwa na kutokwa na manii, au kuwa katika hali ya hedhi, au nifasi, au kugusana tupu mbili na kadhalika.

3. Tohara: Kilugha inamaanisha ni usafi, na kisheria ni kuondoa kila aina ya najasa inayotakikana kuondolewa ili kumtoharisha mtu, nguo au pahala.

4. Tohara ndogo: Kuosha kwa kutumia maji nadhifu viungo mahsusi, kwa taratibu na sifa maalum kama alivyo amrisha Mola Mtukufu katika Surat Al-Maida aya ya 6, “.

﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلاةِ فاغْسِلُواْ وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُواْ بِرُؤُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَينِ.

Maana yake, “Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Salaa basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake (maji) vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni.”.

5. Tohara kubwa: Ni kuoga josho kubwa kwa nia ya kujitoharisha na janaba, au hedhi, au nifasi. Kama alivyo amrisha Mola Mtukufu katika Surat Al-Maida aya ya 6, “.

﴿وَإِن كُنتُمْ جُنُباً فَاطَّهَّرُواْ.

Maana yake, “Na mkiwa na janaba basi ogeni”.

 

FaLang translation system by Faboba