Ibadhi.com

TANBIHI na Mukhtasari wake

TANBIHI na Mukhtasari wa haya ni kwamba:

Zinasema nukulu hizo kwamba: Muslim bin Abi Karima kapokea kutoka kwa Ali, lakini ikiwa wanakusudia kupokea huko ni kupokea riwaya kwa njia ya moja kwa moja kwa kusikia kutoka kwake, basi hilo halipo kwa Abu Ubayda Muslim bin Abi Karima Imamu huyu wa Kiibadhi, kwasababu kazaliwa baada ya kufariki Imamu Ali kwa kitambo, bali hata Sheikh wake ambae ni Abu Sha'athaa Jabir bin Zayd kapokea kutoka kwa Ali kwa njia ya BALAGH . Ama ikiwa wanakusidia kwamba kapokea kutoka kwa Ali Riwaya kwa njia isiokuwa hiyo, basi lililosahihi ni lile alilosema AlBukhari kwamba :  ((مسلم بن أبي كريمة ، يذكر عن علي))Muslim bin Abi Karima anatajakutoka kwa Ali na wala hakusema AlBukhari kwamba ((مسلم بن أبي كريمة روى عن علي)) Muslim bin Abi Karima kapokea kutoka kwa Ali. Ama aliyotaja kutoka kwa Ali bin Abi Talib ni Riwaya (no. 412) kama ilivyo katika Musnad riwaya isemayo:

أبو عبيدة قال: سئل علي بن أبي طالب بأي شيء بعثك رسول الله صلى الله عليه وسلم إلى أبي بكر في حجة عام تسع؟ قال بأربع خصال: ألا يطوف بالبيت عريانا , ولا تدخل الجنة إلا نفس مؤمنة , ولا يجتمع مسلم ومشرك في الحرم بعد عامهم هذا  ومن كان له عند النبي صلى الله عايه وسلم  عهد فالى عهده ومن لم يكن له عهد فالى أربعة أشهر

Kwahivyo maneno ya Al-Bukhari aliposema katika "At-Taarikh Al-Kabiir" (J. 7 UK. 271 No. 1144) kwamba "Muslim bin Abi Karima anataja kutoka kwa Ali" kasema kweli, na wala hakuna Muslim bin Abi Karima (Abu Ubayda) hata mmoja alotaja kutoka kwa Ali zaidi ya huyu Ibadhi ambae yamethibiti katika Musnad masimulizi yake kutoka kwa Ali kama aliyoyasema AlBukhari kwamba anataja kutoka kwa Ali. Vyenginevyo tuleteeni mwengine asiekuwa huyu Ibadhi mwenye kutaja riwaya kutoka kwa Ali ili awe AlBukhari hakumkusudia huyu.   


- ((فصار الذكر هو الرسول، وهذا ما لم يدفع، فصار أهل البيت عليهم السلام المأمور المخلق بسؤالهم، ولم يكلفوا أن يسألوا عبدالله بن يزيد البغداذي ولا عبدالرحمن بن خليل ولا عبدالكريم بن نعيم، ولا مسلم بن أبي كريمة، ولا عبدالصمد ولا المعلم ولا نجدة بن عامر ولا أبا مؤرج السدوسي))

 - Kufikiwa. Yaani imemfikia kutoka kwa Ali bin Abi Talib kadha wa kdha…


Na katika kauli ya Ibnu Hajar katika "Al-Lisaan" wakati akiyafasiri maneno ya Ibnu Hibban ya kukataa kwake kumtolea hoja Abu Ubayda kwasababu ya madhehbu yake, ambapo alisema Ibnu Hajar, hiyo ni kwasababu alikuwa Shia, hapana shaka kwamba hii ni kauli isio  na mwelekeo wowote si wa karibu wala wa mbali, kumuhisabu Abu Ubayda kwamba alikuwa Shia, bali maneno ya Al-Naasir shia wa Zaydiya yanaonesha kwamba Abu Ubayda Muslim bin Abi Karima ambae kamtaja sio Shia, hasa ukizingatia kwamba Al-Naasir huyo kamtaja vile vile katika msururu huo Maibadhi wengine kama vile Abdallah bin Yazid Al-Baghdadiy ambae ni mmoja kati ya wanafunzi wa Imamu Al-Rabi'u bin Habib, na akamtaja Abu Mu-urij Al-Saduusiy nae vile vile ni katika wanafunzi wa Imamu Abu Ubayda Muslim, hivyo basi kwa mkushanyiko huu baina yao inaonesha wazi kwamba Muslim bin Abi Karima ambae kamtaja huyu Al-Naasir Sheikh wa Zaydiya kwamba alikuwa ni Imamu wa Kiibadhi, changanya hilo pamoja na ukweli kwamba huyu Al-Naasir kamzingatia Abu Ubayda kwamba ni mmoja wa Maulamaa ambao wanamrejea, hii ukiachilia mbali maneno ya Al-Jaahidh  kuhusu Abu Ubayda   Muslim bin Abi Karima kwamba ni katika Maulamaa wa Kiibadhi na ni katika wapokezi wao.

Ama Ibnu Hibban kusema kwamba hamtolei hoja kwasababu ya udhalili wa madhehebu yake, hiki si kitu cha ajabu kwake na kwa walio mfano wake kuhusu madhehebu hii ya Kiibadhi na watu wake, na wala hili hakulianza yeye Ibnu Hibban, kwa vyovyote vile hili halizingatiwi katika uwanja wa elimu, na la ajabu zaidi ni kuwa Ibnu Hibban anawafanya kuwa ni hoja Rijaalu Al-Bukhari na Muslim, na lililomaarufu ni kwamba Bukharin a Muslim wamepokea kutoka kwa Mashia (Rawafidh) na Muutazila na Qadiriya na hao walioitwa kuwa ni Makhawarij, na wamewafanya kuwa ni hoja, basi vipi asifanywe hoja Imamu wa Kiibadhi kwasababu ya Uibadhi wake??!! Na tusalim amri kwa ajili ya mjadala na tukubali kwamba Imamu huyo wa Kiibadhi alikuwa ni mtu wa bidaa, sasa kasikia wapi Ibnu Hibban kwamba riwaya ya yule aonekanae kwamba ana bidaa inakataliwa kwasababu ya ubidaa wa mpokezi huyo??!! Kilichomaarufu ni kwamba mtu anaposhutumiwa ubidaa basi riwaya zake hurudishwa iwapo atapokea chenye kuunga mkono misimamo yake ambayo inaonekana kuwa ni ya ubidaa. Kwahivyo utaona wazi kwamba TA'ASSUB za kimadhehebu ndizo zilizowapoteza watu hadi wakaacha misingi hatimae kutokujuwa walisemalo.

Na lakushangaza zaidi baada ya kudai huyu Ibnu Hibban kwamba hamfanyi Abu Ubayda kuwa ni hoja, tunamkuta kamtaja katika kitabu chake "Al-Thiqaat" basi kwanini hakumtaja katika "Al-Majruuhiin" kwahivyo ni wazi kwamba anajuwa fika kwamba Abu Ubayda Muslim bin Abi Karima ni Thiqa mcha Mungu na ni hoja,  lakini hamfanyi hoja kwasababu ni Ibadhi. Allah aulani ujinga (قاتل الله الجهل ما أقبحه)

Ama kuhusu kauli ya Abu Hatim aliposema kuhusu Abu Ubayda Muslim bin Abi Karima kwamba hajulikani (MAJHUUL) na akafatiwa kwa kauli hiyo na Adh-Dhahabiy katika "Al-Miizan", basi hilo litazingatiwa kuwa ni ukosefu wao wa maarifa kuhusu Abu Ubayda, na kwahivyo kutokumjua kwao hakumdhuru kitu madamu kuna wengine wanamjua, na hapana shaka kwamba hili ni jambo linalokubalika kimaumbile kabla ya kifani za kielimu, kwani hakuna ulazima kwa yule ambae atamjuwa Ibnu Ma'iin kwa mfano kwamba na Adh-Dahahabiy au Abu Hatim na wao lazima wamjue, ulazima huu haupo, vyenginevyo itabidi muwakatae enyi Mawahabi wale wapokezi ambao kasema Al-Albaniy kuwa hakuna Tarjama zao au hawajui au hawakutajwa kabisa, na hali ya kuwa wametajwa na Tarjama zao zipo na wanajulikana, sasa je itangulizwe kauli ya huyu aliekosa maarifa ya kuwajuwa watu hao au wale waliowataja na kuwatarjama? Bila shaka kila mtu mwenye insafu atafahamu na kukubaliana nami kwamba kauli ya kutangulizwa na kuzingatiwa ni ya yule aliyemtaja mpokezi na akamuelezea hali yake sio ya yule aliyesema kwamba hamjui.

Lakini haitakuwa vibaya nikikunukulia kwa mukhtasari hapa kuhusu maudhui hii yenye kuthibitisha kwamba ukosefu wa maarifa kwa baadhi ya wapokezi hauzingatiwi kwavile wako waliowajua wapokezi hao na kuwatarjama. Anasema:

1)    Anasema Al-Albaniy kuhuhu Sulaiman bin Shurahbil kwamba: “Na Sulaiman bin Shurahbil…..sikukuta katika tabaka hii mwenye jina Sulaiman bin Shurahbil”. Anasema Al-Qannubi: “Hivyo ndivyo alivyosema, wakati Sulaiman huyu jina lake kamili ni Sulaiman bin Abdil-Rahman bin ‘Issa bin Maimun bin Bint Shurahbil, na hufupishwa (jina lake) wakati mwengine kama ulivyoona (Sulaiman bin Shurahbil). Naye kaelezewa (katika vitabu tafauti vya wapokezi, kama ilivyo hapo chini)”.


[9] - Al-Albani Al-Dhaifa j. 4, uk. 200.  

[10] - Kaelezewa katika Rijalu Al-Bukhari cha Al-Kalaabaadhi j. 1, uk. 314; Al-Taarikh Al-Kabir j. 4, uk. 24; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim j. 4, uk. 29 na pia katika kitabu chake Al-’Ilal; Sualatu Al-Ajurri cha Abi Dawud; Al-Dhu’afaa cha Abu Zur’a Al-Dimashqi; Al-Ma’arifa cha Al-Fasawi; Tahdhibu Al-Kamal j. 8, uk. 79 chapa ya Darul Fikr; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 4, uk. 181; Al-Kashif j. 1, uk. 462; Taarikhul Islam; Siyaru Al-A’alam j. 11, uk. 136; Al-Mizan j. 2, uk. 212; Tadhkiratul Huffadh j. 2, uk. 438; Al-’Ibar vya Al-Dhahabi j.1, uk. 413, Al-Bidaya Wa Al-Nihaya j. 10, uk. 312; Al-Taqrib na. 2588; Khulasat Al-Tahdhib cha Al-Khazraji; Shadharat  Al-Dhahab j. 2, uk. 78; Al-Jami’u Fii Al-Jarhi Wa Al-Ta’adil j. 1, uk. 340; Al-Jam’u Baina Rijali Al-Sahihain j. 1, uk. 183; Hadyu Al-Sari uk. 408; Al-Thiqat cha Ibn Shahin. Naye (mpokezi huyo) ni mpokezi wa Al-Bukhari na (Maimamu) wanne (Abu Dau, Al-Tirmidhi, Al-Nasai na Ibn Maja).


1)    Anasema Al-Albaniy kuhusu Abdul-A’ala bin Abdillah bin Abi Far-wa kwamba:  “Naye ni majhul (hajulikani): sikumuona aliyemuelezea”. Anasema Al-Qannubi: “Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani) na hali haiko hivyo, kwani ‘Abdul-A’ala huyu kaelezewa katika vitabu vingi mno. Na Ibn Ma’in kasema: ‘Abdul-Hakim bin ‘Abdillah bin Abi Far-wa na Salih bin ‘Abdillah bin Abi Far-wa na Abdul-A’ala bin ‘Abdillah bin Abi Far-wa wote ni wenye kuaminika.’ Na mfano wa hayo kayasema Ya’aqub bin Abi Suf-yan, na akasema Al-Daraqutni: ‘Is-haq bin Abi Far-wa ni mwenye kuachwa; ana ndugu watatu ni wenye kuaminika”.

2)  Anasema Al-albaniy kuhusu Said bin Ash-wa’i kwamba sikuiona tarjama (biography) yake”. Hivyo ndivyo alivyosema kwa sababu yeye alitazama baadhi ya vitabu vya wapokezi asimkute Said bin Ash-wa’i, wala hakujua kwamba baba yake jina lake ni ‘Amru bin Ash-wa’i, na wengine wakamnasibisha na babu yake wakasema: ‘Said bin Ash-wa’i’.

3)  Anasema (Al-Albani) katika Sahiha yake: “….isipokuwa ‘Abbaad bin Salim sikumuona aliemtarajimu (aliyemtaja)”. Hivyo ndivyo alivyosema (Al-Albani), na lau alitazama: Al-Tarikh Al-Kabir cha Al-Bukhari; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan, basi angelijua kwamba (mpokezi huyo) ni mwenye kutarajimiwa.

Anasema Al-Albaniy kuhusu Abu Rifa’a, ‘Abdullahi bin Muhammad bin ‘Umar Al-’Adawi “Isnad hii wapokezi wake ni wenye kuaminika wenye kujulikana isipokuwa Abu Rifa’a sikumuona alipotarajimiwa”. Hivyo ndivyo alivyosema, wakati Abu Rifa’a huyu katarjimiwa katika Taarikh Baghdad cha Al-Khatib na akasema: “Ni mwenye kuaminika”.


[11] - Al-Albani Al-Dhaifa j. 1, uk. 213.  

[12] - Miongoni mwa hivyo ni: Al-Taarikh Al-Kabir cha Al-Bukhari j. 6, uk. 71; Taarikh Ibn Ma’in; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim j. 6, uk. 27; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan, j. 7, uk. 130; Al-Dhu’afaa cha Al-Daraqutni uk. 94; Al-Ma’arifa Wa Al-Taarikh cha Ya’aqub bin Sufyaan Al-Fasawi j. 3, uk. 55; Tabaqat Ibn Sa’ad; Tahdhibul Kamal cha Al-Mizzi j. 11, uk. 8-9, tarjama na. 3669 chapa Daru Al-Fikr; Tahdhibu Al-Tahdhib j. 6, uk. 87; Taqribu Al-Tahdhib uk. 331 na akasema Al-Hafidh kuhusu mpokezi huyo: “Ni mwenye kuaminika; Faqihi”; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil j. 2, uk. 47.

[1] - Al-Albani Ir-waau Al-Ghalil  j. 3, uk. 121.

[1] - Na hivi baadhi ya vitabu ambavyo vimetaja tarjama yake: Rijalu Al-Bukhari cha Al-Kalabadhi; Rijalu Muslim cha Ibn Manjuyah j. 1, uk. 247; Al-Ta’arikh Al-Kabir j. 2, uk. 500, Taarikh Ibn Ma’in; ‘Ilalu Al-Tirmidhi; Al-Jarhu wa Al-Ta’adil j. 4, uk. 50; Tabaqat Ibn Sa’ad j. 6, uk. 327; Al-Thiqat cha Ibn Hibbaan; Al-Thiqat cha Al-’Ijli; Tahdhibu Al-Kamal; Tahdhibu Al-Tahdhib; Mizanu Al-I’itidal; Al-Mughni Fii Al-Dhu’afai tarjama na. 2356; Al-Kashif j. 1, uk. 441; Taqribu Al-Tahdhib uk. 239; Khulasat Al-Tahdhib; Al-Jami’u Fii Al-Jarhu wa Al-Ta’adil j. 1, uk. 305; Al-Jam’u baina Rijali Al-Sahihain j. 1, uk. 116; Hadyu Al-Sari uk. 406.

[1] - J. 3, uk. 191.

[1] - J. 6, uk. 38.

[1] - J. 6, uk. 80.

[1] - J. 7, uk. 159

[1] - Al-Albani Sahiha j. 5, uk. 368.


1)    Anasema Al-Albaniy kuhusu Al-Harith bin Muhammad Al-Makfuf kwamba: “Sikuona tarjama (biography) yake”. Hivyo ndivyo alivyosema, na imempita (Al-Albani) kwamba Al-Harith huyu katarjamiwa katika Al-Mizan, na Lisanu Al-Mizan.

2)  Anasema Al-Albaniy kuhusu Ummu Yunus bint ‘Ubaid kwamba: “Katika sanad kufikia kwake kuna Ummu Yunus bint ‘Ubaid, wala hakutajwa katika vitabu vya Tarajim (biographies)”. Hivyo ndivyo alivyosema, ilhali Ummu Yunus huyu katajwa katika Al-Taarikh Al-Kabir, Al-Munfaridat cha Al-Imamu Muslim; Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim.

3)  Anasema Al-Albaniy kuhusu Ummara katika Sahiha yake: “Na ‘Ummara sikumjua (ni nani)”.  Hivyo ndivyo alivyosema, ilhali ‘Ummara huyu ni maarufu. Na akasema kuhusu Amru bin Abi Amri Al-’Abdi kwamba: “Na ‘Amru bin Abi ‘Amri Al-’Abdi sikumjua (ni nani).” Hivyo ndivyo alivyosema, ilhali ‘Amru huyu ni maarufu katarajumiwa katika vitabu vingi. Naye (mpokezi huyu) ni katika wapokezi wa Al-Bukhari na Muslim; na Al-’Abdi ni kunasibishwa na maula (bwana) wake Al-Muttalib bin ‘Abdillah Al-Makhzumi. 

4)  Anasema al-Albaniy kuhusu Abu Salih Al-Khawlani “Na sikumjua”. Hivyo ndivyo alivyosema, wala hakujua kwamba Al-Khawlani huyu ni mwenye kutarajimiwa katika Al-Jarhu Wa Al-Ta’adil cha Ibn Abi Hatim na akanukuu kutoka kwa baba yake akisema “Hana ubaya”.

5)  Anasema Al-Albaniy kuhusu Al-Mu’alla bin Ru-ba “Na Al-Mu’alla bin Ru-ba sikuiona tarjama yake”. Hivyo ndivyo alivyosema, wala hakujua kwamba Al-Mu’alla bin Ru-ba huyu anayo tarjama katika Al-Ma’arifa Wa Al-Taarikh cha Ya’aqub bin Sufyaan Al-Fasawi.

6)  Anasema Al-Albaniy kuhusu Al-Nadharu bin Muhammad Al-Shaibani “Na Sheikh wake Al-Nadharu bin Muhammad Al-Shaibani sikumjua. Hivyo ndivyo alivyosema, na Al-Nadhar bin Muhammad ni mashuhuri katarajimiwa katika vitabu vingi mno.

12) Anasema Al-Albaniy kuhusu Imra-atu Ibni Umar katika Sahiha yake: “Na wapokezi wake ni wenye kuaminika isipokuwa  Imra’atu Ibni Umar (mke wa Ibn ‘Umar) sikumjua”. Na Imra-atu Ibni Umar (mke wa Ibn Umar) huyu ni maarufu mashuhuri, na jina lake ni Safiyya bint Abi Ubaid Al-Thaqafiyya. Al-Imamu Muslim na Al-Imamu Al-Bukhari wamepokea (riwaya zake) katika Al-Ta’aaliq. Na hivi ni vitabu vilivyomtarajimu:

13) Anasema Al-Albaniy kuhusu Isa bin Umar katika maelezo yake juu ya Al-Mishkaa kuhusu Isa bin Umar: “Hajulikani”. Lakini kauli ya Al-Daraqutni “Ni mtu wa madina anajulikana”

Kwahaya machache katika mengi kuhusu haya ya Al-Albaniy na waliomfano wake, inakubainikia wazi ewe ndugu msomaji mpendwa, ukweli wa tuliotangulia kuusema kwamba, kutokujulikana kwa baadhi ya wapokezi na baadhi ya Maulamaa hilo halidhurushi kitu madamu kuna wengine wamewataja wapokezi hao, kwahivyo kauli ya Al-Albaniy waliyoghururika nayo Mawahabi akiwemo Saad Aal Humayd alipodai kwamba Abu Ubaida hakutajwa na kwamba ni majhuul si jambo la kupigiwa kofi lau wangalijua wasiojua, kwani uhakika wa Abu Ubaida kwa Al-Albaniy ni sawa na uhakika wa Isa bin Umar na Imra-atu Ibni Umar na Al-Nadharu bin Muhammad Al-Shaibani na Ummara na Amru bin Abi Amri Al-Abdi na Abu Salih Al-Khawlani na Al-Mu’alla bin Ru-ba na Sulaiman bin Shurahbil na Abdul-A’ala bin Abdillah bin Abi Far-wa na Said bin Ash-wa’i na Abbaad bin Salim na Abu Rifa’a, Abdullahi bin Muhammad bin Umar Al-’Adawi na Al-Harith bin Muhammad Al-Makfuf na Ummu Yunus bint Ubaid, ambapo wote hao Al-Albaniy kadai kuwa hawajulikani au hawajui. Je kutokuwajuwa kwake hao ni uhakika wenye kuzingatiwa? Hapana shaka kwamba kila msomaji mwenye kutafuta haki na akawa na Insafu anaona kwamba huko kumetokana na kasoro zake mwenyewe Al-Albani ya kutokuwajua hao kama ulivyoona kwamba hao wametajwa katika vitabu mama na kutarajimiwa ambapo yeyey anasema hajawaona wala hawajui, kwahivyo hatuoni ajabu wala hatushangai kumuona Al-Albani hamjui Abu Ubayda au Imamu Al-Rabi'u bin Habib vile vile. Kama ambavyo inawezekana kweli kwamba Abu Hatim na Adh-Dhahabiy hawakumjua Abu Ubayda Muslim bin Abi Karima ni nani, lakini kutokumjua kwao hakumdhuru kitu madamu kuna wengine wanamjua, na kwahivyo tunatosheka na kauli ya Ibnu Ma'iin kuhusu kumtaja kwake Abu Ubayda na akasema kwamba: ((لا باس به)) "Hana matatizo" na kwahakika wameafikiana Maulamaa wa Mustalahu Al-Hadiith na Jarhu wa Ta'adiil, kwamba kauli ya Ibnu Ma'iin anaposema ((لا بأس به)) "Hana matatizo" ni sawa na kusema kwake kwamba ni Thiqa. Kwahivyo tunamwambia kila Wahabi mwenye kushuku kuwepo kwa Imamu Abu Ubayda kwamba:

إذا لم تستطع شيئا فدعه *** وجاوزه إلى ما تستطيع

Kama huna uliwezalo basi wacha**Fanya uliwezalo

Naam, kama huna ukiwezacho usijikakamue tafuta jengine uliwezalo ufanye. Ndugu yangu mpendwa msomaji wa makala hii fupi, anasema Sheikh huyu wa Kiwahabi Saad Aal Humayd aliyejitokeza kukanusha kuwepo kwa Imamu Al-Rabiu bin Habib na Abu Ubayda Muslim bin Abi Karima, dhahiri ni kwamba alifanya hivyo kwa kughururika na maneno ya Al-Albaniy, alipodai kuwa hawakutajwa hawa na yoyote wala hawana tarjama, tunamwambia Saad Aal Humayd alodanganyika na maneno ya Al-Albani kwamba:

من جعل الغراب دليلا , يمر به على جيف الكلاب

((Mwenye kumfanya kunguru kuwa ni muongozaji njia, basi atampitisha kwenye mizoga ya mbwa))

وللحديث بقية

والسلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment