Ibadhi.com

LEO KATIKA FUNGA-6

LEO KATIKA FUNGA

Allah  ﷻ Anasema:
 
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}

Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. (2:183)

LEO TENA KWA UWEZO WAKE ALLAH MTUKUFU TUNAENDELEA NA DARSA YETU YA FUNGA, TUKIWA KATIKA MUENDELEZO KUTAFUTA HEKIMA YA KUJA AYA ZA DUAA BAINA YA AYA ZA FUNGA KAMA TULIVYO ELEZA KATIKA DARSA ZA NYUMA.
 فلماذا جاءت بين الآيتين آية الدعاء؟
 
BASI KWANINI NA IPI HEKMA YA KUJA BAINA YA AYA MBILI IKAJA AYA YA DUAA?
 ولهذه الآية قصَّة لا بأس من ذكرها.
 
KWA AYA HII, KUNA KISA AMBACHO HAPANA UBAYA TUKITAJE AU TUKIELEZEE
 عندما جاء أعرابي إلى رسول الله - صلَّى الله عليه وسلَّم - يسأله: يا محمَّد، أقريبٌ ربُّنا فنُناجيه أم بعيدٌ فنُناديه؟
 
WAKATI ALIPOKUJA BEDUI KWA RASULI (ﷺ) AKAMUULIZA: EWE MUHAMMAD, JE MOLA WETU YUPO KARIBU ILI TUMUOMBE KWA SAUTI YA CHINI, AU YUPO MBALI ILI TUPAZE SAUTI ZETU KWA KUMUOMBA?
LAKINI KABLA MTUME (ﷺ) HAJATOA JAWABU. JIBRILU AKATEREMKA NA AYA HII IFUATAYO.
 
 ﴿ وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ ﴾
Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka.  [البقرة: 186]
 
ولنا في هذه الآية وقْفة: لماذا اختلفتْ هذه الآية بالذَّات عن جَميع آيات السُّؤال الموجَّهة إلى رسول الله - صلَّى الله عليه وسلَّم - في القرآن؟
 
KABLA HATUJASONGA MBELE. KWANZA TUSIMAME KATIKA AYA HII.
 
KWANINI AYA HII IMEKUA TOFAUTI NA AYA ZINGINE ZOOTE KWA DHATI, AYA  AMBAZO ZILIKUJA KWA MASWALI YALIYOKUWA YAKIELEKEZWA KWA MTUME (ﷺ) NDANI YA QUR'ANI?
 أيّ سؤال وجِّه إلى النبي - صلَّى الله عليه وسلَّم - في القرآن جاءت الإجابة: قل.

SUALI LOLOTE LILILO ELEKEZWA KWA MTUME (ﷺ) NDANI YA QUR'ANI, BASI JAWABU LILIKUJA KWA KUTUMIA NENO: SEMA UWAAMBIE (YANI QUL)
 
MFANO:
{يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ﴿ 
Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. SEMA: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa. [البقرة: 217]
 
﴿ يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَا أَكْبَرُ مِنْ نَفْعِهِمَا وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنْفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ ﴾
Wanakuuliza juu ya ulevi na kamari. SEMA: Katika hivyo zipo dhambi kubwa na manufaa kwa watu. Lakini dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake.
[البقرة: 219]
 
 يَسْأَلُونَكَ عَنِ الأَهِلَّةِ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ ﴿ 
Wanakuuliza khabarai ya miezi. SEMA: Hiyo ni vipimo vya nyakati kwa ajili ya watu na Hija. [البقرة: 189]
 
  وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْجِبَالِ فَقُلْ يَنْسِفُهَا رَبِّي نَسْفًا ﴿
Na wanakuuliza khabari za milima. WAAMBIYE: Mola wangu Mlezi ataivuruga vuruga.  [طه: 105]
 
 وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي ﴿
Na wanakuuliza khabari za Roho. SEMA: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi.   [الإسراء: 85]
 
HIZI NI BAADHI YA AYA AMBAZO MTUME (ﷺ) KILA ALIPOKUA AKIULIZWA SWALI, BASI ALLAH MTUKUFU ALIMPA MAJIBU KWA KUTUMIA NENO SEMA UWAAMBIE  (YANI QUL)

ZIPO AYA ZINGINE NYINGI MFANO WA HIZO AMBAZO HATUWEZI KUZILETA ZOTE KWA WAKATI MMOJA, BALI TUMECHUKUWA CHACHE TU ILI KUWEKA MFANO WA WAZI.
CHA KUJIULIZA, KWANINI AYA YA DUAA IMEUPUKANA NA NENO (QUL) YANI SEMA PALE MTUME (ﷺ) ALIPO ULIZWA SWALI?
I
N SHA ALLAH TUWE PAMOJA KATIKA DARSA YETU SEHEMU YA SABA.

ALLAH MTUKUFU: TWAKUAOMBA UZIKUBALI FUNGA ZETU NA QIYAMU ZETU, PIA NA BAKI YA IBADA ZETU.
Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment