Ibadhi.com

06. UIMAMU WA KUJITETEA – DIFAAI


UIMAMU WA KUJITETEA –DIFAAI


MJUKUU: Ajabu iliyoje!, Ajabu iliyoje!,  ((Na katika watu yupo ambaye huiuza nafsi yake kwa kutaka radhi za Allah mtukufu; na Allah mtukufu ni Mpole kwa waja wake.)) Baqarah:207, Zimebakia aina mbili za Uimam, nina hamu sana ya kuzijua, niambie yanayohusiana na aina hizo ewe babu yangu.
BABU: Kwa hivyo unafuatilia vizuri ewe mjukuu wangu, basi endelea kujitahidi… Allah mtukufu akubariki.
Aina ya tatu: Ni Uimam wa Difai – Kujiitetea-, “Kikawaida Uimam huu hutokea baina ya Uimam wa siri na dhahiri, wanapokuwa maibadhi wapo katika uimam wa siri na wakakvamiwa na maadui hapo hutangaza hali ya kujitetea, na kujitetea ni katika mambo ya lazima kwa Maibadhi unapokosekana Uimam wa Dhahiri, watamchagua mmoja katika masheikh wao, mjuzi wa mambo ya vita, maarufu kwa ushujaa, ili awaongoze katika mapigano dhidi ya maadui, watamwita Imam wa Difai, mapigano yakimalizika na uimam wake utakuwa umemalizika”
MJUKUU: Hakika mimi nashangazwa na hikma iliyojaa katika fikra ya kisiasa ya Maibadhi, njia yao hii iliwezesha kubaki kwao karne nyingi.
BABU: Usifanye haraka ewe mjukuu wangu, imebakia aina ya mwisho ya uimamu nayo ndiyo aina muhimu zaidi, bali hilo ndio lengo wanaloliendea maibadhi zama zote za historia yao, nao ni UIMAM WA DHUHUR – Dhahiri – “ Maibadhi wanapofikia idadi yao nusu ya maadui kinguvu, mali na elimu, au muda wowote watakaoweza kumshinda adui yao  na kuwa juu yao, itakuwa imewawajibikia kusimamisha Uimamu wa dhahiri na kumchagua Imamu muadilifu, na kama hawakufanya watakuwa kama walioua dini ya Allah mtukufu, na wao Maibadhi  bila shaka wako mbali  na kuiua Itikadi ya kiislamu, ambayo wamepambana muda mrefu, na wamepigana katika njia ya kuihifadhi ibaki safi na iliyosalimika, kwa mujibu wa mafundisho ya Qur-an tukufu na Sunnah sahihi ya Mtume –Sallallahu alayhi wasallam-.
MJUKUU: Nizidishie ewe babu yangu, bado nina hamu ya kusikia mengi kuhusu fikra ya kisiasa kwa Maibadhi.
BABU: Haya yanakutosha ewe mwanangu, leo mazungumzo yamerefuka, kama unataka ziyada rejea katika maktaba ya kiibadhi, usome vitabu vifuatavyo:
1.    Alwuheibi, Musallam bin Salim: Alfikr al-aqadiyy indal ibadhiyyah hattaa nihaayatil qarni thanil hijry, chapa ya mwanzo, Maktabat Dhaamiri, Siib, 1427h/2006.
2.    Taalib, Mahdiyyu Haashim: Alharakatul Ibaadhiyyah fil Mashriqil Arabiyyi, chapa ya pili, Daarul hikmat, London 2003m.
3.    Muammar, Ally bin Yahya: Al-ibadhiyyah bainal firaqil Islaamiyyah inda kuttaabil maqaalaat fil qadiimi walhadiithi, jz 2, wizaaratu turaathil qawmiy wathaqaafah, Usultan wa Oman, 1406h/1986m.

Ndio nini “Azzaaba” ….. Njoo pamoja name makala ifuatayo:


By: Khamis Yahya Khamis Alghammawi Abu Muslim

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment