Ibadhi.com

05. UIMAM WA SHARAA (KUMUUZIA NAFSI ALLAH MTUKUFU)

UIMAM WA SHARAA (KUMUUZIA NAFSI ALLAH MTUKUFU)


MJUKUU: Ewe babu yangu hakika hii ni dalili ya usawa wa fikra ya kisiasa kwa Maibadhi; kwa kuwa wanazingatia hali inayowazunguka na hujiweka kwa namna itakavyowawezesha kueneza daawa yao na kuipa nguvu katika nafsi, ili waweze baada ya hayo kufikia marhala nyingine ya Dhuhuur.
BABU: Ahsante ewe mwanangu, mambo ni kama ulivyotaja, lakini ipo namna nyingine ya Uimam kabla ya kufikia marhala ya Dhuhuur nayo ni marhala ya “Uimam wa Sharaa”; uimam ambao kikawaida husimamishwa wakati wa kitmaan, pale ambapo baadhi ya wapiganaji, wanaume, waliobaleghe, wasiopungua arobaini huchagua kumuuzia Allah mtukufu  nafsi zao, basi wao hutoka dhidi ya hukmu za madhalimu, lakini wao huwa hawamlazimishi yoyote kujiunga nao, wajibu wao ni kutowatisha watu katika waislamu, wala wasiwapige vita mpaka wao wawapige vita. Hili ni jambo la kujitolea hakuna kulazimishwa na yoyote. Na wakichagua njia hii baadhi ya Maibadhi basi watachagua baina yao Imam, ataitwa “IMAAM SHURAA”, utawala wake utakuwa juu ya kundi hilo tu maadam wapo katika marhala hii, atawaongoza katika vita na kuyapanga mambo yao, watampa kiapo cha utiifu cha kupigana jihad na maadui kwa kutetea nafsi  na dini mpaka mauti au kupata ushindi. Na namna ya kuweka kiapo cha utiifu ni kama ifuatavyo:


Atatangulizwa mtu aliyechaguliwa kuwa Imam, hupewa mkono wa kulia kisha anaambiwa: “Hakika sisi tumekutanguliza uwe Imam juu ya nafsi zetu na waislamu, uhukumu kwa kitabu cha Allah mtukufu na Mtume wake –sallallahu alayh wasallam- utaamrisha mema, utakataza mabaya,  utaidhihirisha dini ya Allah mtukufu ambayo amewalazimisha waja wake kumuabudu, na utalingania katika dini na jihaad kwa kadri utakavyopata njia” Akisema: “Ndio” basi inakuwa kiapo chake kimewajibika, hapo atasimama mmoja mmoja katika kundi hilo nao watampa kiapo cha utiifu. Kisha Khatibu atatoa khutba baada ya hapo juu ya usahihi wa kiapo cha utiifu na kufungika kwake kisha atasema “ Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ispokuwa Allah mtukufu, hakuna hukmu ispokuwa ya Allah mtukufu, na hakuna hukmu kwa anayehukumu tofauti na alivyoteremsha Allaah mtukufu, na hakuna utiifu kwa mwenye kumuasi Allah mtukufu, Hakuna hukmu ispokuwa ya Allah mtukufu, kuuzuliwa na kufarikiana na maadui wa Allah mtukufu”


MJUKUU: kwa kuthibiti itikadi yao katika nafsi zao imekuwa rahisi kuzitoa muhanga nafsi zao katika njia ya Allah mtukufu kwa kuinusuru dini ya Allah mtukufu na kuisimamisha sharia yake.
BABU: Umesema kweli ewe mwanangu, Itikadi ikithibiti inakuwa rahisi kutoa muhanga kila kitu, kuzitoa nafsi katika njia ya Allah mtukufu ni moja ya muhanga mkubwa walioutoa maibadhi katika njia ya Allah mtukufu, na katika masharti ya Sharaa ni:
1.    “Haijuzu kwa Mashuraati – waliouza nafsi zao katika njia ya Allah mtukufu – kutumia Taqiyya ya kidini, vyovyote itakavyokuwa hali na matatizo, na kwa sababu yoyote itakayokuwa”
2.    “Haijuzu kwa atakayechagua njia hii kurudi nyumbani kwake ispokuwa kama kuna shida kubwa, na kukaa kwake kutabakia kwa muda, na katika hali hii yeye atazingatiwa ni mgeni pale na itamuwajibikia kusali kupunguza sala kama msafiri”
3.    “Haijuzu kwa watakaochagua njia hii kurudi nyuma na kuacha ispokuwa kama watakapofanikiwa kumshinda adui yao”
Je kuna masharti mengine, au kuna marhala nyingine…. Tukutane makala ijayo


By: Khamis Yahya Khamis Alghammawi (Abu Muslim)

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment