Ibadhi.com

04: KUMCHAGUA NA KUMUUZULU IMAM KWA IBADHI

NURU ING’AAYO KATIKA NJIA YA UADILIFU

 

KUMCHAGUA NA KUMUUZULU IMAM KWA IBADHI


MJUKUU: Allah mtukufu akukirimu ewe babu yangu na anyanyue cheo chako.. umenibainishia yaliyokuwa magumu kwangu, kwa hakika yote haya sikuwa nayajua. Nimejua kutoka kwako kuwa msingi wa Shura ni katika misingi ya hukmu ya kiibadhi, naomba unisifie ewe babu yangu njia ya kumchagua na kumuuzulu Imamu.
BABU: Umegusia jambo muhimu ewe mwanangu…!, “Hakika njia ya kumchagua Imamu Muadilifu inatimia kwa wanachuoni kumchagua na waislamu kumpa ahadi ya utiifu, Amma mtu anayechaguliwa kuwa Kiongozi inawajibika awe ametimiza baadhi ya masharti; zilizokuwa muhimu: Awe ni katika wenye elimu na uchamungu katika dini, kwa kuwa kitakiwacho Imam awe ni kiongozi wa ummah katika kila Nyanja ya maisha yake, na hakuna lililo muhimu katika jamii ya kiislam kama dini, na katika jambo la msingi kulikumbushia hapa ni kuwa Ibadhi haiweki sharti la Uquraishi katika uimam, kwani Uislamu haukuweka mizani ispokuwa ya uchamungu ((Hakika mtukufu zaidi baina yenu kwa Allah mtukufu Yule mchaji zaidi, Hakika Allah mtukufu ni Mjuzi mwenye khabari)).
Jua -ewe mwanangu- kuwa Imam Muadilifu si haki kumuuzulu ispokuwa katika mambo manane, muhimu katika hayo: KUFANYA DHAMBI KUBWA INAYOWAJIBISHA KUSIMAMISHIWA HADDI, hapo atavuliwa na kuwekwa Imamu mwingine amsimmishie Haddi ya kisheria, au ikiwa atafanya dhambi isiyowajibisha haddi kisheria hapo atatakiwa atubie, akitubia ataendelea kama hakutubia atakuwa amejivua utawala”
MJUKUU: Allah mtukufu aninufaishe kwa elimu yako ewe babu yangu… basi vipi kuhusu njia za kuisimamisha dini ambazo wanazifuata Maibadhi kufikia Ukhalifa ?
BABU: Nakuona ni mfuatiliaji na mwenye hamasa, umetanabahi na kufahamu, umejua na kuhifadhi, Allah mtukufu akubariki na adumishe jitihada yako.
“Njia za kusimamisha dini ((Masaalikuddin)) kwa maibadhi ndizo njia za kufikia kwazo kutekeleza hukmu za kisheria; Kwa kutazama uwajibu wa kumchagua kiongozi muadilifu kwa Maibadhi, na kwa vile Maibadhi wanatofautiana na wengine katika fikra hii na madhehebu zingine, na kwa vile daawa ya kiibadhi inapitia katika udhaifu na nguvu, basi wamekubaliana wanachuoni wa kiibadhi kuwa kuna namna nne za uimamu, kila aina moja inafaa kwa wakati maalumu, na aina hiyo inakuwa na masharti na wajibu maalumu yenye kuendana na marhala ambayo daawa ya kiibadhi inapitia, basi sikiliza ewe mwanangu ubainifu wa kila marhala…
AINA YA KWANZA: UIMAM WA SIRI ((KITMAAN))
Aina hii huwa pale maibadhi wanapokuwa hawana nguvu ya kutangaza uimamu, katika hali hii hulingania katika madhehebu yao kwa siri, na wanamchagua mmoja wao awe kiongozi wao na kikawaida huwa mwanachuoni na mchamungu, ili awe ndio msimamizi wa daawa, mpangaji na kusimamia mambo ya wafuasi wake, kama ambavyo atachagua walinganiaji watakaotumwa miji tofauti kueneza madhehebu huko, na ataitwa ((IMAM WA KITMAN)), Maimam Mashuhuri wa marhala hii katika historia ya kiibadhi ni Imam Jabir bin Zaid Al uzdi Muomani na Imam Abu Ubaidah Muslim bin Abi Karimah Altamimi – Allah mtukufu awaridhie- na kwa hakika maimam hawa wawili wana kazi kubwa walioifanya kuendeleza ulinganio wa kiibadhi na kuutangaza, kupitia karne mbili za mwanzo na karne ya pili za hijra.


MUONEKANO WA UENDELEZAJI UIMAM WA KITMAN KWA MAIBADHI.


Katika muonekano wa muendelezo uimam wa kitman ni kujuzu kutumia TAQIYYA ya kidini, ili waweze kuhifadhi itikadi yao, na kujiweka mbali mno na maadui na ujeuri wao, na Taqiyya ewe mwanangu kama anavyosema Imam wetu Alsalimi katika kitabu chake Bahjatul An-waar, na inaweza kuwa kwa Qauli au kwa vitendo: “Taqiyya ya vitendo haijuzu kwa Masahibu zetu ((Maibadhi)), nayo ni kama kuua nafsi au kuigharikisha, Amma Taqiyya ya Qauli inajuzu katika sehemu na inakataliwa sehemu nyingine, amma sehemu inapojuzu ni pale inapokuwa qauli hiyo haina madhara kwa yoyote katika viumbe na ikawa msemaji amelazimishwa kuisema qauli hiyo, hapo itamjuzia kuitetea nafsi yake kwa hiyo qauli hata kama ni neno la ushirikina kutokana na yale anayoyaogopea kama kuuwawa n.k., Kujuzu kwa hilo kumechukuliwa katika Quran na Sunnah, Amma Qur-an ni kwa Qauli yake Allah mtukufu {{ISPOKUWA ATAKAYELAZIMISHWA HALI MOYO WAKE UMETULIA KATIKA IMAN}} Alnahl:106 na kauli yake {{ Ispokuwa ikiwa kwa ajili ya kujilinda na shari zao.}} Al – Imran :21 na Amma sunnah, amesema Mtume sallallahu alayh wasallam- “Wamesamehewa ummah wangu kukosea kwa bahati mbaya, kusahahu, yanayoelezwa na nafsi zao, na yale waliyolazimishwa” na katika hayo ni yale yaliyomtokea Ammar bin Yasir pale washirikina walipomchukua… amma sehemu ambayo inakatazwa Taqiyya ya qauli ni pale itakapokuwa kauli hiyo italeta madhara kwa mwingine, kama kuiua nafsi nyingine, au kukatika kiungo chake, hapo haitajuzu kufanya hiyo taqiya kwa kuwa si halali kwa mtu kuiokoa nafsi yake kwa kumdhuru mwingine”
KUJUZU kubaki chini ya utawala wa madhalimu, na kujuzu kukaa pamoja na wenye kuwakhalifu.
Maibadhi katika wakati huu hawasimamishi baadhi ya hukmu na huduud; kwa kuwa Imam hana uwezo wa kutekeleza hayo, mfano ni kumpiga mawe mzinifu mwenye mke au mme”

Itaendelea wiki ijayo


Khamis bin Yahya bin Khamis Alghammawi
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

 

-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

[2] - Alsaalimi, Abdullah bin Humeid: Bahjatul an-waar sharh an waarul uquul fii Tawhiid, chapa ya nne, Maktabat Imaam Nuruddiin Alssaalimi, Seeb, 2003m uk 165 – 166 kwa uchambuzi.

[3] - Alwuheibi, Musallam bin Salim: Alfikrul aqadiy indal ibadhiyyat hattaa nihaayatil qarni thaani l hijri, chapa ya kwanza, Maktab Dhaamiri, Seeb, 1427h/2006m uk 408 - 409 (( kwa uchambuzi))

 

 

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment