Ibadhi.com

03: MWENDO WA MAIBADHI KATIKA KUSIMAMISHA UADILIFU

 

NURU YENYE KUNG'AA KATKA NJIA YA UADILIFU


MWENDO WA MAIBADHI KATIKA KUSIMAMISHA UADILIFU


MJUKUU: Allah mtukufu anizidishie sehemu ya elimu yako ewe babu yangu na aninufaishe kwayo.. na ulikuwaje mwenendo wa Maibadhi katika kutekeleza sharia ya Allah mtukufu na kusimamaisa uadilifu katika ardhi wakati wa dola ya Amawiyya ?
BABU: Waislamu –wakiwemo Maibadhi-walijaribu kurejesha upindaji huu na kurudisha hukmu katika njia yake ya sawa, amma kwa kuwaambia wafalme na watawala warudi katika kushikamana na hukmu za kiislamu au kwa kuibadilisha dola yenyewe kwa kubadilisha nidhamu ya hukmu”
Na hivi ndivyo ilivyokuwa, Maibadhi walijitahidi na wakapambana kwa ajili ya kutekeleza Uimam adilifu, ambao wanaamini ni lazima kwa mujibu wa itikadi yao, kwa dalili za Qur-an na Sunnah na makubaliano ya Ummah.
MJUKUU: Ndio, ewe babu yangu, nimesoma kuwa Maibadhi wameweka Masharti zinazohusiana na uimamu, kama ambavyo wanalo neno la “Masaalikuddin”, Basi nakuomba unifafanulie yote hayo na unifafanulie ewe babu yangu
BABU: Ndio ewe Mwanangu,ili uwe katika ubainifu, na ili kuondosha uzito wowote uliopo nitakufafanulia kuhusu uimamu, na nitakuelezea njia wanazozichukua kufikia kusimamisha uimamu adilifu.
MJUKUU: Allah mtukufu akuzidishie elimu babu yangu, nami nina kiu sana ya kujua upambanuzi wa mambo haya
BABU: Jua ewe mwanangu… kuwa “Uimamu, Ukhalifa, Uamiri, na Uraisi, ni maneno tofauti yenye maana yenye kuwafiqiana kwa maana ya pamoja. Huo ni uraisi wa pamoja wa mambo ya dini na dunia kwa mtu aitwaye IMAMU, nao ni ukhalifa wa Mtume sallallahu alayh wasallam- katika kusimamisha dini, kuhifadhi mipaka ya dini kwa wenye kuhusika nayo, na kwa hivyo wanaamrishwa raia wote kumfuata na kumtii maadam hajaamrisha kumuasi muumba. Hivyo kazi ya msingi ya uimam ni kusimamisha dini na kutekeleza hukmu za dini na kuhifadhi umoja wa kiislamu na kuutetea ummah. Nazo ndizo kazi za Mtume –sallallaahu alayh wasallam- baada ya kupewa utume mpaka alipofariki, basi kila aliyekamata kazi hizi anazingatiwa kuwa ni khalifa wa Mtume –sallallahu alayh wasallam- katika kuchunga mambo ya ummah huu”
Jua ewe Mwanangu – Namuomba Allah mtukufu aangazie uoni wako kwa haki- kuwa “mpangilio wa kiibadhi umesimama kimsingi katika kuitazama jamii, maana yake ni kuipa uzito wa uhakika rai ya jamii katika kila jambo miongoni mwa mambo ya jamii. Na hili limechaguliwa na Maibadhi kutokana na kufahamu kwao vizuri sharia ya kiislamu ihimizayo Shura, kwa ajili hii Masheikh au wanachuoni wa kiibadhi ndio wenye kumiliki utawala wa mambo, nao ndio wenye haki ya kumkosoa Imam, kumchunga na kuhakikisha kufuata kwake sharia, nao ndio wenye haki ya kumuuzulu akijaribu kuchupa mipaka, kama ambavyo inawajibika juu ya Imam kuwaomba ushauri wanachuoni katika anayoyasimamia.
Na hivi ndivyo inavyokubainikia ewe mwenye kutafuta uongofu kuwa msingi wa shura na kushirikiana ni msingi wa fikra ya kisiasa ya kiibadhi, bali ni upambanuzi wa roho ya Madrasa ya kiibadhi, na katiba ya kiibadhi inasema kuwa Shura kwa Imam ni Lazima, akiipinga anakuwa kafiri - wa neema sio wa kutoka katika uislamu – sawa akiwa ni mwananchuoni au dhaifu” Itaendelea makala ijayo….


Khamis bin Yahya Alghammawi Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

__________________________________________________

- Marejeo yaliyopita uk 56
-Alwuheibi, Musallam bin Salim: Alfikrul aqadiy indal ibadhiyyat hattaa nihaayatil qarni thaani l hijri, chapa ya kwanza, Maktab Dhaamiri, Seeb, 1427h/2006m uk 405 (( kwa uchambuzi))
- Marejeo yaliyopita, uk 405 ((kwa uchambuzi))

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment