Ibadhi.com

II. Salaa zilizocheleweshwa bila ya sababu.

Salaa zilizocheleweshwa bila ya sababu ni Salaa zile zilizizo cheleweshwa kwa ajili ya uzembe au uvivu au sababu nyingine ambazo hazikubaliwi kisheria. Na kuchelewesha Salaa kwa uzembe au kwa uvivu au bila ya sababu iliyo ruhusiwa kisheria ni madhambi makubwa. Inabidi Salaa ile ilipwe na aliye ichelewesha atubu.  Ikiwa Salaa zilizo chelewesha ni nyingi basi atazilipa zote wakati ule aliokumbuka isipokuwa wakati ulio haramishwa kusaliwa Salaa. Na ushahidi wakulipa Salaa, ni kwamba kama vile mtu anavyotakiwa kulipa saumu alizoacha, au zaka, ni kiasi hicho hicho kwa Salaa. Kwani hilo ni deni mbele ya Mwenyezi Mungu, na deni la Mwenyezi Mungu lina haki ya kulipwa kwanza kuliko madeni mengine. Kutoka kwa Ibn Abbaas kasema, "Kasema Mtume S.A.W., “[1]

فَاللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ.

 Maana yake, “Deni la Mwenyezi Mungu lina haki ya kulipwa”.

Namshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuniwezesha kuandika juzu ya pili ya vitabu vya Fiqh. Na kwa vile masuala ya Salaa ni mengi na nimeyaeleza kwa muhtasari, hayakuweza yote kuenea katika kitabu hiki. Kwa hali hiyo nimeyagawa katika sehemu mbili, sehemu ya pili ya kitabu cha Fiqh cha Salaa yaani juzu ya tatu ya vitabu vya Fiqh itakuwa kama ifuatavyo kwa mukhtasari:

1.Salaa ya Jamaa na  hukumu zake. 2. Imam wa Salaa, hukumu na shuruti zake. 3.  Namna ya kusimama wakati wa Salaa. 4. Salaa ya Ijumaa, hukumu na shuruti zake. 5. Salaa ya safari hukumu na shuruti zake. 6. Muda wa safari na maana ya safari. 7. Salaa ya maiti shuruti na hukumu zake. 8. Salaa za Sunna muakkada, za Idi, Witri, sunna za alfajiri, magharibi, tahiyatu masjid, na kadhalika. 9. Salaa zilizo mandub, Salaa za dhuha, taraweh, Salaa ya kuomba mvua. 10. Salaa za nafla, Salaa za usiku, 11.Salaa ya kuomba ushauri kwa Mwenyezi Mungu, na kadhalika. Sijdat sahau na sijdat tilawa. Misikiti haki zake na fadhila zake. Na mambo mengineyo Inshaallah. 

 

والله ولي التوفيق

 DUA.

NAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ALIETUKUKA ATUANDIKE SOTE PAMOJA MIONGONI MWA WAJA WAKE WALE WALIOTUBIA, NA ATUJAALIE KATIKA WAJA WAKE WANAOMWABUDU BILA YA  KUMSHIRIKISHA, NA KATIKA KUNDI LAKE LENYE KUFAULU NA KATIKA VIPENZI VYAKE WAMWOGOPAO, AMIN.

EWE MWENYEZI MUNGU TUNAKUOMBA UTUTENGENEZEE DINI YETU AMBAYO NI KINGA YA MAMBO YETU, NA UTUTENGENEZEE DUNIA YETU AMBAYO YAKO MAISHA YETU, NA UTUTENGENEZEE AKHERA YETU AMBAYO NDIYO MAREJEYO YETU. AMIN.

EWE MWENYEZI MUNGU TUNAKUOMBA USITUACHILIE TUKIWA NA DHAMBI YOYOTE ILE ILA UMEISAMEHE, NA WALA MGONJWA KATI YETU ILA UMEMREJESHEYA AFYA YAKE, NA WALA ALIYEPOTOKA NJIA ILA UMEMWONGOZA, NA WALA ALIE ADUI KWETU ILA UMETUKINGA NAYE, NA UMEMTOSHELEZA[1] Ahmad 5/285 (3224). Mfano wa Hadithi hii imetolewa na Bukhariy 22/293 (6771). 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment