Ibadhi.com

I. Salaa zilizocheleweshwa kwa sababu maalum.

Salaa zilizocheleweshwa kwa sababu maalum ambazo haziko katika uwezo wake bila ya kukusudia, kama vile Salaa zilizocheleweshwa kwa sababu ya usingizi, kusahau, au kusali bila ya kuwa na tohara kamili na baadae mtu akakumbuka baada ya muda wa Salaa ile kupita. Salaa za namna hii zinasaliwa mara tu mtu anapokumbuka. Kasema Jaabir bin Zaid R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W., [1]

مَنْ نَسِيَ صَلاَةً أَوْ نَامَ عَنْهَا فَلْيُصَلِّهَا إِذَا ذَكَرَهَا.

Maana yake, “Atakaesahau Salaa au akalala mpaka Salaa ikampita basi aisali atakapoikumbuka.” Na mtu hahisabiwi dhambi kwa kutokukusudia kuichelewesha Salaa. Kasema Ibn Abbas R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W.,[2]

رَفَعَ اللَّهُ عَنْ أُمَّتِي الْخَطَأَ وَالنِّسْيَانَ، وَمَا لَمْ يَسْتَطِيعُوا، وَمَا أُكْرِهُوا عَلَيْهِ .

Maana yake, “Ameusamehe Mwenyezi Mungu umma wangu makosa (Bila ya kukusudia) na kusahau na mambo wasioyaweza kuyafanya na mambo waliolazimishwa kuyafanya.”

 [1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/56 (184), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Ibn Maajah 2/390 (690), At-Ttirmidhiy 1/296 (162), Ddaaramy 1/305 (1229), Nnasaai 2/469 (611).

[2] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/251 (794), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Ibn Maajah 6/215 (2033).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment