Ibadhi.com

7. Dua baada ya Kushuhudia kabla ya kutoa salam.

Inapendeza baada ya Ttahiyatu ya mwisho na kabla ya kutoa salam kuomba dua. Kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W. Kasema Abdillah R.A.A., “Mtume S.A.W alikuwa akitufundisha kusema ttahiyatu halafu anatuambia,[1]

ثُمَّ يَتَخَيَّرُ مِنْ الدُّعَاءِ أَعْجَبَهُ إِلَيْهِ فَيَدْعُو.

Maana yake, “Halafu na achague katika dua inayompendeza na aombe.” 

Zifuatazo ni baadhi ya dua zilizothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W ambazo alikuwa akiziomba na alizo wafundisha baadhi ya Masahaba wake kabla na baada ya kutoa salam, basi ni bora na inapendeza mtu kuziomba kama ifuatavyo:

 

I. Kasema Abi Masoud R.A.A., “Mtume S.A.W. alitujia katika seble (ukumbi) wa Sa`ad bin `Ubaadah, Bashiyr akamwambia Mtume S.A.W., “Mwenyezi Mungu ametuamuru tukusalie basi vipi tukusalie?” Akanyamaza kimya mpaka tukasahau kama kamuuliza “(Halafu) Akasema, “Semeni,[1]

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا صَلَّيْتَ عَلَى إِبْرَاهِيمَ وَعَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ وَبَارِكْ عَلَى مُحَمَّدٍ وَعَلَى آلِ مُحَمَّدٍ كَمَا بَارَكْتَ عَلَى إِبْرَاهِيمَ وَعَلَى آلِ إِبْرَاهِيمَ فِي الْعَالَمِينَ إِنَّكَ حَمِيدٌ مَجِيدٌ.

Allahumma salli ala Muhammad, wa ala ali Muhammad, kama sallaita ala Ibrahim, wa ala ali Ibrahim, wa barik ala Muhammad wa ala ali Muhammad, kama barakta ala Ibrahim wa ala ali Ibrahim, fi l`alamiina innaka Hamidun Majid. 

Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu mpe Rehema Muhammad na watu wake, kama ulivyompa rehema Ibrahim na watu wake. Na umbarikie Muhammad na watu wake, kama ulivyombarikia Ibrahim na watu wake. Wewe ndiye unastahiki kuhimidiwa[2] na kila kiumbe, na ndiye Mwenye Utukufu.”

II. Kasema Abdillah R.A.A., “Mtume S.A.W alikuwa akitufundisha kusema Ttahiyatu halafu anatuambia,[3]

ثُمَّ يَتَخَيَّرُ مِنْ الدُّعَاءِ أَعْجَبَهُ إِلَيْهِ فَيَدْعُو.

Maana yake, “Halafu na achague katika dua inayompendeza na aombe.”

III. Kasema Ibn Abbas R.A.A., “Alikuwa Mtume S.A.W. anatufundisha dua hii kama vile Sura katika Quraani,[4]

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جَهَنَّمَ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَسِيحِ الدَّجَّالِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الْمَحْيَا وَالْمَمَاتِ .

Allahumma inni a’udhu bika min adhabil-qabr, wa audhubika min adhabi Jahannam, wa a’udhu bika min fitnatil`-Masiyhid-dajjaal[5]. Wa audhubika min fitnatil mahya wal`mamat.

Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu wangu mimi najikinga Kwako na adhabu za kaburini, na najikinga kwako  na adhabu ya jahanamu, na najikinga Kwako dhidi ya fitna za Masihi-dajjaal, na najilinda Kwako dhidi ya majaribio[6] ya uhai[7] na fitna ya mauti[8].

 

IV. Kasema Sayyidna Abu Bakar R.A.A. kumwambia Mtume S.A.W., “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nifundishe dua niombe wakati wa Sala akasema, [9] “Sema, “

اللَّهُمَّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي ظُلْمًا كَثِيرًا وَلا يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلا أَنْتَ فَاغْفِرْ لِي مَغْفِرَةً مِنْ عِنْدِكَ وَارْحَمْنِي إِنَّك أَنْتَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ.

Allahumma inni dhalamtu nafsi dhulman kathiiran, wala yagh`firu dhunuuba ila Anta, fagh`fir li maghfiratan min indika war`rahmni Innaka Annta l`Ghafuuru Rrahiim.

Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu mimi nimeidhulumu nafsi yangu dhulma nyingi, na hakuna mwenye kusamehe madhambi isipokuwa Wewe, nisamehe msamaha kutoka Kwako, na unirehemu Wewe ndio Mwenye Kusamehe na Mwenye Kurehemu”.

 

V. Kasema Ali bin Abi Talib R.A.A, “Kasema Mtume S.A.W., “Halafu aseme mwisho baina ya tashahadu na salam, [10]

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أَخَّرْتُ وَمَا أَسْرَرْتُ وَمَا أَعْلَنْتُ وَمَا أَسْرَفْتُ وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي أَنْتَ الْمُقَدِّمُ وَأَنْتَ الْمُؤَخِّرُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ.

Allahumma gh`firli ma qaddamtu wama akh`khartu, wa ma asrarutu, wa ma a`alantu wa ma asraftu, wa ma anta a`alamu bihi minni antal muqadimu wa an`nta muakhiru La ilaha illa ant.

Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe madhambi yangu niliyoyafanya, na ambayo niliyo ya bakisha nyuma[11], yaliyo ya siri, na yaliyo ya wazi, na yote yale niliyovuka mpaka, na ambayo Wewe unayoyafahamu zaidi kuliko mimi. Wewe unavitanguliza vitu, na Wewe unaviakhirisha[12]. Na hakuna Mungu mwingine anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe”.

 

VI. Kasema Abi Saleh kutoka kwa baadhi ya Masahaba wa Mtume S.A.W. kuwa, "Mtume S.A.W. kasema kumwambia mwanamume mmoja aliemuuliza aseme nini katika Sala? akamwambia, "Sema, [13]"

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ الْجَنَّةَ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ النَّارِ.

Allahumma inni as`aluka l`jannata wa audhubika minn-naar.

Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu mimi nakuomba pepo na najikinga Kwako na moto".

 

8. Kuomba dua baada ya kutoa salam katika Salaa.

Inapendeza kuomba dua baada ya kumalizika kwa Salaa baada ya kutoa salam. Wakati huo ni wakati mzuri wa kukubaliwa dua haraka. Na huu ndio uliokuwa mwenendo wa Mtume S.A.W. na pia aliwahimiza Masahaba wake kufanya hivyo. Na kama vile ilivyothibiti ndani ya Quraani. Kasema Mola Mtukufu. Katika Surat Inshiraah aya ya 7 na 8, “

﴿فَإِذَا فَرغتَ فَانصب ﴿ وَ إِلَى  رَبِّكَ فَارغَب.

Maana yake, “Basi ukishamaliza (kulingania) shughulika (kwa ibada) (yaani kuomba dua). Na jipendekeze kwa Mola wako.”

Zifuatazo ni baadhi ya dua zilizothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W.:

I. Kasema Thauban R.A.A., “Alikuwa Mtume S.A.W. baada ya kumaliza Sala anastaghfiru mara tatu (yaani kuomba kusamehewa madhambi) (ana weza kusema"ASTAGHFIRU LLAH") halafu anasema,[14]

اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلامُ وَمِنْكَ السَّلامُ تَبَارَكْتَ ذَا الْجَلالِ وَالْإِكْرَامِ.

Allahumma anta ssalam, waminka ssalam, tabarkta dha l`jalaali wal`ikram.

Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu Wewe ndiye Mwenye salama, na Kwako iko salama, Umetukuka. Ewe Mola Mwenye utukufu na ukarimu.” 

II. Kutoka kwa Mughaira Ibn Shuubah R.A.A. kasema, “Alikuwa Mtume S.A.W. akisema kila baada ya Sala za faridha,[15]

لَا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ اللَّهُمَّ لا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ.

La ilaaha illa Llahu, Wahdahu la shariika lahu, lahu L`Mulk wa lahu l`hamdu, wa huwa ala kulii shayi`n Qadiir. Allahumma la mania lima Aa`tayta, wala Mu`utia lima mna`ata, wala yanfau dha l`jaddi minka l`jaddu.

Maana yake, “Hakuna Mungu anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Peke Yake hana mshirika, Naye Ndiye Mwenye Ufalme, na Mwenye kustahiki sifa njema na shukrani zote; Naye ana uwezo wa kila kitu. Ewe Mwenyezi Mungu hakuna anayeweza kuzuia Uliempa na hakuna anayeweza kumpa Uliye mzuwilia, na mwenye utajiri hawezi kunufaishwa na utajiri wake[16].”

III. Kasema Abu Huraira R.A.A., “Baadhi ya Muhajirina waliokuwa masikini walimwendea Mtume S.A.W. wakasema, “Matajiri wana daraja ya juu na watapata pepo ya kudumu.” Mtume S.A.W. akawauliza, “Kwa vipi?” Wakasema, “Wanasali kama tunavyosali, na wanafunga kama tunavyofunga, na wanatoa sadaka, na sisi hatuna cha kutoa sadaka, na wanawaachia watumwa uhuru, na sisi hatuna watumwa wa kuwaachia huru.” Mtume S.A.W. akajibu akasema, “Jee nikufundisheni kitu ambacho mkifanya mtaweza kuwafikia wale walio kupiteni? Na mtawashinda wale walio nyuma yenu?, isipokuwa wale tu watakaofanya kama mtakavyofanya, au zaidi wao watakuwa bora kuliko nyinyi.” Wakasema, “Ndio.” Akajibu Mtume S.A.W. akasema,[17]

تُسَبِّحُونَ وَتَحْمَدُونَ وَتُكَبِّرُونَ خَلْفَ كُلِّ صَلاةٍ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ.

Maana yake, “Msifuni Mwenyezi Mungu, na mshukuruni Mwenyezi Mungu, na Mtukuzeni Mwenyezi Mungu, baada ya kila Sala (ya Faridha) mara thalathini na tatu. Na hii inakuwa kwa kusema: (SUBHANA ALLAH mara 33)(ALHAMDU LILLAH mara 33)(ALLAHU AKBAR mara 33).

IV. Kutoka kwa Abu Huraira R.A.A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W., [18]

مَنْ سَبَّحَ اللَّهَ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاةٍ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَحَمِدَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَكَبَّرَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ فَتْلِكَ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ وَقَالَ تَمَامَ الْمِائَةِ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ غُفِرَتْ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ.

Maana yake, “Atakaye sabih katika kila Sala mara 33 (Kumtakasia kwa kumsifu) (SUBHANALLAH)  na atakaye Mshukuru mara 33 (ALHAMDU LILLAH)  na atakaye Mtukuza mara 33 (ALLAHU AKBAR) na mwishowe akasema LAA ILAHA ILLA LLAHU, WAHDAHU LA SHARIKA LAHU, LAHUL MULKU, WALAHUL HAMDU, WA HUWA ALAA KULLI SHAYN KADIYR. (“Hakuna Mwenyezi Mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah. Yeye ni peke Yake hana Mshirika yeyote yule. Ufalme wote ni Wake, sifa njema na shukrani zote ni Zake, Naye Ana uwezo wa kila kitu”. Basi mtu akisema hivi anafutiwa madhambi yake hata kama ni mengi kama mapovu ya bahari.”

V. Kusoma ayat Kursiy[19].

VI. Kusoma Surat al Ikhlas` na Surat al Falaq na Surat NNaas. Kutoka kwa Ukba bin Aamir R.A.A. kasema,[20]

أَمَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ أَقْرَأَ بِالْمُعَوِّذَاتِ دُبُرَ كُلِّ صَلاةٍ.

Maana yake, “Mtume S.A.W. aliniamrisha kusoma Al Muawwidhat baada ya kila Sala.” (Yaani Qul huwa Llahu Ahad, na Surat Falaq, na Surat Naas).

 

VII. Kasema Abu Zubair, "Ilikuwa Abdullah bin Zubair akisema katika kila Sala anapotoa salamu, [21]"

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ لَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَلَا نَعْبُدُ إِلَّا إِيَّاهُ وَلَهُ النِّعْمَةُ وَلَهُ الْفَضْلُ وَلَهُ الثَّنَاءُ الْحَسَنُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ.

La ilaaha illa Llah, Wahdahu la shariika lah, lahu L`Mulk wa lahu l`hamdu, wa huwa ala kulii shay`in Qadiir. La hawla wala quwwata illa Billah, la ilaha illa Llahu wala na`abudu illa iyyaah, walahu ni`imatu, walahu l`fadh`lu, walahu th`thanaa`u l`hasanu, la ilaha illa Llahu mukh`lisiina lahud-diina walau kariha l`kaafiruun. 

Maana yake, "Hapana Mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, Peke yake hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake sifa njema na shukrani, Nae ana uwezo wa kila kitu, hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa vinatokana na Allah. Hapana Mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, wala hatumuabudu isipokuwa Yeye, ni Zake neema na ni Zake fadhila, na ni Zake sifa nzuri. Hapana Mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, hali ya kumtakasia dini Yake, hata kama watakereka makafiri".

 

VIII. Kasema Muadh bin Jabal R.A.A., “Siku moja Mtume S.A.W. alinishika mkono na akaniambia, “Ewe Muadh mimi nakupenda.” Nikamjibu, “Mimi pia nakupenda ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Akasema, “Nakuusia ewe Muadh usiache kusema kila baada ya Sala, [22]

اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ.

Allahumma ainni ala dhikrika wa shukrik, wa husni ibaadatik.  (Aseme mara tatu).

Maana yake, "Ewe Mwenyezi mungu, nisaidie katika kukutaja, kukushukuru, na kuifanya ibada yako kuwa bora[23]".

 

IX. Kasema Ali bin Abi Talib R.A.A., "Mtume S.A.W. akitoa salam anapomaliza Sala anasema, [24]"  

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي مَا قَدَّمْتُ وَمَا أَخَّرْتُ وَمَا أَسْرَرْتُ وَمَا أَعْلَنْتُ وَمَا أَسْرَفْتُ وَمَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي أَنْتَ الْمُقَدِّمُ وَأَنْتَ الْمُؤَخِّرُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ.

Allahumma gh`firli ma qaddamtu wama akh`khartu, wa ma asrarut, wa ma a`alantu wa ma asraftu, wa ma anta a`alamu bihi minni antal muqadimu wa an`ta l`muakhiru La ilaha illa ant.

Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe madhambi yangu niliyoyafanya, na ambayo niliyo ya bakisha nyuma[25], yaliyo ya siri, na yaliyo ya wazi, na yote yale niliyovuka mpaka, na ambayo Wewe unayoyafahamu zaidi kuliko mimi. Wewe unavitanguliza vitu, na Wewe unaviakhirisha[26]. Na hakuna Mungu mwingine anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe”.

 

X. Kutoka kwa Muslim bin Abi Bakar kutoka kwa baba yake kasema, “Mtume S.A.W. alikuwa akisema kila baada ya Sala, [27]

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الكُفرٍ وَ الفَقرِ وَ عَذَابِ الْقَبْرِ.

Allahumma inni audhubika minal`kufri, wal`faqri, wa adhabi l`qabri.

Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu mimi najikinga Kwako na kukufuru, na ufakiri, na adhabu ya kaburi".

 

XI. Kasema Mus`aab, "Alikuwa Sa`ad anaamrisha mambo matano kujikinga nayo, na akisema, "Alikuwa Mtume S.A.W. anayaamrisha kwa kusema,[28] "  

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ الْبُخْلِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ الْجُبْنِ وَأَعُوذُ بِكَ أَنْ أُرَدَّ إِلَى أَرْذَلِ الْعُمُرِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ فِتْنَةِ الدُّنْيَا يَعْنِي فِتْنَةَ الدَّجَّالِ وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ الْقَبْرِ.

Allahumma inni a’uwdhu bika minal-bukhli, wa audhu bika minal-jubni, wa audhu bika min an uradda ila ardhalil ‘umur, wa audhu bika min fitnatid-dduniya wa adhaabil-qabri.

Maana yake, "Ewe Mwenyezi Mungu wangu, najikinga Kwako na ubakhili, na najikinga Kwako na uoga, na najikinga Kwako na kurudishwa katika umri wa uzee wa kudhalilika[29], na najikinga Kwako na fitna za dunia[30] na adhabu za kaburi".

 

XII. Kasema Abi Baraza, "Alikuwa Mtume S.A.W. akitaka kuinuka kutoka katika kikao anasema,[31] "

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ.

Subhanaka Allahumma wa bihamdika, ash`shahadu an laa ilaha illa anta astagh`firuka wa atub ilaiyka.

Maana yake, "Kutakasika ni Kwako Ewe Mwenyezi Mungu, na sifa njema na shukrani zote ni Zako, nashuhudia kwamba hakuna Mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe, nakuomba msamaha, na narudi Kwako".[1] Ttirmidhiy 11/9 (3144).

[2] Kutukuzwa, kushukuriwa.

.[3] Bukhary 3/335 (791)

[4] Al Rabi`u 1/198 (490), mfano wa Hadithi hii imetolewa na Abu Dawud 3/166 (834), Ibn Maajah 3/157 (899), Muslim 3/246 (924).

[5] Mtume wa uongo na hii ni fitna ambayo kailezea Bwana Mtume S.A.W. kuwa ni fitna kubwa ambayo hitotokea fitna kubwa kuliko hio ulimwenguni.

[6] Fitna, mitihani.

[7] Makusudio ya mitihani anayopata mwanadamu wakati wa uhai yamefafanuliwa zaidi katika Hadithi iliyotolewa katika mlango wa “Kujikinga na deni”.

[8] Kuepushwa na mwisho mbaya wakati wa kufa.

[9] Bukhary 3/333 (790).

[10] Muslim 4/169 (1290), Ttirmidhiy 11/300 (3343).

[11] Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Al Infitwaar aya ya 5, "Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilichobakisha nyuma". Wamesema Ibn Masoud, na Akramah na At`taa na wengine katika kuilezea aya hii kuwa ni vitendo vizuri alivyoviacha ambavyo waliendelea baada yake kuvifanya, na ilichobakisha nyuma ni shari alioiacha ambayo wataendelea kufanya baada yake. Mfano mtu kwa kutumia simu yake akasambaza habari za uongo zikaendelea kuzagaa baada yake, au ya wale ya wasanii yanayochusha ambayo yanajenga katika jamii na kuendelea kufanyiwa kazi, au kajenga sehemu ya maasi kama vile ya ulevi. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat alA`nkabut aya ya 13, “Na hapana shaka wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao. Na kwa yakini wataulizwa Siku ya Kiyama juu ya waliyo kuwa wakiyazua”. Pia kasema katika Surat An nah`l aya ya 25, “Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba!”.

[12] Kwa elimu Yako na hekima Yako.

[13] Abu Dawud 2/446 (672).

[14] Muslim 3/254 (931), mfano wa hadithi hii imetolewa na Abu Dawud 4/308 (1292), Ibn Maajah 3/178 (914), Ttirmidhiy 2/4 (275).

[15] Bukhary 3/348 (799), Muslim 3/257 (934).

[16] Imekusudiwa haumfalii mwanadamu utajiri wake, wala hadhi yake, wala heshima yake, wala utukufu wake mbele ya Mwenyezi Mungu, kwani akitaka Mwenyezi Mungu limfike jambo baya basi hakuna kinga ya kuzuia, hata akiwa tajiri au mwenye nguvu. Kasema Mwenyezi Mungu katika Surat Imraan aya ya 26 Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye, na humtukuza umtakaye, na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikononi mwako. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu. Wewe huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku. Na humtoa hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Na unamruzuku umtakaye bila ya hisabu". Amri yote iko katika mikono ya Mwenyezi Mungu".

  

[17] Bukhary 3/347 (798).

[18] Muslim 3/262 (939).

[19] Tuh`fat Al`Abrar, mlango wa dua na adhkar baada ya kutoa salamu ukarasa 147.

[20] Abu Dawud 4/319 (1302). Ahmad 35/286 (16776).

[21] Muslim 3/258 (935), Ahmad 32/333 (155533).

[22] Abu Dawud 4/318 (1301), Ahmad 45/96 (21103).

[23] Kuikamilisha kama jinsi vile ulivyoiamrisha.

[24] Abu Dawud 4/306 (1290).

[25] Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Al Infitwaar aya ya 5, "Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilichobakisha nyuma". Wamesema Ibn Masoud, na Akramah na At`taa na wengine katika kuilezea aya hii kuwa ni vitendo vizuri alivyoviacha ambavyo waliendelea baada yake kuvifanya, na ilichobakisha nyuma ni shari alioiacha ambayo wataendelea kufanya baada yake. Mfano mtu kwa kutumia simu yake akasambaza habari za uongo zikaendelea kuzagaa baada yake, au ya wale ya wasanii yanayochusha ambayo yanajenga katika jamii na kuendelea kufanyiwa kazi, au kajenga sehemu ya maasi kama vile ya ulevi. Kasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat alA`nkabut aya ya 13, “Na hapana shaka wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao. Na kwa yakini wataulizwa Siku ya Kiyama juu ya waliyo kuwa wakiyazua”. Pia kasema katika Surat An nah`l aya ya 25, “Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba!”.

[26] Kwa elimu Yako na hekima Yako.

[27] Sahih Ibn Haziima 1/367 (747).

[28] Bukhary 19/454 (5888).

[29]  Kuwa mzee sana mpaka kujishindwa kimaumbile na kupoteza fahamu.   

[30] Fitna za masih dajjal.

 

[31] Abu Dawud 12/496 (4217). [1] Bukhaari 3/335 (791)

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment