Ibadhi.com

III. Kufahamu kibla nae yuko ndani ya Salaa.

Ikiwa wakati wa Salaa kaelekea sehemu ya kibla ambayo siyo sahihi kwa makosa bila ya kukusudia, akafahamishwa upande sahihi iliopo kibla nae bado yuko ndani ya Salaa, basi Atageuka kuelekee sehemu iliyo sahihi ya kibla bila kukatiza Salaa yake, na wala hana dhambi na Salaa yake InshaAllah ni sahihi. Kutoka kwa Ibn Umar R.A.A. kasema, [1]

بَيْنَمَا النَّاسُ بِقُبَاءَ فِي صَلاَةِ الْفَجْرِ إِذْ جَاءَهُمْ آتٍ فَقَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ أُنْزِلَ عَلَيْهِ اللَّيْلَةَ قُرْآنٌ وَأُمِرَ أَنْ يَسْتَقْبِلَ الْكَعْبَةَ، فَاسْتَقْبَلُوهَا وَكَانَتْ وُجُوهُهُمْ إِلَى الشَّامِ، فَاسْتَدَارُوا إِلَى الْكَعْبَةِ وَهُمْ يُصَلُّونَ.

Maana yake, “Wakati watu walipokuwa Quba ndani ya Salaa ya Alfajiri, aliwajia mtu mmoja akasema, “Usiku wa leo, Mjumbe wa Mola ameteremshiwa aya ya Q`uraani na ameamrishwa aelekee L-Ka`aba, basi nanyi elekeeni upande huo, na wakati ule nyuso zao zilikuwa zimeelekea upande wa Sham, wakageuka kuelekea L-Ka`aba na ilhali wamo katika Salaa wanasali.”

 [1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/67 (207), mfano wa hii imetolewa na Bukhaari 2/164 (388), Muslim 3/119 (820), Ahmad 12/201(5664).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment