Ibadhi.com

II. Asie fahamu wapi kibla.

Ikiwa anayetaka kusali hafahamu wapi kibla kilipo, basi anaruhusiwa kukisia kwa maarifa aliyo nayo kwa kuangalia jua, mwezi au dira, au akauliza watu. Baada ya kutumia jitihada zake akawa amefanya makosa, anakuwa hana kosa na Salaa yake ni sahihi. Kasema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Al-Baqara aya ya 115 kasema, “

﴿وَللهِ المَشرِقُ وَالمَغرِبُ فَأَينَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجهُ اللهِ.

 

Maana yake, “Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuwamrisheni Mwenyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu.” 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment