Ibadhi.com

I. Vipi kuelekea kibla.

Kwa wale walio ndani ya Masjid Al-Haram wao wataielekea Al-Kaaba, ama yule anaye sali nje ya msikiti atauelekea msikiti mtukufu yaani Masjid al Haram, na yule anaye sali nje ya mji wa Makka basi ataelekea sehemu iliopo Makka. Kasema Abu Huraira R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W.,[1]

مَا بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ قِبْلَةٌ.

Maana yake, “Baina ya Mashariki na Magharibi kibla.”

 

II. Asie fahamu wapi kibla.

Ikiwa anayetaka kusali hafahamu wapi kibla kilipo, basi anaruhusiwa kukisia kwa maarifa aliyo nayo kwa kuangalia jua, mwezi au dira, au akauliza watu. Baada ya kutumia jitihada zake akawa amefanya makosa, anakuwa hana kosa na Salaa yake ni sahihi. Kasema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Al-Baqara aya ya 115 kasema, “

﴿وَللهِ المَشرِقُ وَالمَغرِبُ فَأَينَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجهُ اللهِ.

Maana yake, “Na Mashariki na Magharibi ni ya Mwenyezi Mungu. Basi mahala popote mgeukiapo (alikokuwamrisheni Mwenyezi Mungu mtazikuta) huko radhi za Mwenyezi Mungu.”

 [1] Ibn Maajah 3/289 (1001), At-Ttirmidhiy 2/74 (313).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment