Ibadhi.com

18. KUELEKEA KIBLA.

Kuelekea kibla wakati wa Salaaa ni sharti ya lazima kukamilika kwa Salaa. Kasema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil-Baqara aya ya 144, “

﴿قَد نَرَى تَقَلُّبَ وَجهِكَ فِى السَّمآَءِ فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبلَةً تَرضَـهاَ فَوَلِّ وَجهَكَ شَطرَ المَسجِدِ الحَرَامِ وَحَيثُ مَاكُنتُم فَوَلُّواْ وُجُوهَكُم شَطرَهُ,.

Maana yake, “Kwa yakini tukiona unavyogeuza geuza uso wako mbiguni. Basi tutakugeuza kwenye kibla ukipendacho. Basi geuza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu (Al Kaaba), na popote mnapokuwa basi zielekezeni nyuso zenu ulioko (msikiti huo).”

Kabla ya kuanza kuelekea Masjid Al Haraam (Makka) wakati wa Salaaa, Waislamu walikuwa wakisali kuelekea Masjid al Aqsa iliyoko Al Quds, Palestine. Kasema Ibn Abbas R.A.A.,[1]

فُرِضَتْ عَلَيْهِ صَلَوَاتُ الْخَمْسِ قَبْلَ هِجْرَتِهِ بِنَحْوِ سَنَتَيْنِ، وَصَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى بَيْتِ الْمَقْدِسِ بَعْدَ هِجْرَتِهِ سَبْعَةَ عَشَرَ شَهْرًا، وَكَانَتِ الأَنْصَارُ وَأَهْلُ الْمَدِينَةِ يُصَلُّونَ إِلَى بَيْتِ الْمَقْدِسِ نَحْوَ سَنَتَيْنِ قَبْلَ قُدُومِ النَّبِيءِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَيْهِمْ، وَكَانَ النَّبِيءُ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَّى إِلَى الْكَعْبَة بِمَكَّةَ ثَمَانِيَ سِنِينَ إِلَى أَنْ عُرِجَ بِهِ إِلَى بَيْتِ الْمَقْدِسِ ثُمَّ تَحَوَّلَ إِلَى قِبْلَتِهِ.

Maana yake, “Alifaridhishwa (Mtume S.A.W.) Salaa tano kabla ya kuhama kwake kwenda Medina kwa kiasi cha miaka miwili, na alisali Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kuelekea Baitul Maqdis baada ya Hijra yake kwa muda wa miezi kumi na saba, Ma`ansary na watu wa Madina walikuwa wakisali kwa kuelekea Baitul Maqdis kiasi cha miaka miwili kabla ya kuja kwake Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kwao (Madina). Na alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. akisali kuelekea L-Ka`aba kule Makka kwa muda wa miaka minane mpaka alipopelekwa Baitul Maqdis, halafu tena akaelekea kunako kibla chake.”

 

 [1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/67 (206), mfano wa Hadithi imetolewa na At-Ttirmidhiy 10/22 (2888), Bukhaari 1/71 (39), Ahmad 37/452 (17765). 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment