Ibadhi.com

7. Tohara ya mahali pakusalia.

Mahali pa kusalia panatakiwa pasiwe na aina yoyote ile ya najasa, na wala pasiwe ni sehemu ambayo uchafu unatupwa pale. Imethibiti kutoka kwa Mtume S.A.W. kuwa kakataza Salaa zisisaliwe makaburini, machinjioni, kwenye mazizi ya ngamia, barabarani, majaani (unapotupwa uchafu), vyooni, na sehemu zozote zile zilizo na najasa.

Kasema Ibn Abbas R.A.A., "Kasema Mtume S.A.W, [1]

لاَ صَلاَةَ فِي الْمَقْبَرَةِ، وَلاَ فِي الْمَنْحَرَةِ  وَلاَ فِي مَعَاطِنِ الإِبِلِ، وَلاَ فِي قَارِعَةِ الطَّرِيقِ.

Maana yake, “Hakuna Salaa katika makaburi, wala machinjioni, wala kwenye mazizi ya ngamia, na wala katikati ya barabara.”  Pia Ibn Umar R.A.A. kasema, [2]

نَهَى أَنْ يُصَلَّى فِي سَبْعَةِ مَوَاطِنَ فِي الْمَزْبَلَةِ وَالْمَجْزَرَةِ وَالْمَقْبَرَةِ وَقَارِعَةِ الطَّرِيقِ وَفِي الْحَمَّامِ وَفِي مَعَاطِنِ الإِبِلِ وَفَوْقَ ظَهْرِ بَيْتِ اللَّه.

Maana yake, “Amekataza Mtume S.A.W., Salaa kusaliwa katika sehemu saba: Sehemu inayotupwa uchafu, na machinjioni, na makaburini, na njiani na chooni, na sehemu wanayo kaa ngamia, na juu ya Al-Kaaba (kwa vile atakuwa hana kibla)”. Salaa inajuzu kusaliwa kila sehemu iliyo safi na juu ya ardhi.

Kasema Ibn Abbas R.A..A., “Kasema Mtume S.A.W., [3]

جُعِلَتْ لِيَ الأَرْضُ مَسْجِدًا وَتُرَابُهَا طَهُورًا.

 Maana yake, “Imejaliwa kwangu (na umma wangu) ardhi kuwa ni msikiti (yaani unaweza kusali juu yake), na udongo wake ni tahir (safi kwa kutayammam).

 

Pia Jabir R.A.A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[4]

حَيْثُمَا أَدْرَكَتْكَ الصَّلاةُ فَصَلِّ وَالأَرْضُ لَكَ مَسْجِدٌ.

Maana yake, “Mahali popote itakapokukuta Salaa basi usali, na ardhi kwako ni msikiti.”

 [1] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/95 (293), mfano wa Hadithi imetolewa na Abu Daawud 1/141 (92), Ibn Maajah 1/482 (392).  .

[2] Ibn Maajah 2/456 (739), At-Ttirmidhiy 2/79 (316).

[3] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/52 (167), na mfano wa hio imetolewa na Abu Daawud 2/81(413), Ibn Maajah 2/199 (560), At-Ttirmidhiy 2/32(291).

[4] Muslim 3/105 (808), Ibn Maajah 2/464 (745), Bukhaari 11/152 (3115), Ahmad 35/373 (21468).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment