Ibadhi.com

II. Kuingia wakati wa Salaa.

Kuingia wakati wa Salaa ni sharti ya lazima ya kutimia kwa adhana. Kasema Malik, “Kasema Mtume S.A.W.,[1]"

إِذَا حَضَرَتْ الصَّلاةُ فَأَذِّنَا ثُمَّ أَقِيمَا ثُمَّ لِيَؤُمَّكُمَا أَكْبَرُكُمَا.

Maana yake, “Ikifika wakati wa Salaa muadhini, halafu mukimu na awaongoze katika Salaa mkubwa katika nyinyi.” (na katika riwaya nyingine aliye bora kuliko nyinyi yaani ubora katika dini na ucha Mungu).”

Inaruhusiwa kwa Salaa ya Alfajiri katika mwezi wa Ramadhani, na Salaa ya Ijumaa kuadhini kabla ya wakati, halafu ikaadhiniwa tena unapoingia wakati wa Salaa. Kasema Ibn Abbas R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W., [2]

إِذَا سَمِعْتُمْ بِلاَلاً فَكُلُوا، وَإِذَا سَمِعْتُمْ ابْنَ أُمِّ مَكْتُومٍ فَكُفُّوا.

Maana yake, “Mkimsikia Bilal (anaadhini), kuleni, na mkimsikia Ibn Maktoum acheni (kula Daku)”.

 [1] Abu Daawud 2/203 (498), Bukhaari 3/6 (594), Ahmad 31/197 (15048).

[2] Al-Imamu Al-Rab`iu 1/130 (319). Mfano wa hii hadithi imetolewa na Bukhaari 22/208 (6706), Muslim 5/381 (1830), Ahmad 8/7 (3472), Abu Daawud 6/293 (2000).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment