Ibadhi.com

V. Ushahidi kutoka katika Hadithi za Mtume S.A.W.

Hadithi iliyo hadithiwa na Ibn Masoud R.A.A. kasema, “Kasema Mtume S.A.W.,[1]

سِبَابُ الْمُسْلِمِ فُسُوقٌ وَقِتَالُهُ كُفْرٌ.

 Maana yake, “Kumtukana Muislamu ni ufasiki na kupigana nae vita ni ukafiri.”  Na wanavyuoni wote wamekubaliana kwamba Muislamu kupigana na Muislamu mwenzake ni katika maasia makubwa. Lakini kitendo hicho hakimtoi mtu katika Uislamu. Kama ilivyothibiti katika Surat H`ujuraat aya ya 9, “

﴿وَإِن طَآئِفَتَانِ مِنَ المؤمِنِينَ اقتَتَلُواْ فَأَصلِحُواْ بَينَهُما.

Maana yake, “Na ikiwa makundi mawili katika Waislamu yanapigana, basi fanyeni suluhu baina yao.” Pia kasema Abu Huraira R.A.A., “Kasema Mtume S.A.W.,[2]

اثْنَتَانِ فِي النَّاسِ هُمَا بِهِمْ كُفْرٌ الطَّعْنُ فِي النَّسَبِ وَالنِّيَاحَةُ عَلَى الْمَيِّتِ.

Maana yake, “Watu wawili miongoni mwa watu wana ukafiri: anaye mkashifu mtu kuhusu ukoo wake, na anaelia kwa kumuombolezea maiti”.

Kwa ushahidi huo maibadhi wanasema sio kila anaetenda kosa kubwa linafikia daraja ya kufur shirk, na kumpelekea kumtoa katika uisilamu.

 [1] Ibn Maajah 11/427 (3929), Nnasaai 12/477 (4036), At-Ttirmidhiy 7/255 (1906), Muslim 1/202 (97).

[2] Muslim 1/207 (100).

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment