Ibadhi.com

E. KULELEWA KWAKE NA BABA YAKE MDOGO BWANA ABU TALIB

Bwana Abdul Muttalib alipoona ajali yake imefika, aliwakusanya wanawe waliokuwa wakubwa, akawausia kufanya wema juu ya ndugu zao wadogo – Bwana Abbas na Bwana Hamza –. Bwana Hamza alikua ni kijana wa miaka 12, na alitokea kuwa shujaa mkubwa wa ajabu na akausaidia sana Uislamu kwa cheo chake mbele ya Makureshi na  kwa ushujaa wake wakati wa vita. Ama Bwana Abbas alikuwa ni kijana wa miaka 11 tu, na mwisho naye alisilimu na akawa baba wa ukoo wa Banil – Abbas (Abbasides).

 

Halafu baada ya kuwausia haya alimchagua Bwana Abu Talib na Bwana Zubeyr – mahalisa wa Bwana Abdullah, baba yake Mtume (s.a.w.) – akawataka wao ndio wamchukue Mtume (s.a.w.) wamlee, lakini akae katika nyumba ya Bwana Abu Talib chini ya mikono ya mkewe, Bibi Fatma bint Asad bin  Hashim bin Abd Manaf. Watu hawa wawili walifuata vilivyo wasia wa baba yao. Bwana Abu Talib alikua ni mtu wa heshima kubwa mbele ya Makureshi, kwani yeye ndie aliyerithi utukufu wa baba yake, lakini alikuwa masikini sana. Alitokea kumpenda sana Mtume (s.a.w.), hata akitaka kuwagaia tunu watoto wake, kwanza humtanguliza yeye Mtume (s.a.w.), akamchagulia kilicho kizuri, ndipo akawapa wengine. Alikuwa hendi popote ila pamoja naye, kwani Mtume (s.a.w.) hakuwa akipenda sana kucheza na watoto kama yeye. Kutwa alikuwa pamoja na Bwana Abu Talib.

 

Mwanamke huyu Bibi Fatma alikuwa akitukuzwa sana na Mtume (s.a.w.). Hata siku alipokufa, Mtume (s.a.w.) mwenyewe aliteremka kaburini pamoja na mtoto wa marehemu huyu, naye ni Sayyidna Ali

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment