Ibadhi.com

7. WENGI WANAPOONA IBADHI.COM WANAHISI TUNAJIENGUA.

Tumepokea ujumbe unaosema:

Wengi wanapoona ibadhi.com wanahisi tunajimegua.

Asalamu alaykum warahmatullahi wabarakatuh.

Tunawashauri waanzilishi/wanaotumia ibadhi.com wabadilishe jina na kuwa Istiqama.com au linalokaribiana.

Tusameheni ila tunajaribu tulete umoja wa ummah badala ya makundi ya madhahid.

JAWABU:

Kwanza: Tunafurahi kupata ujumbe wenu na sisi tunaupokea kwa furaha na ukunjufu na tunasema haihitaji samahani, Allah mtukufu awalipe kwa juhudi zenu kila la kheri.

Pili: Ushauri wenu tunaupokea kwa mikono miwili, nao upo katika meza yetu na tunashukuru sana kwa ushauri nzuri.

Tatu: Sisi hatuoni ubaya wowote wa kutumia jina la Ibadhi.com kwa sababu jina ni kiwakilishi tu, kwa hiyo mazingatio ni katika yale yaliyowakilishwa na lile jina.

Nne: Kuwepo madhehebu tofauti ni dharura ya kuhifadhi mafundisho ya vyuo tofauti na athari zake na kuhusika kila upande na mafundisho yake; kwa hiyo hatuoni ubaya wa kuwepo Ibadhi.com ikiwa tu itakuwa mbali na mafundisho ya kuusambaratisha umma na kuujengea uhasama baina ya wafuasi wake.

Tano: Sisi tunaamini kuwa ibadhi.com ni chuo cha kufikisha mafundisho ya Uislamu kupitia kwa wanavyuoni wa Madhehebu ya Ibadhi na kutegemea msingi ya ibadhi katika utoleaji wa dalili.

Sita: Ama kuhusu suala la umoja, kwa hakika Ibadhi.com haipingi umoja wa umma wala haina siasa ya kuvunja umoja wa umma, bali ibadhi.com inahimiza umoja wa umma kwa misingi ya kushikamana katika tuliyokubaliana na katika yenye tofauti kila upande uhusike na majukumu yake.

Saba: Ibadhi.com msingi wake ni Haki kwa dalili mkono kwa mkono hadi peponi.

Kwa hiyo hisia za kujimegua ni hisia batili, na hisia sahihi ziwe za kujenga umma kwa kueneza mafundisho sahihi na ya haki kwa mujibu wa dalili.

Asante sana.

Sh. Hafidh Al-Sawafi

Website: ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment