Ibadhi.com

11. SEMA IMEKUJA HAKI - SIRAATI NA MIZANI

 


MWANAFUNZI: Basi nini maana ya Sirati, na je kuna khilaf baina ya madhehebu kuhusu uhakika wake ?
SHEIKH: Umesoma Tungo ya Ghayatul muraadi…. Siraati Ewe mwanangu ni dini ya Allah mtukufu; Uislamu, ambayo inamuwajibikia mwanadamu kuipita, na dalili ya hayo ni kuwa Allah mtukufu ameiita ni njia iliyonyooka, kama alivyosema: “Tuongoe njia iliyonyooka” Alfaatiha: 6 nayo sio njia ilowekwa juu ya Jahannam wanapita juu yake wapitaji kama zisemavyo baaadhi ya madhehebu, amma riwaya zilokuja zinazosema ni daraja kama ukali wa upanga, au kama unywele ulotandazwa juu ya moto wa Jahannam, na ati watu watatofautiana katika kuvuka, wapo watakaovuka kama umeme, au kama pepo, wengine kwa kutembea, wengine kwa kukimbia, na wengine wataporomoka katika moto wa Jahannam; ikiwa zitasihi riwaya hizo basi hizo zimepigiwa mfano tu wa kutofautiana watu katika kuifuata dini ya Allah mtukufu hapa hapa duniani.
MWANAFUNZI: Na vipi kuhusu Mizani ?
MWALIMU: Anasema Allah mtukufu: “Na Siku hiyo kipimo –mizani - ni Haki.” Aaraf : 7
Basi mizani Ewe mwanangu siyo mizani ya vitu kama mizani ya dunia, hiyo ni mizani ya kimaana, maana yake ni haki na uadilifu, wala sio vyombo viwili vitiwe ndani yake matendo ya waja.
MWANAFUNZI: Uzuri ulioje wa nuru ya Haki inapomuangazia mwenye uoni, ikamuongoza katika njia ya sawa!, Hamu yangu ilioje ya kujizidshia faida zako ewe sheikh wangu, lakini nakhofia kukutia uzito, Allah mtukufu akujazi kila la kheri.
SHEIKH: Jua ewe mwanangu kuwa mapenzi yako makubwa ya kuitafuta haki, na jitihada yako katika kufuata uhakika, ni jambo lenye kufurahisha, na linabashiria kheri, Basi Allah mtukufu akithirishe walio mfano wako, na kila sifa njema ni za Allah mtukufu ambaye kwa neema yake mema yanatimia.


MWISHO:

Ewe -mtafutaji elimu- ikiwa unataka kushindana na mwanafunzi huyu mwenye akili, basi kunywa kutoka vitabu vya kiarabu vifuatavyo:
1. Alkhalili, Ahmed bin Hamed Alkhalili: Sharh ghaayatil muraad fii Nadhmil iitiqaad, 1424h/2003m
2. Alkhalili, Ahmed bin Hamed Alkhalili: Alhaqqu daamigh, chapa ya kwanza, Muscut, 1409h/1989m.
3. Alsaalimi, Abdullah bin Humeid: Bahjatul An-waar sharh An-waaril uquul fii tawhiid, chapa ya nne, Maktabat Imaam Nuruddin Alsaalimi, Siib, 2003m.
4. Aljaabiri, Farahaat: Albuudul hadhwaari lil-aqiidatil ibaadhiyyah, chapa ya mwanzo, 1408h, 1987m.
5. Almasqari, Nasir bin Matar: Al-ibaadhiyyah fii Maidanil haqq, chapa ya tatu, maktabatul anfaal, Muscut, 1429h/2008m
6. Alwuhaibi, Musallam bin Salim: Alfikr al-aqadiy indal Ibaadiyyah hattaa nihaayatil qarn thaani lilhijrat, chapa ya mwanzo, Maktabat dhaamiri, Siib, 1427h/2006m.

Kwa kuzidisha maarifa yako, rejea vitabu vifuatavyo ((Kwa Kiswahili))


1. HISTORIA YA MADHEHEBU YA IBADHI cha Sh. Abdallah bin Humeyd Albahri, chapa 1, 2013, Madrasat Shaqsiy Zanzibar
2. Historia ya Ibadhi cha Sh. Issa Altiwani chapa 1
3. IBADHI NA SUNNI – UCHAMBUZI WA TOFAUTI cha sh. Hafidh Alsawwafi, 1425h/2001m Bujumbura, Burundi. (( hakijachapishwa, lakini kinapatikana mitandaoni ))
4. HAKI KWA DALILI cha Sh. Abdallah Alshueli
5. MADHEHEBU YA MWANZO YA KIISLAMU cha Abdulaziiz Almaawali Tarjama Khamis Alghammawi
6. UFUPISHO WA DALILI ZETU KATIKA KUTOONEKANA ALLAH MTUKUFU cha Sh. Hafidh Alsawwafi upangaji wa Khamis Alghammawi
7. HOJA ZENYE NGUVU KATIKA KUTOONEKANA MWENYEZI MUNGU cha Sh. Juma Almazrui
8. FIMBO YA MUSA jz 1 na Jz 4 cha Sh. Juma Almazrui


Kuwasiliana na mtunzi wake kwa lugha ya kiarabu: Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

kuwasiliana na mtarjimu: Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona. , Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Waweza kupata tarjama hii kupitia link hii

Kwa video utapata tarjama hii katika youtube www.youtu.be/NI7qDSN6uKK
Ni vizuri kutembelea tovuti hizi za kiarabu:

1. www.baseera.net,
2. www.almajara.com,
3. www.ibadiyah.net,
4. www.waleman.com,
5. www.nafosa-net.com,
6. www.youtube.com/user/YUONIS88

WALHAMDULILLAHI RABBIL AALAMIINA

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment