Ibadhi.com

10. SEMA IMEKUJA HAKI - HUKMU YA ALIYEKUFA NA MADHAMBI MAKUBWA

 

HUKMU YA ALIYEKUFA NA MADHAMBI MAKUBWA


SHEIKH: Allah mtukufu akubaarik ewe mwanangu, Je unaijua hukmu ya Qur-an kwa wenye kufanya madhambi makubwa ?
MWANAFUNZI: huenda sijalifaham swali lako ewe mwalimu wangu, nifafanulie vizuri kwa hisani yako
SHEIKH: Ewe mwanangu, wapo katika watu wanaamini kuwa mwenye madhambi makubwa ataingia motoni kwa siku zenye kuhesabika na kutoka, kwa sababu wanasema inamtosha mtu katika kuamini kusema tu, amma vitendo ataadhibiwa kwa kiasi chake.

MWANAFUNZI: Vipi itakuwa hilo hali ya kuwa Allah mtukufu anasema: “Na wenye kumuasi Allah mtukufu na Mtume wake, basi hakika hao watapata Moto wa Jahannamu wadumu humo milele " Jinn:23 pia Allah mtukufu ametueleza kuwa hiyo ni itikadi potofu ya mayahudi na wakristo, Amesema Allah mtukufu “Na walisema: Hautatugusa Moto ila kwa siku chache tu. Sema: Mmechukua ahadi kwa Allah mtukufu? Kweli Allah mtukufu hatokwenda kinyume na ahadi yake. Au mnamsingizia Allah mtukufu mambo msiyo yajua?" Baqarah:80
SHEIKH: Kisha; hakika hilo la kusema watatoka motoni -ewe mwanangu- inampelekea mwanadamu katika kupuuzia maasi, kwani yeye ana matarajio ya kuingia peponi hata kama baada ya kuingia motoni kama wanavyozusha, na hilo halikubaliki kiakili wala kimantiki, na vipi iwe sahihi katika akili jambo ambalo Allah mtukufu kalihukumia kuwa ni haramu, na mwenye kulifanya ni muasi kisha amkirimu pepo !!,
Hebu nambie kwa jina la mola wako unapopitia aya za Qur-an ukiwa ni mwenye kuzingatia, je unakutia lafdhi yoyote ya wazi inayotaja kutoka motoni. Na law ingejuzu hilo basi ingejuzu kutoka peponi pia, basi tumia akili yako vyema, wala yasikutoe katika haki maandiko ya viumbe.

MASAAIL HAYA YALIPELEKEA MWANAFUNZI KUSOMA VITABU VYA ITIKADI, YAKAMPITIA KICHWANI MASUALA MENGI, AKARUDI KWA SHEIKH WAKE AKISEMA:

MWANAFUNZI: Yamenibainikia mambo mengi nilikuwa siyafahamu, na kuna mambo mengine sijafahamu bado.
SHEIKH: mambo gani ambayo hujayafahamu Ewe mwanangu ?
MWANAFUNZI: Anasema Nuru ya dini, Imaam Abdullah bin Humeid Assaalimi – Allah mtukufu amridhie-
Siraati si njia kama walivyozusha ** wala hesabu ya siku ya qiyama sio kwa namba mfano wa anayesahau.
Basi nini maana ya Sirati, na je kuna khilaf baina ya madhehebu kuhusu uhakika wake ?

Endelea kuwa nasi katika makala ya kumi na moja…
Khamis bin Yahya bin Khamis Alghammawi

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

 

 

Said Al Habsy

Website: https://www.ibadhi.com Email Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
Add comment